Kilele9
JF-Expert Member
- Jun 1, 2017
- 1,452
- 1,093
Adamoo na wenzake ni makomandoo waliohitimu. Kwa taarifa zilizopo mafunzo ya ukomandoo siyo mchezo.
Ilikuwaje wakanyong'onyezwa na mateso ya polisi yakiwemo kunyimwa chakula, kufungwa kitambaa machoni na kutishwa na bastola iliyoko kiunoni mwa polisi mpaka wakasema wasiyopaswa kusema.
Kama polisi wanawagwaya askari jeshi wa kawaida hawa makomandoo kulikoni?
Ni kweli kuwa mafunzo ya ukomando sio mchezo ndio maana wapo mahakamani wangekuwa wa kawaida,kama wewe, wangekuwa hospitali ,mochuari au wameshazikwa kwa mateso.
Pili uelewe kuwa uchunguzi wa police sio vita na hawakustahili kuteswa wakati wa kuhojiwa/kuchunguzwa.