Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Habari wanabodi
Nimefuatilia kwa kitambo sana mwenendo wa mfumo wa sheria na utawala nchini kwetu, nimekuja kupata swali linalonipa ukakasi sana sana
KWa tukio la juzi kukamatwa usiku wa manane Dokta W. Slaa na namna tuhuma dhidi yake kwamba upelelezi haujakamilika inaleta picha ya namna vyombo vyetu vya dola vinavyoshiriki matendo ya kigaidi dhidi ya raia.
Tukija mahakamani ambapo imezuia dhamana yake kwa kigezo cha HOFU DHIDI YA USALAMA WAKE... imepelekea kuaminisha korido za sheria kwamba Mahakama ya Tanzania imeshikilia conset ya kila mtuhumiwa anayesimama mbele yake. Tukivuta kumbukumbu ya kijana Thabit Kombo.ambaye ukamatwaji wake ulikiuka misingi yote ya kisheria na haki za binadamu ambapo mahakama ilikatalia dhamana yake kwa sababu zisizo na msingi kabisa.
Tumeona hata kesi mbalimbali za kisiasa nchini zikiendeshwa kama upande wa mahakama ukionesha waziwazi namna ya kupuuza sheria na michakato ya haki.
Sambamba na hilo, tunaona namna ambayo mtanzania yeyote anayeapishwa kuwa rais anavyogeuka kama ndiye final and conclusive wa kila jambo na hata nafsi za watu. Yaani kwa rehema zake anaruhusu nani aishi na nani atolewe roho. Facts zilizopo kwenye kitabu cha Kabendera ni sahihi sasa raia kujiuliza kuwa huyu mungu anayetokana na wizi wa kura na ubakwaji wa demokrasia nchini anatokana na katiba na sheria zetu ama utashi wa vyombo vya dola vilivyoasi katiba na sheria za nchi?
Naomba tuelimishane au nipingwe kwenye mizania hii ya Mahakama kugeuka kuwa adui wa Haki na rais kujipa umugu wa Tanzania.
NB
Najua mnanitafuta na bahati mbaya sana mnautafuta mwili wangu na siyo utu na roho yangu.