Je, Mhe. Rais anayo haja ya kuwa na wasiwasi na mashaka dhidi ya Chanjo ya Corona?

Je, Mhe. Rais anayo haja ya kuwa na wasiwasi na mashaka dhidi ya Chanjo ya Corona?

Sio Magufuli tu hata mimi siikubali hyo chanjo.
Huu ugonjwa umekaa kibiashara zaidi.
gonga malimao yako gonga tangawizi zako. Kwisha habari
jina lako linaakisi wewe ulivyo, sawasawa tu na huyo unayemuunga mkono maamuzi yake!
 
Ndugu yangu umeandika upuuzi mtupu.

Ungefuatilia historia ya magonjwa ya milipuko Dunia, usingeandika huu ujinga. Wenye akili wanajiuliza, kwa nini karibia kila baada ya muda fulani, licha ya jitihada kubwa za Dunia, lazima utokee mlipuko wa kuua watu wengi? Lakini siyo upuuzi huu uliouandika.

Mwaka 1350 - Tauni ilipotangazwa kupata tiba, ilikuwa imeua watu wanaokadiriwa kufikia milioni 25

Mwaka 1980 - ndui ilipotangazwa kupotea, tayari watu si chini ya milioni 300

1817 - Kipindipindu kilianza. Mpaka leo, kimeua zaidi ya watu milioni 50.

1918 - spannish flue iliua watu wanaofikia milioni 39

2020 - Covid 19, tayari imeua zaidi ya watu milioni 2, na inaendelea kuua Duniani kote.

Kwa fikra zako hizi za kipuuzi, magonjwa yote, ni wazungu wanataka kupunguza waafrika ilihali na wao wanakufa? Lazima uwe mpumbavu hasa kuamini hii nadharia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ubaya wenu mnasoma historia na kuielewa kwa juu juu!

Yaani sawa kuelezwa jua linatoka mashariki kuelekea magharibi na wewe kujua hilo tu tayaritayari unajiona tayari umeishakuwa "astronomical field guru"! Hautaki kuhoji zaidi kwa nini jua lianzie mashariki...kwa nini lisianzie kusini lakakatiza mashariki ya kati hilo likaelekea kaskazinimagahribi !

Na hautakiwi kujiuliza tu ni kuhakikisha unapata majibu sahihi ya maswali yako!

NARUDI kwenye hoja yako. Je. Umejaribu kujishughulisha kujua chanzo cha maradhi mazito haya kujirudia baada ya muda uliotaja ni nini? Je. Umejaribu kuoanisha tawala za dunia wakati huo wa maradhi yanatokea zilikuwa zinajishughulisha na nini? Na zilkuwa na mahusiano gani?

Mkuu, hutakiwi kujiuliza tu maswali haya bali ni pamoja na kutafuta majibu yake sahihi!

Sasa ujipime mwenyewe "upuuzi wa akili" unao uona kwa wenzako uko chini mara ngapi ya " wa kwako"!
 
Nasikia kuna tafiti iliwahi kufanyika kuhusu IQ za nchi tofauti tofauti Africa, Tanzania tulikua nafasi mbaya; watu kama nyie ndio huenda mlichukuliwa kama sample ya Wabongo; kila kitu kwenu nyie mmegeuza siasa; hata hamjioneagi AIBU nyie wenyewe? Corona inaangalia itikadi ya chama cha mtu? Rais Magufuli ni rais wa ccm au Tanzania?
Mafyatu hao.
 
Akae akijua,imebaki miaka 4 tu atupishe.
Huwezi kutawala milele.
Walikuwepo wafalme wengi sana,wenye nguvu mara 1000+ ya kwake,Ila sasa hawapo.
Miaka 4 ni mingi mkuu,kwani kasema anataka kutawala milele?
 
Unajua Corona ilipotokea?
Unajua kuwa ni UGONJWA wa MAABARA?
Lisemwalo lipo ? Unajua mkuu ni mawili kama tunataka hapa kuchangamsha baraza na kuongelea consipiracy theories na story ambazo hazipo substantiated hilo ni jambo moja (ndio maana hata humu kuna Jukwaa la Chit Chat) Ila kama tunaongea mambo serious tunayoyajua yenye vivid evidences naomba unitag tuendelee na mjadala... (unless otherwise kila mtu atakuja na conspiracies zake na mwisho wa siku tutakuwa tunawashutumu watu wasio na hatia....
 
Mkuu hao jamaa lazima watafanikiwa tu, yani tutake tusitake tutachanjwa.

Kuna habari nimesoma sehem inasema WHO wanampango wa kutoa kadi za chanjo ya korona. (Mfano wa kadi ya chanjo ya homa ya manjano) ambayo itatumika katisa safar ya nchi na nchi, yani asie na kadi hiyo hata safiri kwenda nchi nyingine.

Me naona hapa ndio watatukamata wengi.
Angalia mpango wao hapa juu ya hii dunia
 
Attachments

  • 20210127_225116.jpg
    20210127_225116.jpg
    57 KB · Views: 12
Unajua Corona ilipotokea?
Unajua kuwa ni UGONJWA wa MAABARA?
Unajua maana ya Kujua ?
Au unataka kila mtu alete yeye anavyojua na tukubaliane nae kwamba ni facts ?
Official Reports kuhusu Corona zinasemaje au nichambue conspiracy report moja na tuifanye iwe factual
 
Corona ni virus vilivyotoka MAABARA.
Huo ndo ukweli
Unajua maana ya Kujua ?
Au unataka kila mtu alete yeye anavyojua na tukubaliane nae kwamba ni facts ?
Official Reports kuhusu Corona zinasemaje au nichambue conspiracy report moja na tuifanye iwe factual
 
Maisha ya mwanadamu yamejawa na changamoto nyingi Sana, na nyingi ya changamoto hizo zimetengenezwa na mwanadamu huyo huyo ili kujiletea mazingira rafiki yatakayo muwezesha kuishi kwa jinsi anavyotaka ama kupenda.

Ni kwa namna hio tunaweza kusema Kila alietangulia hutamani asiwepo wa kumfikia na kuficha mbinu alizotumia kufikia hapo alipo.

Nchi za Africa na hata hapa kwetu Tanzania tumekua miangoni mwa wenye kuathirika na athari zitokanazo na kule kuendelea kwa wake walioitwa wameendelea.

Kitu kibaya kinacho tuathiri na kitakachotuasiri Sana hapa afrika ni kikosekana vision kwa viongozi wetu, Kila anaeingia madarakani ana kuja na lake na anapoingia mwingine hupangua hili na kupanga lile.

Hii imepelekea kupelekeshwa na wenzetu kwa kizingizio kwamba Bado hatujaweza kuji control.
Kwamba hakuna lolote tutakaloweza isipokua limetokana na wao.

Hili suala la Corona mjadala wake sio wa Leo Wala Jana na hautaisha leo Wala kesho.

Kila nchi imeoipokea kwa namna yake, na sisi kiongozi wetu amelipokewa kwa namna yake.

Tokea kipindi kile tulipotangaziwa kuwepo kwa ugonjwa huu na maamuzi yale yalioafikiwa na kiongozi wetu, na matokeo yake mpaka leo hi athari zake zio Kama zilivyo kwa wengine, Basi hatuna haja kupingana nae.

Kama Kuna mtu ana intereste zake na huu ugonjwa ni lazima apingane na kiongozi wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm mwapenda sapoti ujinga sana; sijui kwanini mna muono mdogo hivyo! Watu hata condom mwashindwa tengeneza lakini kutwa kucha mnapiga kelele. Mbuzi nyie na mtapimwa tena kwa anal swap na mtachanjwa
 
Ila hii chanjo hata nikichajwa itakua sio kwa hiyari yangu.
Binafsi siwezi kubali hii chanjo, kipindi covid imeshika kasi nilipata dalili zote za covid, niliendelea kupiga kazi na kujifukiza hata sijajua niliponaje!

Ni ugonjwa dhaifu mno! Na hasa ni ugonjwa wawazungu, kwani huko kwao miaka nenda rudi flu imekuwa ikiwatandika kwelikweli!

Ila hii ya sasa ndo wanaipromote iwe ya dunia nzima, kimkakati zaidi na biashara!

Tangu zamani mpaka leo hii, mzungu ndie anaemtesa mwafrika, haijawai na haitatoke mzungu kumtakia mema yote mwafrika.

Naungana na raisi wetu, viva JPM"
 
Hizi ni Nadharia za wakomunist za inferiority complex zilianza miaka ya 70 ziliwaathiri Sana waliosoma syllabus za zamani kuanzia miaka ya 70 Hadi 80 mwishoni,ziliasisiwa na wajamaa na makomunist baada ya kushindwa kuwaletea waafrika maendeleo wakatunga nadharia ya kisingizio cha mabeberu na kupenyeza chuki dhidi ya wazungu kwamba ndio msingi wa kutoendelea kwa mwafrika sawa na sasa upinzani usingiziwao kwamba ndo umezuia maendeleo Hali wapinzani awakusanyi kodi.waafrika tunajifia wenyewe kwa matatizo yote hata kabla ya covid.

Hisia za chuki ya ubaguzi ni mbaya sana ukiwa mchawi na muuaji uhisi unataka kurogwa au kuuliwa mda wote.raslimali zetu bila kuwauzia wazungu zinageuka takataka.

Tangu utoto unadundwa chanjo imetoka ulaya, unakunywa cocacola, colgate,madawa ya hospital,nk leo wakuue kwa chanjo zote hizi ni madhara ya syllabus za zamani ziliwafunga wanafunzi kujua external world na kuwapandishia hisia za chuki.
Nadharia za zamani ukumbuke kipindi hicho nchi nyingi za kiafrika zilikuwa hazijakaa vizur kiuchumi ,Mana zilitoka kujikomboa.Vile vile mkoloni hakuwa na shaka na Africa coz wasomi walikuw wachache hivyo ni ngumu kuwatikisa kwa lolote.Vita ya kiuchumi baina ya mataifa yao ,na mapinduzi ya viwanda yameleta yote haya.Karibu asilimia kubwa ya mataifa hayo yanajiweza upande wa science and technology.Thus why Wana kesha usiku na mchana kutafuta masoko Africa na kwengineko ili mambo yaende sawa.Innovation imekuw kubwa kiasi kwamba ushindani umekuw mkubwa Kwenye masoko,hapo ndo wanatumia nafasi hiyo ku create tatizo Kisha kulifanya biashara.matokeo yake ndo tulipofika hapa ,sisi wa nadharia za miaka ya 70
 
Nadharia za zamani ukumbuke kipindi hicho nchi nyingi za kiafrika zilikuwa hazijakaa vizur kiuchumi ,Mana zilitoka kujikomboa.Vile vile mkoloni hakuwa na shaka na Africa coz wasomi walikuw wachache hivyo ni ngumu kuwatikisa kwa lolote.Vita ya kiuchumi baina ya mataifa yao ,na mapinduzi ya viwanda yameleta yote haya.Karibu asilimia kubwa ya mataifa hayo yanajiweza upande wa science and technology.Thus why Wana kesha usiku na mchana kutafuta masoko Africa na kwengineko ili mambo yaende sawa.Innovation imekuw kubwa kiasi kwamba ushindani umekuw mkubwa Kwenye masoko,hapo ndo wanatumia nafasi hiyo ku create tatizo Kisha kulifanya biashara.matokeo yake ndo tulipofika hapa ,sisi wa nadharia za miaka ya 70
Binafsi siwezi kubali hii chanjo, kipindi covid imeshika kasi nilipata dalili zote za covid, niliendelea kupiga kazi na kujifukiza hata sijajua niliponaje!

Ni ugonjwa dhaifu mno! Na hasa ni ugonjwa wawazungu, kwani huko kwao miaka nenda rudi flu imekuwa ikiwatandika kwelikweli!

Ila hii ya sasa ndo wanaipromote iwe ya dunia nzima, kimkakati zaidi na biashara!

Tangu zamani mpaka leo hii, mzungu ndie anaemtesa mwafrika, haijawai na haitatoke mzungu kumtakia mema yote mwafrika.

Naungana na raisi wetu, viva JPM"
Adui wa mwafrika ni mwafrika mwenzake, Mwafrika ndie anaeuwa waafrika wengi kwa njaa,vita, umasikini,maradhi eti unakuta mtawala anajivunia kuzalisha idadi ya Mzungu ndie
Anaehudumia wakimbizi afrika waliosababishwa na waafrika, ndie uwarudisha wahamiaji haramu wa ethiopia nchini mwao,ndie utoa misaada wakati wa njaa,nk
 
Unaloongelea ni lilelile! Hivi vita na wakimbizi ndani ya afrika kiasi kikubwa vina mkono wa wazungu wakishirikiana na vibaraka waliopo ndani ya afrika,

angalia mifano ya waziwazi shida iliopo kongo inasababishwa na wazungu, wakimbizi wa libya wamesababishwa na nani?

Tangu zamani ni nani amekuwa akiwaua viongozi wanoonekana kupigania maslai ya waafrika ktk nchi zao?

Tangia kipindi cha ukoloni mpaka sasa falsafa za wazungu juu ya afrika hazijawai kubadilika, ni njia tu ndo zinabadilishwa na lengo lao sio kuua tu waafrika ni kumiliki biashara na kujipatia faida.

Vita, maradhi, na njaa vyote ni biashara kubwa zinazoendesha uchumi wa nchi zao na ni lazima wasababishe ili waje na suluhisho linalowapatia faida kubwa.

Angalia kimfano malaria, ukimwi, kifua kikuu nk. Yote haya faida wanapata wao, achilia mbali makundi ya kimapigano yanayowapa faida kubwa zaidi.

Nigeria wananufaika nn kwa uwepo wa boko haram? Ona yaliotokea syria, yanayoendelea mashariki ya kati.

Usiwaamini wanachojali wao ni faida tu hawana habari na ustawi wa nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom