Falsafa ya kwanza ya kuwepo kwa Waziri Mkuu ni Kumkinga Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa nchi. Katika hali ya kawaida ikitakiwa Waziri Mkuu awe Mkuu wa Serikali ili aweze kuwa na nguvu ya kiuongozi ndani ya Serikali. Rais angebaki na Ukuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu. Mtu mwenye vyeo hivyo viwili vikubwa hapaswi kuwa mtu wa kulaumiwa laumiwa na wa kufanya teuzi hadi za Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa.
Kazi ya kuwa Mkuu wa Serikali, kuunda, kuiratibu na kusimamia ingebaki kwa Waziri Mkuu.
Falsafa ya pili ya kuwepo kwa nafasi ya WM Tanzania ni kuusharabu mfumo wetu wa Semi-Parliamentary System. Yaani sisi mawaziri wetu wanakuwa wabunge kabla ya kuwa mawaziri. Mawaziri wetu huwajibika kwa Bunge moja kwa moja ndani ya Bunge. Serikali yetu huwajibika kwa Bunge kupitia mawaziri na hivyo kuhitajika Mkuu wa Shughuli za Serikali.
Falsafa ya 3 ni kuusharabu na kuimarisha mfumo wetu wa Muungano. WM wa TZ ni kama leader of Tanganyika.
Kuhusu misuguano: haiepukiki. Hata bila PM, kungetokea mojawapo wa Mawaziri anakuwa machachari, anatishia nafasi ya Boss.