Je, milioni 35 nizi-invest katika biashara ipi kati ya hizi?

Wote tungeishi hivi, dunia ingekuwa sehemu bora zaidi kuishi, ila ndio haiwezekani...



Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Hongera mkuu
 
Naongezea wazo langu kwako.

Go for Mobile Money kama Mpesa, airtel Money, NMB WAKALA, CRDB, hii haina ku expire mkuu.

HAPA NI PESA INALETA PESA KILA SIKU.

9. Fanya biashara Ya mazao mkuu hautojutia. Chukua milioni 6-8 utafurahia faida yako.

nina kaka yangu yeye kila wiki anaingiza laki 5 kwenye mchele. Mtaji wake unakimbilia 10 mil. Kukunja laki 5 mpaka milioni 1 per week ni kitu ya kawaida



Nb: research ni muhimu kwa kila biashara
 
Ubarikiwe sana mkuu
 
Thanks mkuu

Hii ya financial services..nikifungua hata vituo vitano..sehemu iliyochangamka..naweza kuingiza shingapi kwa makusanyo ya vituo vyote..kwa mwezi?
 
Thanks mkuu

Hii ya financial services..nikifungua hata vituo vitano..sehemu iliyochangamka..naweza kuingiza shingapi kwa makusanyo ya vituo vyote..kwa mwezi?
Kuna jamaa mmoja aliwahi kuleta mgawanya wa faida anayopata kwa Mpesa, Airtel na Tigo, kila moja ilikuwa inamuingizia Tsh 300,000!

kwa zote tatu alikuwa anapata laki 9 monthly.

sasa kama ukiongeza na uwakala wa Crdb, NMB na huku unachajisha na simu mkuu utapata pesa sana.

Maeneo ya stendi zenye watu wengi sana naona ndio wanufaika wazuri.

Nakushauri uingie front ufanye utafiti sana kabla hujaingiza pesa kwenye investment.

vp hio ya mazao hujaipenda?
 
Ya mazao mkuu sina experience nayo ..labda unipe muongozo zaidi..kwa maana pia hii lazima uwe na soko la uhakika
 
Ya mazao mkuu sina experience nayo ..labda unipe muongozo zaidi..kwa maana pia hii lazima uwe na soko la uhakika
inategemeana na namna ya biashara unavyotaka kuifanya.

mfano biashara ya MPUNGA/MCHELE. kuna watu wananunua mchele huko vijijini wanakuja kuuza mashineni (pale pale mpunga unapokobolewa)

wengine wananunua mpunga vijijini wanakuja wanakoboa na kuuza hapo hapi mashineni (hii ndio common).
Faida (net profit) kwa gunia inaanzia 10,000 - 15,000

Upande wa mazao mengine sasa ni wewe kujiongeza. buy at a low price and sell in a big price.

BIASHARA NYINGINE NZURI NI YA NG'OMBE
hii biashara bwana inalipa sana asikwambie mtu.
kuna watu wananunua ng'ombe waliokondoena kwa laki 2 mpaka 2.5 kisha wanakuja kuwanenepesha kwa miezi miwili mitatu wanakuja kuwauza laki 5 mpaka zaidi.

Ukienda shinyanga kipindi cha kiangazi ndio utazipata kwa hizo bei ndogo sana, ama miezi ile ya watoto wanaenda shule mifugo inashuka sana bei.
 
Kuna majamaa niliyakuta kule kwetu isenye, yanakuja yananunua ng'ombe wala high Grade. Wanaenda kuuza Kenya Huko. Biashara hio inalipa.

wengine wananunua ndani ya wiki hio hio anauza anafukuzia faida elfu 50😅😅

cha msingi ujue namna ya kumpiga fix mkulima/mfugaji
 
4: UWAKALA VINYWAJI VYA AZAM - nichukue mzigo kutoka kiwanadani na ninunue bajaji used kwa ajili ya kusambaza mzigo.
Hii inazungusha hela fasta kama 10G network.
Uweke na akina Mo energy. Hii mie pia ndo naifanya. Ina faida kidogo Ila kwa mzunguko. Afu let say katoni ya maji unapata faida 400 Kuna mteja anachukua katoni 20, mwingine 30, mwingine 10, mwingine 50 hapo ni kulingana na uwezo wao nadhani na mzunguko wa biashara zao
 
Wote tungeishi hivi, dunia ingekuwa sehemu bora zaidi kuishi, ila ndio haiwezekani...



Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Usingetambua thamani ya icho kitu. Ungeona kawaida. Yaani ili uitwe mzuri inabidi mbaya awepo. Ama uitwe tajiri masikini lazima awepo. Sasa wote matajiri hakuna Mana ya utajiri. Do you get me or the concept my dear
 
Kweli biashara ni mbinu hahahahah
 
Ahsnate mura
 
Kaka yako yeye anafanyaje aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…