Je, Mhe. Rais anayo haja ya kuwa na wasiwasi na mashaka dhidi ya Chanjo ya Corona?

Inategemea na chanjo yenyewe.corona ujanja ujanja mwingi.
Hizo chanjo hata huko ulaya na marekani hawazitaki.
Na Wana mwambia bill gates ndo katengeneza Corona ili apige hela
Gates ndio owner wa Pfizer ?
 
Magufuli anajua sana angalia hapa hao waliochanjwa wanavyo teseka huko.

Mpk Rais aseme tayari anazo taarifa zote

Wanaotaka chanjo waende huko wakachanjwe.

View attachment 1688888
Akae akijua,imebaki miaka 4 tu atupishe.
Huwezi kutawala milele.
Walikuwepo wafalme wengi sana,wenye nguvu mara 1000+ ya kwake,Ila sasa hawapo.
 
Anayembishia ubora wa chanjo bila kutoa scientific evidence.Yaani anachukulia kama siasa tu.

Wewe ukisema hii ni chanjo ya Corona huo ndio uthibitisho wa kisayansi ulioutoa kwenye jamii?

Hujasikia baadhi ya chanjo zinazoathiri watu huko nje ya nchi?
 
Akae akijua,imebaki miaka 4 tu atupishe.
Huwezi kutawala milele.
Walikuwepo wafalme wengi sana,wenye nguvu mara 1000+ ya kwake,Ila sasa hawapo.

Wewe umebakiza miaka mingapi utupishe duniani?

Mbona unawaza kama mtoto wa shule ya msingi anayewaza kuhitimu darasa la saba ili asiwahi namba shuleni
 
Hao waliotoa chanjo wametoa uthibitisho upi wa kisayansi?
Angalia kwenye chanjo hiyo utauona.
Tatizo hata watu wasiojua hata maana ya chanjo wanajadili chanjo.Philosophically, you can't discuss about a thing,which you don't know it's etymology.
 
Angalia kwenye chanjo hiyo utauona.
Tatizo hata watu wasiojua hata maana ya chanjo wanajadili chanjo.Philosophically, you can't discuss about a thing,which you don't know it's etimology.

Chanjo ipi sasa maana zipo kama kumi hivi. Chanjo ya taifa gani?

Hivi unafikiri wewe ndio unajua maana ya chanjo kuliko hao wanaopinga?
 
Inaweze kana akawa NI yeye au Ana mkono wake
Lisemwalo lipo.
Maana ugonjwa wa MAABARA huu.
Lisemwalo lipo ? Unajua mkuu ni mawili kama tunataka hapa kuchangamsha baraza na kuongelea consipiracy theories na story ambazo hazipo substantiated hilo ni jambo moja (ndio maana hata humu kuna Jukwaa la Chit Chat) Ila kama tunaongea mambo serious tunayoyajua yenye vivid evidences naomba unitag tuendelee na mjadala... (unless otherwise kila mtu atakuja na conspiracies zake na mwisho wa siku tutakuwa tunawashutumu watu wasio na hatia....
 
Simple logic ambayo haitaji elimu kiwango cha PhD


Chanjo iliyopo iliqndaliwa kulingana na kirus cha mwanzo sasa kwa hiki kirus jipya haiwez kuwa na ufanis hata Dr tendros sijuj anajua
 
Ndugu yangu umeandika upuuzi mtupu.

Ungefuatilia historia ya magonjwa ya milipuko Dunia, usingeandika huu ujinga. Wenye akili wanajiuliza, kwa nini karibia kila baada ya muda fulani, licha ya jitihada kubwa za Dunia, lazima utokee mlipuko wa kuua watu wengi? Lakini siyo upuuzi huu uliouandika.

Mwaka 1350 - Tauni ilipotangazwa kupata tiba, ilikuwa imeua watu wanaokadiriwa kufikia milioni 25

Mwaka 1980 - ndui ilipotangazwa kupotea, tayari watu si chini ya milioni 300

1817 - Kipindipindu kilianza. Mpaka leo, kimeua zaidi ya watu milioni 50.

1918 - spannish flue iliua watu wanaofikia milioni 39

2020 - Covid 19, tayari imeua zaidi ya watu milioni 2, na inaendelea kuua Duniani kote.

Kwa fikra zako hizi za kipuuzi, magonjwa yote, ni wazungu wanataka kupunguza waafrika ilihali na wao wanakufa? Lazima uwe mpumbavu hasa kuamini hii nadharia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli anajua sana angalia hapa hao waliochanjwa wanavyo teseka huko.

Mpk Rais aseme tayari anazo taarifa zote

Wanaotaka chanjo waende huko wakachanjwe.

View attachment 1688888
Msimpaishe. Hakuna anachojua. Yeye kwa kiasi kikubwa ni mropokaji.

Magufuli ni mtu mwenye self denial. Yeye kila mtu anafikiria ni mtu anayemfikiria vibaya na anayetaka kumtendea ubaya.

Kwa Magufuli, wakenya ni wabaya, wanatuonea wivu.

Wazungu ni wabaya, wanataka kupora mali zetu.

Wapinzani ni wabaya wanataka kumwua.

Wachaga ni wabaya, hawampendi.

Kwake kila mtu ni mbaya. Na watu wenye spirit za namna hiyo huwa wapo. Hawajiamini, kila wakati wanafikiria kuna mtu atawatendea ubaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Apinge kwa evidence sio kuongea kama watu wa vijiweni
Mnataka na chanjo tuichome kwenye oil, kware, na mapapai!? Warudishieni hela zao waliowatuma! Tutapokea chanjo na kuitumia endapo tu tutajiridhisha pasipo shaka kuwa ni salama kwa kizazi chetu cha sasa na vijavyo.
 

Hahahaha! Mkuu hujakosea kwa mtazamo wako, yote uliyoyasema ni sawa kwa mtazamo wako na mna unavyomjua Magufuli, halikadhalika mwingine naye anamjua kivingine.
 
Ili mradi katika nchi zote kubwa duniani Hakuna hata 1 inayopinga hili jiandaeni kisaikolojia.


Tena Bora Trump alikuwa anaipinga WHO ila baada ya Democrats kuchukua mamlaka jiandaeni.
 

Mkuu kila kitu mtu hukiona na kukihukumu kwa mtazamo wake
 
. Wazungu waliwekeza na bado wanawekeza kwenye wataalam wetu hapa nchini, wataalwwam wengi walipewa Scholarship kusomea nje ya nchi, na wengi wakirudi ni vibaraka vya hao mabeberu.
Inasikitisha kwamba tuna watu wenye mtazamo kama wako. Tujiulize bila ya hao unaowaita mabeberu tungekuwa wapi kimaendeleo. Viongozi wengi tunaowapa heshima leo wamesomeshwa na hao unaowaita mabeberu. Mifano ni mingi tukianza na baba wa taifa J. K. Nyerere, hayati Ben Mkapa maprofesa wengi kama Palamagamba Kabudi na wengine nao je ni vibaraka. Ikiwa wote waliosomeshwa na "mabeberu" watakuwa ni vibaraka wao viongozi wangapi watakuwa ndiyo wazalendo wa kuliongoza taifa. Na je wewe unashaurije watu wetu wasiende kusoma nje?
 
Unafikiri kwa nini kuna hayo magonjwa ya Mlipuko kama ulivyoyaita? Ukishajua sababu ndio nitaelewa kuwa wewe ni mtu wa dizaini ipi na uelewa wako upo kwa level ipi
 
Kwa mantiki hiyo basi, hakuna sababu ya kuamini chanjo yoyote dhidi ya magonjwa kama polio na pepopunda kwa kuwa inatoka kwa mabeberu. "It's funny. Is it not?"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…