Je, Makocha wa timu za vijana ni matapeli au ni wachezaji wetu wagumu kuelewa?

oladipo

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2022
Posts
1,885
Reaction score
3,305
Wakuu jana nilipata fursa ya kuangalia mashindano ya under 20 kwa timu za ligi kuu kati ya azam na dodoma jiji. Kiukweli nilichokiona kilinisikitisha sana.

Wachezaji wa under 20 kwa kawaida ungetegemea wawe na viwango kuonyesha wapo tayari kiuchezaji kutokana na umri wao.

Lakini huwezi kuamini wachezaji wa timu zote mbili walikuwa wanastruggle hata kutuliza pasi. Yaani wachezaji karibia wote first touch zao zilikuwa mbovu mno. Kwnye kutoa pasi kwenyewe hawatoi pasi za kueleweka pasi mkaa zilikuwa nyingi sana.

Kwa kifupi wachezaji wote walicheza hovyo sana. Sasa nikajiuliza hawa wachezaji huwa wanafundishwa nini huko mazoezini ikiwa kutuliza tu mpira ni kasheshe?

Je, Wana makocha sahihi wa kuwafundisha mbinu sahihi je makocha hawa wanakidhi viwango au wameokotwa tu mitaani?

Je, nini hatma ya soka letu ambalo kwa kiasi kikubwa limetawaliwa na wageni ikiwa wachezaji wetu wa under 20 tunaowategemea hata kutuliza mpira hawawezi?
 
Si ndio maana team zinapanda ligi na kuanza kuwatumia kina kongwe Sabatho maana huko under 21 hakuna wachezaji wenye kukidhi mtiti wa ligi kuu
Wana viwango vya chini mno. Acha waking Aziz ki wajichotee mipesa maana wabongo hawajitambui hat kidogo
 
Hiyo mechi niliangalia jana,sio wabovu unavyosema,madogo wana ball control hata kumzidi kibu wa kwenye ligi kuu,wana pasi nzuri,umaliziaji tu ndo mbovu kwa timu zote
Hiyo kibu ana nafuu kwa nilichokiona mechi hiyo
 
Utapeli upo nikikumbuka timu ya vijana ya Simba kycha mgosi Kampanga na mwanae hamna kitu
 
Wakuu jana nilipata fursa ya kuangalia mashindano ya under 20 kwa timu za ligi kuu kati ya azam na dodoma jiji. Kiukweli nilichokiona kilinisikitisha sana.

Wachezaji wa under 20 kwa kawaida ungetegemea wawe na viwango kuonyesha wapo tayari kiuchezaji kutokana na umri wao.

Lakini huwezi kuamini wachezaji wa timu zote mbili walikuwa wanastruggle hata kutuliza pasi. Yaani wachezaji karibia wote first touch zao zilikuwa mbovu mno. Kwnye kutoa pasi kwenyewe hawatoi pasi za kueleweka pasi mkaa zilikuwa nyingi sana.

Kwa kifupi wachezaji wote walicheza hovyo sana. Sasa nikajiuliza hawa wachezaji huwa wanafundishwa nini huko mazoezini ikiwa kutuliza tu mpira ni kasheshe?

Je, Wana makocha sahihi wa kuwafundisha mbinu sahihi je makocha hawa wanakidhi viwango au wameokotwa tu mitaani?

Je, nini hatma ya soka letu ambalo kwa kiasi kikubwa limetawaliwa na wageni ikiwa wachezaji wetu wa under 20 tunaowategemea hata kutuliza mpira hawawezi?
Hao wote watoto wa vigogo au wamepata connection tu vipaji halisi vipo mtibwa huko
 
Back
Top Bottom