Serikali ya Tanzania si ya Majimbo, kila taasisi ipo kitaifa, hakuna taasisi za majimbo
Watumishi wa Serikali wanaweza kufanya kazi katika mkoa wowote nchini, bila kujali wanatoka mkoa gani. Kwa mantiki hiyo, fursa za kupata elimu inayowawezesha kuingia kwenye ajira za Serikali zinapaswa pia kuwa na mgawanyo unaozingatia usawa wa kitaifa.
Lakini kumekuwa na hali ya kutokuwepo kwa usawa katika mgawanyo wa vyuo nchini. Kuna mikoa au kanda yenye vyuo vingi, huku baadhi ya mikoa au kanda ikiwa haina hata chuo kikuu cha Serikali.
Matokeo yake, vijana wanaoishi katika maeneo yenye vyuo vingi wanakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata Diploma na Degrees zinazohitajika katika kuomba ajira za Serikali, taasisi kubwa, jeshi na sekta nyingine zinazohitaji sifa za kitaaluma.
Vijana wenye uhaba wa mikoa au kanda zenye vyuo huingia gharama zaidi kwenda kusoma mbali
Hivyo swali si kwa nini watu wanapata ajira kutoka mikoa fulani. Swali ni: Je, Serikali imehakikisha kuwa vijana wa mikoa yote wanapata fursa zinazolingana za kupata sifa zinazohitajika kuingia kwenye “System”?
Kama ajira za Serikali ni za kitaifa, je, fursa za kuzalisha sifa zinazowawezesha Watanzania kushindania ajira hizo hazipaswi pia kuwa na usawa wa kitaifa?
Na kama kuna tofauti kubwa katika mgawanyo wa vyuo, je, huo ni uzembe wa mipango, changamoto ya kihistoria, au kuna jambo la kina zaidi linalopaswa kuchunguzwa?