Kuhusu hili la Issa na Yesu. Sioni shaka nalo.
Mwa imani yangu binafsi sijui wengine.
1: Issa ni jina la Yesu kwa kiarabu sio kiislam. Kama ilivyo John na Yohana kwa kwa kiswahi au kilatini.
2: Maelezo ya Issa wa Kwenye Quran yanaendana japo kwa utofauti na maelezo ya Yesu wa kwenye Biblia na mama yake.
Hivyo naamini Yesu wa kwenye Quran ni toleo jipya la Yesu yuleyule wa kwenye Biblia ila amehafifishwa au kawekwa ili quran isijekuonekana ni kitabu cha Mungu mpya ambaye hana uhusiano na Mungu yule wa wakina Yesu, Yakobo, Musa, Ibrahim na Yohana.
Kwa hiyo Muislam anayemjifunza Issa ni kama anajifunza mwangwi tu au kivuli cha Yesu wa kwenye Biblia. Anatakiwa aje afundishwe vizuri huku kwetu.
Huu ndio ufahamu wangu ambao sikutaka kuuweka wazi mwanzo ili nipate mawazo mapya. Kutokea hapo mkuu unaweza kusema au kuongezea ulichokusudia kusema.