Je majibu ya utra sound kuhusu jinsia ya mtoto huwa ni %100?

Je majibu ya utra sound kuhusu jinsia ya mtoto huwa ni %100?

ITR

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
7,637
Reaction score
20,676
Mambo vip wajf kama kichwa cha habari hapo juu kinavyo sema, je majibu ya utrasound kuhusu jinsia ya mtoto huwa ni ya uhakika Kwa asilimia 100 au huwa Kuna saa nyingine inakosea?

Maana nisije kununua rundo la nguo alafu jinsia ikatoka tofauti ikala kwangu.
 
kama imefanywa kwenye ujauzito wa miezi 5+ na mtoto alikua amejimanua US haiwezi kudanganya maan jinsia huonekana fresh kabisa
Imefanyika akiwa na miezi 7na wiki 3.
 
Inategemea.

Lakini kujibu swali lako, kutategemea zaidi na umri wa mimba, ubora wa mashine na utalaam wa anayeangalia.

Kuna scenario moja, mtaalam yeye aliona kitovu cha mtoto akajua dudu la kiume. Kumbe mtoto ni wa kike.

So, siyo 100% sure lakini uwezekano huwa ni mkubwa sana pia.
 
Ultrasound haina uhakika wa 100%, huwa kuna nafasi pia ya makosa. Accuracy yake ya kugundua jinsia kwa kawaida huwa ni kati ya 90% hadi 95%.

Makosa huwa yanatokea sana pale ambapo mtoto anakuwa amebana miguu au kitovu kinakuwa kimekaa katikati ya miguu.

Umri wa ujauzito pia unachangia sana kupata majibu sahihi. Ukifanya ultrasound mapema mno, mfano chini ya wiki 18 hadi 20, sehemu za siri za mtoto zinakuwa bado hazijakomaa vizuri. Ni rahisi sana daktari kushindwa kutofautisha kama ni mvulana au msichana.
 
Inategemea.

Lakini kujibu swali lako, kutategemea zaidi na umri wa mimba, ubora wa mashine na utalaam wa anayeangalia.

Kuna scenario moja, mtaalam yeye aliona kitovu cha mtoto akajua dudu la kiume. Kumbe mtoto ni wa kike.

So, siyo 100% sure lakini uwezekano huwa ni mkubwa sana pia.
Alipigwa utra sound mimba ikiwa na miezi 7 na wiki 3.
 
Ndio kwa asilimia kubwa na mtaalamu akiyajua bila kukosea.. Pale kati pale kidwudwu uonekane.. Kama hakipo ni KE na palivyo 😀

Sasa msomaji awe mjuzi haswa kama haoni aseme haoni hiyo sehemu
 
Mambo vip wajf kama kichwa cha habari hapo juu kinavyo sema, je majibu ya utrasound kuhusu jinsia ya mtoto huwa ni ya uhakika Kwa asilimia 100 au huwa Kuna saa nyingine inakosea?

Maana nisije kununua rundo la nguo alafu jinsia ikatoka tofauti ikala kwangu.
50/50 Sisi Daktari alitudanganya tukajiandaa na nguo za kike halafu wife akajifungua wakiume
 
50/50 Sisi Daktari alitudanganya tukajiandaa na nguo za kike halafu wife akajifungua wakiume
Basi ngoja niwe mpole nisubilie mtoto azaliwe kwanza ndo nifanye shopping.
 
Back
Top Bottom