Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kama mjuavyo, kutokana na namna ya uchaguzi mkuu ulivyofanyika hapa nchini mwaka 2020, hakuna Mbunge yeyote wa upinzani aliyechaguliwa, isipokuwa wawili tu ambao ni yule mama wa Chadema, aliyechaguliwa kutoka mkoani Rukwa na Mbunge mwingine wa upinzani kwa tiketi ya CUF toka mkoani Mtwara.
Kwa kifupi ni kuwa kutokana na mkakati alipokuwa ameuweka Mwendazake, ni kuwa alihakikikisha kuwa hakuna kitu kinachojulikana kama uchaguzi mkuu na badala yake kukawa na "uchafuzi" kwa lengo la kuirejesha nchi yetu kwenye mfumo wa chama kimoja cha siasa tuliokuwa nao hapo awali!🥺
Hata hivyo mbinu hizo za Mwendazake, zilikuwa za kutumia vyombo vya dola, kama vile kuwaengua wagombea wa upinzani, kutoruhusu mawakala wa vyama vya siasa vya upinzani vituoni na hata kuona maboksi ya kura yakiingizwa kinyemela na hao "manjagu" wetu kwenye vituo vya kupigia kura.
Hata hivyo tumeshuhudia baada ya Bunge letu, tunaloweza kudiriki kuliita la mfumo wa chama kimoja, akiibuka Mbunge mmoja wa CCM, wa Jimbo la Kisesa akitema cheche Bungeni, utadhani kuwa yeye anatoka chama cha upinzani hadi amekuwa ni mwiba mkali Sana kwa Mawaziri wa CCM, hadi baadhi ya Mawaziri, wakijikuta wakiweweseka na kujikuta wakinena lugha, kama ambavyo yaliyomkuta Waziri wa chenji, Madeluu, wakati anajibu swali wa wapi zilipo trillion 360 za makinikia?
Ndipo Waziri huyo alipoonekana kama yupo kwenye maombi mazito huku ananena kwa lugha, akitumia lugha yayayayayayayaya.
Hata hivyo, siyo Madelu pekee aliyeonja chungu za Mbunge huyo Luhaga Mpina, bali Mawaziri wengine akina Bashe na Makamba nao "waliingiakwenye 18 zake" na kuonja chungu za Mbunge huyo machachari wa CCM.
Ndipo hapo ninauliza je Luhaga Mpina, ameziba pengo la kambi rasmi ya upinzani Bungeni, iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge Freeman Mbowe wa Chadema?
Hilo ni swali tu naomba majibu, msije mkanipopoa mawe😄