Je, Mgawanyo wa Vyuo usio na usawa unalenga kuminya baadhi ya mikoa au kanda na kurahisishia wengine kuingia kwenye taasisi, idara, n.k?

Angalaia matokeo ya siku hizi division 4 na 0 ni chache sana, wahitimu wengi wa sekondari wana sifa za kwenda vyuoni lakini wengine ndoto zao zinakatwa kwasababu vyuo vipo mbali, eneo halina exposure ya vyuo, n.k.
 
Mwanza wana SAUT na CUHAS bana labda useme wamekosa chuo kikuu cha serikali.
Saut sio chuo cha serikali na ni kimelenga zaidi kozi za ualimu, sociology, mass communication.

Cuhas ni chuo cha kanisa na kimeelemewa kwa muda mrefu na nafasi chache hivyo kuendelea kulazimu watu wengi sana kwenda mikoa mingine,

Ni muda sasa Serikali ijenge hata chuo kikuu kimoja kikubwa hapo Mwanza

Watu wengi wa Mwanza wanaenda mikoani kwa gharama kubwa kusomea engineering, law, udaktari, computer science, n.k.
 
Kuwa wazi kabisa taja mikoa au kanda zinazoathirika na mgawanyo huu.
Tabora, kigoma, shinyanga, Rukwa na Katavi hapo hakuna chuo hata kimoja walau kina ishu za Mechanical, Electrical, Civil, Computer Science, Uhasibu, Sheria, Ugavi, Finance kwa level ya bachelor degree hii si hatari kabisa.
 
Waluguru pamoja na kuwa na muamko mdogo kwenye elimu lakini uwepo wa chuo ndani ya mkoa umewasaidia kuwapa exposure ya kwenda vyuoni kwasababu ya ease of accessibility, sikuhizi ukienda Mzumbe na SUA kuna waluguru wengi tu mkuu hasa wanaomaliza form 4 wanaunga moja kwa moja diploma, times have changed.

Jiulize kwanza gharama ya Mhaya kutoka Kagera kwenda kusoma Dar kwa kukosa vyuo vya engineering hata Mwanza

Wangejengewa huko Kagera Vyuo basi wengi zaidi wangepata fursa hio.
 
Pia kuna Mr. Thomas alitokea La Grange Illinois U.S.A alikuja Tanzania kwa ishu fulani ilitokea kama expert ukiachana na shahada yake ya uchumi alisomea pia diploma ya heavy duty mechanic na kafanya kazi Electromotive Diesel (EMD) kwa miaka mingi ni expert mchafu mno kwenye diesel engine na electrical systems.
 
Acha kuchafua makabila ya watu for the sake of forcing validation to your point

Pamoja na kuwepo muamko mdogo wa elimu kwa wagogo lakini huwezi kuwashusha kiasi hicho kwa kuwadharau hawajui kusoma na kuandika, have some respect.

Uwepo wa vyuo Dodoma umeleta muamko kwa wanafunzi wanaomaliza form 4 na 6 kwenda katika vyuo vilivyowazunguka, inakuwa rahisi hata kuwashawishi wazazi kupeleka watoto vyuoni.

Zamani ni kweli kulikuwa na tatizo kubwa la jamii nyingi kutoona tija ya elimu lakini sikuhizi watu wanazidi kuona umuhimu wa kupeleka watoto vyuoni, mitandao nayo imechochea sana hata vijana wa mikoa iliyokuwa imedumaa kielimu.

Acha kudharau makabila ya watu mkuu hasa katika kipindi hiki karibia form 4 na form 6 wote mikoa yote wanabutua division 1 hadi 3 na kuwa na sifa za kwenda vyuoni
 
Tabora, kigoma, shinyanga, Rukwa na Katavi hapo hakuna chuo hata kimoja walau kina ishu za Mechanical, Electrical, Civil, Computer Science, Uhasibu, Sheria, Ugavi, Finance kwa level ya bachelor degree hii si hatari kabisa.
Mkuu hio ni point kubwa sana

Sikuhizi wamejenga college za Uhasibu na mambo ya finance lakini bado hakuna vyuo vya sheria, Computer Science, Engineering.

Vijana wanateseka kusafiri umbali mrefu kwa gharama kubwa sana katka mazingira mapya kufuata elimu, Imagine mtu yupo Kagera kule mpakani na Uganda aende kusoma Dodoma, Arusha, Mbeya, au Dar. nauli ya kwenda tu ni kubwa, akifika huko hana mwenyeji aanze kulala kwenye gesti za elfu 5 za uswahilini, bado haujui mji izuri kuna risk nyingi sana, yote hio kwasababu kwao hakuna vyuo.
 
DIT Mwanza. Pia SAUT wanatoa Engineering
DIT Mwanza hakuna hata kozi moja ya Engineering mkuu.

Kile chuo ni kama veta wanatoa kozi za fashion, mambo ya ngozi za wanyama, n.k.
 
Kwani umejua kwamba siyo wa hayo makabila niliyoyataja? kama nimejitaja kwamba kuwepo kwa vyuo hakuna uhusiano na usomi na fursa za ajira nimekosea wapi? Huoni kutoka Kagera kwenda Moshi au Dar au Dodoma ni kusoma tosha maana unakuwa umepata na exposure? Nyie vijana wa leo ndo mnataka kuwa kama kuku wa Kienyeji. Vijana wa zamani kutoka Mara kuja Mazengo Technical na Mgogo wa Dodoma kwenda Tanga Technical, Mdigo wa Tanga kwenda Musoma Technical, Mgoni wa Songea kuja Umbwe na Mchaga wa Msohi kwenda Kigonsera wakati Mfipa wa Rukwa akija Galanos tanga na wa tanga akaenda Kantalamba n.k ilikuwa shule kamili maana inajenga utaifa zaidi kuliko kuwa kuku wa kienyeji.
 
Hata mkoa Mara hakuna chuo cha maana lakini Wajaluo,wajita na wakurya wamesoma sana nchi hii,
Chuo hata kingejengwa lindi kama kinatoa elimu bora watu wangejaa tu,
Bukoba hakuna chuo lakini kuna wasomi wa kutosha,
 
Mkoa wa Ruvuma ndio umetupwa kabisa kwenye masuala ya vyuo, hakuna chuo kinachotoa Degree,
Duuuh.
Hivi degree mtu anaipata kwakua anatokea mkao flani palipo na chuo au ni vigezo vya kufauru tu. Basi Wazaramo na Wagogo ndiyo wasomi wengi nchi hii
 
Kuna ukweli mkubwa kwenye hoja yako, hasa kuhusu umuhimu wa elimu ya vitendo na kuunganisha elimu na mahitaji halisi ya soko la ajira. VETA na elimu ya ufundi ni muhimu sana, na si lazima kila kijana awe degree holder.

Lakini pia kuna kada kama accountants, lawyers, doctors, engineers, procurement officers na nyingine nyingi ambazo, kadri unavyopanda kwenye taaluma na nafasi za kitaaluma, degree na qualifications za juu ni muhimu.

Hapo ndipo hoja ya msingi ilipo: kama Tanzania si nchi ya majimbo, Serikali ni ya kitaifa na ajira zake ni za kitaifa, je, fursa za kupata qualifications zinazowawezesha Watanzania kushindania ajira hizo zimesambazwa kwa usawa kitaifa?

Kuwa na vyuo vingi si kosa lenyewe. Tatizo ni mgawanyo wake na usawa wa fursa. Huwezi kuwa na mkoa wenye vyuo na taasisi nyingi za elimu, huku kijana wa mkoa mwingine akilazimika kusafiri mamia ya kilomita kutafuta chuo, halafu tukasema wote wamepewa fursa sawa kwa sababu tu “hakuna anayezuiwa kwenda kusoma.” Huo si usawa wa fursa.

Kijana wa eneo lisilo na vyuo anaweza kuwa na bidii zaidi, lakini bado anakutana na gharama kubwa za usafiri na maisha, ugumu wa kuwashawishi wazazi wampeleke mbali, kukosa ndugu au mtandao wa kumsaidia huko anakoenda, pamoja na changamoto nyingine za mazingira. Kwa hiyo, haki ya kwenda kusoma inaweza kuwa sawa kisheria, lakini mazingira ya kufikia fursa hiyo si sawa.

Na hapa pia kuna tofauti kati ya private sector na Serikali. Mwajiri binafsi anaweza kuamua kumchukua fundi mwenye certificate ya diesel engine na miaka 20 ya experience badala ya mechanical engineer mwenye degree, kulingana na mahitaji yake. Lakini katika Serikali, qualifications za kitaaluma zina nafasi kubwa katika kuingia kwenye kada, kupanda madaraja na kushika nafasi mbalimbali za kitaaluma na kiutawala.

Kwa hiyo hili si suala la kusema “vyuo ni vingi” au “watu wasome ufundi.” Ni suala la mkakati wa taifa: tunahitaji elimu ya juu, elimu ya ufundi na practical skills, lakini pia tunahitaji kuhakikisha miundombinu na fursa za kupata elimu hiyo zinasambazwa kwa uwiano wa kitaifa.

Tusipange tu watu wasome nini; tupange pia nchi inahitaji wataalamu gani, wapi wanahitajika, na kila kijana atapataje nafasi ya kufikia elimu hiyo bila kubebeshwa gharama zisizo sawa kwa sababu tu amezaliwa mkoa fulani.
 
Sijajua kwa zama hizo kama serikali ilikuwa inalipia gharama lakini kwenda kusoma mikoa au kanda ya mbali kuna gharama za nauli zinazohitajika, lakini pia nje ya hapo hizo shule zilikuwa zenye mabweni na chakula hivyo mtu akifika tu kamaliza.

Huwezi kumlinganisha kijana anaesomea chuo ndani ya mkoa na kijana anaetoka mikoa ya mbali, kuna gharama za ziada nyingi

Pia kuna utofauti wa kumshawishi mzazi ambae yupo mkoa wenye chuo na mzazi ambae inabidi amsomeshe mtoto nje ya mkoa, kwanza huyu anaanza kuwaza safety ya mtoto mazingira mapya hasa kama ni kumsomesha mtoto walemavu wa kike, kwasababu kufikia huko unakuta hakuna hata ndugu wa kumpokea itabidi aanze kulala kwenye gesti za mtaani na kumekuwa na matukio ya wanafunzi wa kike kulazimika kulala kwenye nyumba za watu wasiowajua ili wapate sehemu za kulala wanapokuta hostel zimejaa vyuoni au mkopo umechelewa kutoka hela walizofia nazo zimeisha, jambo linalopelekea wengine kunyanyaswa kingono.
 
Sina hakika kama hapa kuna hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…