Je, Mgawanyo wa Vyuo usio na usawa unalenga kuminya baadhi ya mikoa au kanda na kurahisishia wengine kuingia kwenye taasisi, idara, n.k?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Serikali ya Tanzania si ya Majimbo, kila taasisi ipo kitaifa, hakuna taasisi za majimbo

Watumishi wa Serikali wanaweza kufanya kazi katika mkoa wowote nchini, bila kujali wanatoka mkoa gani. Kwa mantiki hiyo, fursa za kupata elimu inayowawezesha kuingia kwenye ajira za Serikali zinapaswa pia kuwa na mgawanyo unaozingatia usawa wa kitaifa.

Lakini kumekuwa na hali ya kutokuwepo kwa usawa katika mgawanyo wa vyuo nchini. Kuna mikoa au kanda yenye vyuo vingi, huku baadhi ya mikoa au kanda ikiwa haina hata chuo kikuu cha Serikali.

Matokeo yake, vijana wanaoishi katika maeneo yenye vyuo vingi wanakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata Diploma na Degrees zinazohitajika katika kuomba ajira za Serikali, taasisi kubwa, jeshi na sekta nyingine zinazohitaji sifa za kitaaluma.

Vijana wenye uhaba wa mikoa au kanda zenye vyuo huingia gharama zaidi kwenda kusoma mbali

Hivyo swali si kwa nini watu wanapata ajira kutoka mikoa fulani. Swali ni: Je, Serikali imehakikisha kuwa vijana wa mikoa yote wanapata fursa zinazolingana za kupata sifa zinazohitajika kuingia kwenye “System”?

Kama ajira za Serikali ni za kitaifa, je, fursa za kuzalisha sifa zinazowawezesha Watanzania kushindania ajira hizo hazipaswi pia kuwa na usawa wa kitaifa?

Na kama kuna tofauti kubwa katika mgawanyo wa vyuo, je, huo ni uzembe wa mipango, changamoto ya kihistoria, au kuna jambo la kina zaidi linalopaswa kuchunguzwa?
 
Kuwa wazi kabisa taja mikoa au kanda zinazoathirika na mgawanyo huu.
 
Kuwa wazi kabisa taja mikoa au kanda zinazoathirika na mgawanyo huu.
Kanda ya ziwa hakuna hata chuo kimoja cha serikali.kanda ya kati pia ukiondoa udom ambayo ilijengwa sababu tu ya kuwa ni makao makuu.sa100 kaamu a kuanzisha ujenzi wa chuo kikuu kule zanzibar
 
Sioni mantiki kanda ya ziwa kuna vyuo vingi sio lazima vya serkali na wasomi wengi tu. Dodoma ni chuo kikubwa kuliko vyote nchini.
 
Swala la vyuo kuwa upande au kanda fulani sidhani kama ni tatizo, tatizo linakuja labda kwenye aina za ajira. Pengine ungezungumzia kuna baadhi ya jamii zinapata ajira zenye mshahara mkubwa au mashirika na taasisi nyeti huku jamii zingine pamoja na kuwa na uwezo hawawezi kupenya kwenye hizo ajira na hata wakipenya ni wachache mno. Kwani inaweza kuwa ni rahisi kwa mtu wa hali yeyote kufikia chuo popote kilipo ila siyo rahisi kwa mtu yeyote kufikia baadhi ya ajira kirahisi.
 
Kanda ya ziwa hakuna hata chuo kimoja cha serikali.kanda ya kati pia ukiondoa udom ambayo ilijengwa sababu tu ya kuwa ni makao makuu.sa100 kaamu a kuanzisha ujenzi wa chuo kikuu kule zanzibar
Zanzibar chuo kikuu kilikuwepo toka mama akiwa mdogo.Msimsingizie mama wa watu.
 
Mwamko wa kujenga chuo sehemu wakati mwingine inatokana na tabia ya watu wa sehemu hiyo.
Watu wanaendekeza kucheza ngoma na ushirikina unategemea nini.
Pia msije dhani eti chuo kikijengwa sehemu flani wakazi wa eneo hilo watapata fursa kuingia kusoma kiulaini.
Kuingia chuo ni lazima uwe na sifa na vigezo.Sasa utakuta wakazi wa eneo husika hawathamini shule inabidi wadahili wachukue wanaotoka mikoa mingine.
Rejea enzi za mwalimu kufaulu std7 ilitungiwa jina la kisiasa kuchaguliwa.
Nyerere aliibana sana mikoa ya Kilimanjaro na Ziwa magharibi(Kagera).Ili kutoa fursa kwa mikoa mingine kupata elimu.

Walivyokuwa na mwamko wa elimu mikoa hiyo ikaona na isiwe tabu wakajenga shule za kulipia(privates).

Ajabu sasa watu wa mikoa mingine wakawa wanakwenda kusoma Kilimanjaro na Kagera.
 
Serikali imelitelekeza jiji la mwanza vyuo vya serikali ni vichache sana nilitegemea kwa jiji kama hili liwe na chuo kikuu sio vicollege
 
Ndugu zangu mfano think2 Sumaye ameshawahi kukiri walipokosea.Walianzisha vyuo vikuu vingi kama utitiri bila kuzingatia nafasi za ajira.

Vyuo vimekuwa vingi mno ni ajabu eti madaktari na walimu wanakosa kazi?.
Tulikosea sana kuisahau elimu ya vitendo yaani vyuo vya ufundi.mfano VETA. Sina maana havikuwepo ila hatukuvipa kipaumbele.
Waajiri wengi binafsi siku hizi hawahitaji academics wa longo longo.

Nenda migodini utanielewa wanathamini watu wa vitendoNa wakati migodi inafunguliwa ndio walikuwa wa kwanza kuajiriwa.Na ndio walioshika nafasi za uongozi.Nchi zilizoendelea ni kweli wana vyuo vikuu vingi ila hawako nyuma kwenye mafunzo ya amali.Unakuta mzungu anakuambia yeye ana certificate ya diesel engine tu na ana experience ya miaka 20.Je unategemea wewe umemaliza mechanical engineering na yeye nani atachukuliwa? .

Utawala wa Nyerere japo wanafunzi wa vyuo mfano Dar tech walilalamika kwanini iitwe FTC Lakini aliona hilo mbali kuwe na watendaji na viongozi.
Nimefanya kazi migodini nalijua hili na nimeona mengi.
Dunia ya sasa iko kasi hata watoto wetu wakisoma tuone mbali wanasoma nini.Kwa sasa tuko kwenye AI na techno hama.

Sisi unakuta syllabus inamkaririsha mtoto kujua miji mikuu dunia nzima na kimchora panzi.
Nenda Marekani wanafunzi wao hawajui Geography ya dunia nzima ukimwambia unatoka Tanzania anaweza kukuuliza iko Nigeria au Nairobi?.

Study with purpose not as a prestige.
Sikatai big brains kusoma elimu za juu hawa wataalamu tunawahitaji pia lakini kwa moderate and low brains wasome kinachowastahili.
 
Unataka kutuaminisha kuwa WALUGURU wa Morogoro wengi wana Ma Degree na Diploma kuwazidi Wahaya wa Kagera na Wanyaki wa Mbeya siyo. Na kwamba Wazaramo na Wakwere wa Pwani na DSM ni wasomi kuliko Wapare wa Same na Mwanga Siyo? na Kwamba sisi Wagogo hapa Dodoma tuna degree za kufa mtu siyo???
 
Mkoa wa Ruvuma ndio umetupwa kabisa kwenye masuala ya vyuo, hakuna chuo kinachotoa Degree,
Duuuh.
Wangoni mrudi kwenu South na Wamakua na Wayao muende zenu Msumbuji na wale Wanyasi waende zao Malawi.🙂🙂🙂 Just a joke. Kuwa na Chuo hakuna uhusiano na kuwa na wasomi wengi. Sisis wagogo hapa Dodoma pamoja na kuwa na vyuo vikongwe hapa mjini kama Mipango, CBE na sasa UDOM na St. John's lakini bado hata darasa la saba tunamaliza kwa taabu sana na kusoma hatujui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…