makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 31,583
- 92,670
Wote tungeishi hivi, dunia ingekuwa sehemu bora zaidi kuishi, ila ndio haiwezekani...Hahahaa Baba, naomnba nikopeshe dawa....Dah nimekumbuka a very sad story, mwaka jana October 2020 nilikua Njombe kwa kazi fulani, sasa kuna Kijana akawa amesafiri akaniachia geto lake, nikatoka Lodge nikaenda kupunguza gharama za accomodation kwake....
Jioni moja narudi, nikasimama mahali nikanunua mahindi nitafune kidogo, aliyekua anauza ni Bibi mtu mzima sana, mara akaja binti mdogo around 10-13 yrs akasema, Bibi amekataa...... Bibi nikaona anasikitika sana kwamba angempelekea pesa yake tu akimaliza kuuza mahindi, ile story ikanigusa, nikauliza shida nini Bibi? Kasema anaumwa na alitaka panadol ameze ila ndio hivyo amenyimwa hadi apeleke pesa.
Nilihisi mwili wangu umepigwa ganzi aisee, nikavuta picha ya Marehemu Mama yangu, nikajikuta natoa buku mbili, akaenda kununua hizo panadol, nikalipia mhindi wwangu, lile jambo liliniumiza sana sana, sikupata usingizi kabisa.
Kesho jioni, nikiwa narudi nikapitia dukani nikamfanyia shopping ya vitu vya ndani, sukari, mchele, dawa za meno, sabuni, unga, mafuta na maharage, dah nikawa niko chini ya salio kidogo maana nilikua bado sijakamilishiwa cheque yangu.
MUNGU alivyo wa ajabu, kesho nikapokea cheque yangu na siku ile iliyofuata nakumbuka ilikua Jumatano asubuhi nikapigiwa simu ya tender nyingine...nikatambua yuko MUNGU juu Mbinguni anayejibu sala na maombi yetu. Siku nikirudi Njombe nitaenda kumsalimia.
Umenikumbusha mbali
Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app