Ikizu Bukama
Senior Member
- Nov 26, 2023
- 183
- 378
Kuanzia
Kuanzia mwanzo sikuona nia ya Samia kuhusu hili,mkuu wa majeshi ile hotuba aliyoitoa pale haikuonyeshwa kuungwa mkono na Amiri jeshi mkuu,kuna hisia napata yuko compromised haswa baada ya ile safari ya M7 na Kagame pamoja na Kabarebe kuja Zanzibar kuonana naye...kumbuka wakati wa ile michuano iliyofanyika Zanzibar,Kabarebe alitia kambi kule alikaa Zanzibar kwa wiki kama moja hiviJe Jeshi la TZ and SA limeshidwa na M23?
Maana tunasikia wanasonga tu. Sasa tumefikia sehemu hizi nchi kubwa kwa ukanda wa huku South wameshindwa na M23. Hii ni hatari sana kupuuza au kwenda kwenye vita nusunusu.
Waandishi wa habari wa Tanzania badala ya kuuliza maswali kama haya wanabaki kusifia sifia kila kitu. Yaani miradi yetu ya treni ina maana gani kama hakuna usalama Congo ya mashariki?. Jeshi letu kama halipigani kwa manufaa ya nchi wanabaki kuonyesha misuli kwenye sherehe tu sio powa. Haya ndiyo mambo ambayo jeshi letu linatakiwa kupigania sio kutishia waandamanaji au kusaidia wizi wa kura kwa wapinzani bali kupigania nchi na sio kinyonge nyonge
Watanzania tunabaki kuchekeshwa chekeshwa na serikali kama watoto wadogo. Hii ni dharau kubwa. Hakuna mtu anajua kuhusu mazishi wa wanajeshi, hakuna bendera nusu mlingoti.......... huu ndiyo uzalendo