Wakuu
Nimekuwa nikikutana na madai kwamba maji ya mvua huwa yanaharibika baada ya kuchotwa.
Naomba kufahamu ni kwa nini maji ya mvua huwa yanaharibika baada ya siku kadhaa baada ya kukingwa,na pia huku mitaani kwetu tunayawekea chumvi kidogo kwa iman kuwa hayata haribika,je ni kweli chumvi husaidia maji ya mvua yasiharibike au tunajidanganya tu?🤣
Nimekuwa nikikutana na madai kwamba maji ya mvua huwa yanaharibika baada ya kuchotwa.
Naomba kufahamu ni kwa nini maji ya mvua huwa yanaharibika baada ya siku kadhaa baada ya kukingwa,na pia huku mitaani kwetu tunayawekea chumvi kidogo kwa iman kuwa hayata haribika,je ni kweli chumvi husaidia maji ya mvua yasiharibike au tunajidanganya tu?🤣
- Tunachokijua
- Uhalisia wa maji ya mvua kuharibika
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa ni kweli maji ya mvua yanaweza kuharibika lakini muda mfupi baada ya kuvunwa lakini si kwamba yenyewe ni mabaya moja kwa moja bali ni kile kinachoingia ndani ya maji hayo baada ya kukingwa.
Kisayansi, maji ya mvua yanaonekana masafi, lakini yanapopita hewani yanaweza kuchukua uchafu kama vumbi, moshi, au kemikali. Baada ya kukusanywa, hasa kwenye vyombo au paa, yanaweza kuchafuliwa zaidi na:
a)Bakteri na vijidudu
b) Kinyesi cha ndege au wanyama
c) Majani na uchafu mwingine
Hivyo hali hii inaweza kusababisha maji hayo kuanza kubadilika haraka kwa kubadilika harufu, ladha, au hata kuwa hatari kiafya.
Mathalani bakteria kama Escherichia coli wanaweza kuingia kwenye maji muda mfupi baada ya kukingwa na hivyo kuzaliana kwa wingi kama maji yatakuwa yamehifadhiwa kwenye joto la kawaida bila kufunikwa vizuri.
Shule ya sayansi ya maji kutokea nchini Marekani kupitia tovuti ya USGS wameandika makala yao ambayo inaelezea namna bakteria haya wanavyoweza kutoka kwenye kinyesi cha wanyama na kuingia kwenye maji.
"Kunywa maji yenye uchafu huu kunaweza kusababisha maradhi makubwa; watoto walio chini ya miaka mitano, watu wenye kinga dhaifu ya mwili, na wazee wako katika hatari zaidi."
Vijijidudu huingiaje kwenye maji ya mvua?
Maji ya mvua yanaweza kukusanya vijidudu na kemikali kutoka hewani na pia yanapoingia kwenye mfumo wa kuyakusanya. Vumbi, moshi, na chembe nyingine angani vinaweza kuyachafua maji ya mvua kabla hata hayajafika kwenye paa lako.
Baada ya mvua kunyesha, kemikali kama asbesto, risasi, au shaba zinaweza kuingia kwenye maji. Kemikali hizi zinaweza kutoka kwenye: Vifaa vya paa, mifereji ya maji, mabomba, pamoja na vifaa vya kuhifadhia maji.
Uchafu na vijidudu kutoka kwenye paa pia vinaweza kuingia kwenye maji ya mvua unayokusanya. Kwa mfano, kinyesi cha ndege kilicho juu ya paa kinaweza kuishia kwenye pipa au tanki la maji ya mvua. Hii inaweza kutokea wakati wowote, lakini huwa rahisi zaidi hasa mvua inaponyesha baada ya siku kadhaa za ukavu.