Pre GE2025 Je, Mbunge wako ana hali nzuri hapo Bungeni kuelekea 2025? Wabunge wangu Askofu Gwajima (Kawe) na Jesca (Iringa Mjini) hali ni tete

Pre GE2025 Je, Mbunge wako ana hali nzuri hapo Bungeni kuelekea 2025? Wabunge wangu Askofu Gwajima (Kawe) na Jesca (Iringa Mjini) hali ni tete

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ili kushinda uchaguzi kuna njia nyingi

1000011299.jpg
 
Ni wakati wa kuwaambia ukweli Wabunge wetu kama bado tunahitaji huduma yao 2025 - 2030 au wakatafute Ajira nyingine.

Tumia Uzi huu kutuma salamu kwa Mbunge wako iwe za kumtakia kheri au kumpa angalizo. Sisi Iringa mjini na Kawe tunatarajia kupata Wabunge wapya.

Mungu ni Mwema wakati Wote 😄

Soma Pia:
Wabunge waliobebwa kwa mbeleko mwaka 2020 hali ni tete, Arusha mjini na Mbeya mjini kimeumana
Mahudhurio Bungeni, Wabunge wengine wapo wapi mbona hata majimboni hawaonekani?
Angalau Dr. Gwajima anajitahidi kwenye uwaziri, hata kule jamuhuri ya X anapongezwa sana tofauti na mawaziri wenzake.

Sijajua upande wa ubunge huko kwenu bwashee lakini ameitendea wizara haki na labda inaweza kumbeba kwenye ubunge.
 
Mbunge anaewakilisha Jimbo letu Sasa HIvi namuona Misibani anakuja amevaa shati la kijani na suruali nyeusi,namshauri asitumie kiinua mgongo chake kuhonga Bali awakimbie machawa
 
Askofu Gwajima ni mbunge wa hovyo sana hapo Kawe. Kama wakimpitisha kugombea ubunge mimi siji ng'o kupiga kura.
 
Kuna mbunge huku jimboni yeye anatembelea mashina na wananchi usiku tu mana alipotea ss ivi uchaguzi umekaribia ndo anajidai anaishi uku jimboni....amechelewa sana na atakula aliko peleka mboga
 
Angalau Dr. Gwajima anajitahidi kwenye uwaziri, hata kule jamuhuri ya X anapongezwa sana tofauti na mawaziri wenzake.

Sijajua upande wa ubunge huko kwenu bwashee lakini ameitendea wizara haki na labda inaweza kumbeba kwenye ubunge.

Mkuu huyo mama Ni jembe kwani habetui mabega wala hajui kupinda mdomo kwenye kazi yake full time yupo kazini & active
 
J. Gwajima ni Ajaye 202V ,HATOGOMBEA ubunge.
 
Back
Top Bottom