Je, Mhe. Rais anayo haja ya kuwa na wasiwasi na mashaka dhidi ya Chanjo ya Corona?

Sio Magufuli tu hata mimi siikubali hyo chanjo.
Huu ugonjwa umekaa kibiashara zaidi.
gonga malimao yako gonga tangawizi zako. Kwisha habari
jina lako linaakisi wewe ulivyo, sawasawa tu na huyo unayemuunga mkono maamuzi yake!
 
Ubaya wenu mnasoma historia na kuielewa kwa juu juu!

Yaani sawa kuelezwa jua linatoka mashariki kuelekea magharibi na wewe kujua hilo tu tayaritayari unajiona tayari umeishakuwa "astronomical field guru"! Hautaki kuhoji zaidi kwa nini jua lianzie mashariki...kwa nini lisianzie kusini lakakatiza mashariki ya kati hilo likaelekea kaskazinimagahribi !

Na hautakiwi kujiuliza tu ni kuhakikisha unapata majibu sahihi ya maswali yako!

NARUDI kwenye hoja yako. Je. Umejaribu kujishughulisha kujua chanzo cha maradhi mazito haya kujirudia baada ya muda uliotaja ni nini? Je. Umejaribu kuoanisha tawala za dunia wakati huo wa maradhi yanatokea zilikuwa zinajishughulisha na nini? Na zilkuwa na mahusiano gani?

Mkuu, hutakiwi kujiuliza tu maswali haya bali ni pamoja na kutafuta majibu yake sahihi!

Sasa ujipime mwenyewe "upuuzi wa akili" unao uona kwa wenzako uko chini mara ngapi ya " wa kwako"!
 
Mafyatu hao.
 
Akae akijua,imebaki miaka 4 tu atupishe.
Huwezi kutawala milele.
Walikuwepo wafalme wengi sana,wenye nguvu mara 1000+ ya kwake,Ila sasa hawapo.
Miaka 4 ni mingi mkuu,kwani kasema anataka kutawala milele?
 
Unajua Corona ilipotokea?
Unajua kuwa ni UGONJWA wa MAABARA?
 
Angalia mpango wao hapa juu ya hii dunia
 

Attachments

  • 20210127_225116.jpg
    57 KB · Views: 12
Unajua Corona ilipotokea?
Unajua kuwa ni UGONJWA wa MAABARA?
Unajua maana ya Kujua ?
Au unataka kila mtu alete yeye anavyojua na tukubaliane nae kwamba ni facts ?
Official Reports kuhusu Corona zinasemaje au nichambue conspiracy report moja na tuifanye iwe factual
 
Corona ni virus vilivyotoka MAABARA.
Huo ndo ukweli
Unajua maana ya Kujua ?
Au unataka kila mtu alete yeye anavyojua na tukubaliane nae kwamba ni facts ?
Official Reports kuhusu Corona zinasemaje au nichambue conspiracy report moja na tuifanye iwe factual
 
Maisha ya mwanadamu yamejawa na changamoto nyingi Sana, na nyingi ya changamoto hizo zimetengenezwa na mwanadamu huyo huyo ili kujiletea mazingira rafiki yatakayo muwezesha kuishi kwa jinsi anavyotaka ama kupenda.

Ni kwa namna hio tunaweza kusema Kila alietangulia hutamani asiwepo wa kumfikia na kuficha mbinu alizotumia kufikia hapo alipo.

Nchi za Africa na hata hapa kwetu Tanzania tumekua miangoni mwa wenye kuathirika na athari zitokanazo na kule kuendelea kwa wake walioitwa wameendelea.

Kitu kibaya kinacho tuathiri na kitakachotuasiri Sana hapa afrika ni kikosekana vision kwa viongozi wetu, Kila anaeingia madarakani ana kuja na lake na anapoingia mwingine hupangua hili na kupanga lile.

Hii imepelekea kupelekeshwa na wenzetu kwa kizingizio kwamba Bado hatujaweza kuji control.
Kwamba hakuna lolote tutakaloweza isipokua limetokana na wao.

Hili suala la Corona mjadala wake sio wa Leo Wala Jana na hautaisha leo Wala kesho.

Kila nchi imeoipokea kwa namna yake, na sisi kiongozi wetu amelipokewa kwa namna yake.

Tokea kipindi kile tulipotangaziwa kuwepo kwa ugonjwa huu na maamuzi yale yalioafikiwa na kiongozi wetu, na matokeo yake mpaka leo hi athari zake zio Kama zilivyo kwa wengine, Basi hatuna haja kupingana nae.

Kama Kuna mtu ana intereste zake na huu ugonjwa ni lazima apingane na kiongozi wetu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm mwapenda sapoti ujinga sana; sijui kwanini mna muono mdogo hivyo! Watu hata condom mwashindwa tengeneza lakini kutwa kucha mnapiga kelele. Mbuzi nyie na mtapimwa tena kwa anal swap na mtachanjwa
 
Ila hii chanjo hata nikichajwa itakua sio kwa hiyari yangu.
Binafsi siwezi kubali hii chanjo, kipindi covid imeshika kasi nilipata dalili zote za covid, niliendelea kupiga kazi na kujifukiza hata sijajua niliponaje!

Ni ugonjwa dhaifu mno! Na hasa ni ugonjwa wawazungu, kwani huko kwao miaka nenda rudi flu imekuwa ikiwatandika kwelikweli!

Ila hii ya sasa ndo wanaipromote iwe ya dunia nzima, kimkakati zaidi na biashara!

Tangu zamani mpaka leo hii, mzungu ndie anaemtesa mwafrika, haijawai na haitatoke mzungu kumtakia mema yote mwafrika.

Naungana na raisi wetu, viva JPM"
 
Nadharia za zamani ukumbuke kipindi hicho nchi nyingi za kiafrika zilikuwa hazijakaa vizur kiuchumi ,Mana zilitoka kujikomboa.Vile vile mkoloni hakuwa na shaka na Africa coz wasomi walikuw wachache hivyo ni ngumu kuwatikisa kwa lolote.Vita ya kiuchumi baina ya mataifa yao ,na mapinduzi ya viwanda yameleta yote haya.Karibu asilimia kubwa ya mataifa hayo yanajiweza upande wa science and technology.Thus why Wana kesha usiku na mchana kutafuta masoko Africa na kwengineko ili mambo yaende sawa.Innovation imekuw kubwa kiasi kwamba ushindani umekuw mkubwa Kwenye masoko,hapo ndo wanatumia nafasi hiyo ku create tatizo Kisha kulifanya biashara.matokeo yake ndo tulipofika hapa ,sisi wa nadharia za miaka ya 70
 
Adui wa mwafrika ni mwafrika mwenzake, Mwafrika ndie anaeuwa waafrika wengi kwa njaa,vita, umasikini,maradhi eti unakuta mtawala anajivunia kuzalisha idadi ya Mzungu ndie
Anaehudumia wakimbizi afrika waliosababishwa na waafrika, ndie uwarudisha wahamiaji haramu wa ethiopia nchini mwao,ndie utoa misaada wakati wa njaa,nk
 
Unaloongelea ni lilelile! Hivi vita na wakimbizi ndani ya afrika kiasi kikubwa vina mkono wa wazungu wakishirikiana na vibaraka waliopo ndani ya afrika,

angalia mifano ya waziwazi shida iliopo kongo inasababishwa na wazungu, wakimbizi wa libya wamesababishwa na nani?

Tangu zamani ni nani amekuwa akiwaua viongozi wanoonekana kupigania maslai ya waafrika ktk nchi zao?

Tangia kipindi cha ukoloni mpaka sasa falsafa za wazungu juu ya afrika hazijawai kubadilika, ni njia tu ndo zinabadilishwa na lengo lao sio kuua tu waafrika ni kumiliki biashara na kujipatia faida.

Vita, maradhi, na njaa vyote ni biashara kubwa zinazoendesha uchumi wa nchi zao na ni lazima wasababishe ili waje na suluhisho linalowapatia faida kubwa.

Angalia kimfano malaria, ukimwi, kifua kikuu nk. Yote haya faida wanapata wao, achilia mbali makundi ya kimapigano yanayowapa faida kubwa zaidi.

Nigeria wananufaika nn kwa uwepo wa boko haram? Ona yaliotokea syria, yanayoendelea mashariki ya kati.

Usiwaamini wanachojali wao ni faida tu hawana habari na ustawi wa nchi nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…