Je, maisha ya wahadzabe ni sifa au aibu kwa nchi?

Je, ni kitu cha kujivunia au ni Kitu cha aibu?
Waafrika wote tumetoka huko hayo ndio maisha yetu halisi, wanaishi hawana maji, umeme, shule wala hospitali wala vyombo vya dani kama sahani, chumvi na kisu. Ni wajibu wa Serikali yenu kuwabadilishia mifumo za maisha ili waishi kama Watanzania wengine sio kuja hapa kuwananga, na kuwakejeli ati ni ushamba
 
Hata Mimi sioni faida ya kuwafosi kubadilika, acha waishi kwenye asili yao! Akiamka anaenda kuwinda na ni uhakika hakosi nyani, familia inakula. No vocha, no bili ya umeme, no hospital, no gari, no need for money, everything free.....
Kubadilika ni kuvaa bikini na wanaume kuwa mashoga huku wanaimba "No reform No Election" ndio anavyotaka huyo pimbi wa Lissu Retired 😂😂😂
 
Ni taaswira mbaya sana kwa Taifa.
Hizo picha zinazopigwa na kusambazwa huko duniani zinadharirisha Taifa....

Nasisitiza ni udharirishaji kwa Tanzania kama taifa,
Hakunaga utalii wa hivyo.

Nyerere alisema hii nchi ina maadui watatu...ujinga, umasikini na magonjwa
Ni wajibu wa serikali kuwasaidia hazabe kujinusuru na maadui hao.

Niwape mfano mmoja,
Kuna kipindi katikati hapo kuna mzungu alirekodi filamu ikiwaonyesha Wasukuma wakila skeleton za sangara (wao wanaita panki) zilizokuwa zikitupwa kwny majalala ya viwanda vya samaki.

Wazungu walitushangaa sana iweje wakazi wa jirani na ziwa wakoswe Samaki halafu hapohapo Viwanda vina-export maelfu ya tani za samaki ulaya.

Serikali ya Tanzania ilibidi ijitokeze kukanusha japo ilikuwa ni kweli.
Sasa kwann hizo jamii za kanda ya ziwa zisiachwe na maisha ya kama hazabe.
 
Wazee wa zamani waliishi mapangoni, sasa mambo yamebadilika, nao wabadilike, serikali ijitahidi kuwabadilisha.
 
Serikali itaingiza pesa nyingi? Kuna tofauti gani kati ya hao na mababu zako waliogeuzwa watumwa na maonyesho kama wanyamapori? Unaunga mkono utumwa?
 
Third world [emoji289] country
"Third World" ni neno lililokuwa linatumika kipindi cha cold war kutofautisha nchi ambazo hazipo upande wa USA na The Soviet Union. Unapenda kujiona si chochote kwa vigezo vya wemgine?
 
Wote hatukutoka huko, ni wabara tu, hata ukiangalia sasa hivi utaona hivyo. Watu wapwani walikuwa wanaishi kistaarabu kwa miaka mingi.

Ni uhalisia wala sio chuki za kikabila.
 
Serikali itaingiza pesa nyingi? Kuna tofauti gani kati ya hao na mababu zako waliogeuzwa watumwa na maonyesho kama wanyamapori? Unaunga mkono utumwa?
Yawezekana huelewi maana ya utumwa!

Wahadzabe tangu lini wakawa watumwa?,Wamasai ni watumwa?,Mmasai na muhadzabe wanatofauti gani?
 
Waendelee tu na maisha yao ili waendelee kuwa vivutio ili taifa lipate mapato ya utalii
 
Swali langu:
Je, ni kitu cha kujivunia au ni Kitu cha aibu?
Ni aibu, na sio wahazabe tu hata wamasai maisha yao ni aibu na kinyume na ustaarabu, halafu wavivu na wachafu.
 
Wahadzabe wenyewe wanayachukia? Kama jibu ni hapana, kwanini wabadilishwe? Hukohuko youtube kuna nchi za ulaya na asia, raia wao ni primitive kuliko hata wahadzabe.
 
Wote hatukutoka huko, ni wabara tu, hata ukiangalia sasa hivi utaona hivyo. Watu wapwani walikuwa wanaishi kistaarabu kwa miaka mingi.

Ni uhalisia wala sio chuki za kik
Uko sahihi jamii ya watu wa pwani walikuwa watu wa mwanzoni kufanya biashara na wageni na hatimae kupata mavazi, fedha na chumvi ila sio jamii ya mwanzo kuelimika. Jamii za mwanzo kuelimika ni Wahemiti na Timbuktu huko Ghana ndio maana hapa kwetu hakuna chuo wala alama yoyote iliyoachwa na jamii hiyo kama ukumbusho zaidi ya misikiti walizojengewa ya waarabu .

Wahemiti ndio jamii ya kwanza kugundua na kuvaa nguo.
 
Hivyo vitu ulivyovitaja ndio vinavyotupatia STRESS na mwisho wa siku ukosefu wa afya ya akili, sonona, bifu, usaliti, michepuko hatimaye kesi juu ya kesi, migogoro hadi kifo. WA-HADZABE wameepuka hivyo vitu kwa wingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…