Je, Mkurugenzi wa manispaa kufuturisha wenyeviti wa serikali za mitaa ni sahihi?

Hii ni mujibu wa Sheria au Kanuni ipi kwamba ukitumia cheo basi lazima fedha za ofisi zitumike na ukitumia jina lako basi unatumia fedha zako binafsi?
Cheo chako hakifungamani na imani yako ya dini na thawabu utakayopata haitokani na cheo chako! Kumbuka kufanya ibada unawasiliana na Mungu!

Ni logic tu wala haihitajiki kanuni yo yote!
 
Je Kama anatumia hela yake
 
Kuwaambia watu mmealikwa na mkurugenzi wa manispaa kuna shida? Na umejuaje anatumia fedha za umma? Mimi na wewe hatujui, ivyo tusimshuku.
Ndiyo kuna shida kwani waalikwa watakuja kwa kuheshimu cheo chako na wala siyo imani yako wala mahusiano mliyonayo!
Hata kama hajatumia fedha za umma, kitu ambacho nakitilia shaka lakini ametumia cheo cha umma kuita watu!

Dhambi kubwa hiyo!
 
Wewe akili zako umepeleka wapi? Kwani angetumia jina lake ujumbe usingefika? Anahofia nini kutumia jina lake? Uhusiano wake na aliyowaalika uko vipi au hafahamiki na watu ndiyo sababu akatumia cheo chake?
 
Wewe akili zako umepeleka wapi? Kwani angetumia jina lake ujumbe usingefika? Anahofia nini kutumia jina lake? Uhusiano wake na aliyowaalika uko vipi au hafahamiki na watu ndiyo sababu akatumia cheo chake?
Are you serious?
Yaani mkurugenzi wa manispaa asifahamike?

Ndio hafahamiki na watu na ndio maana ametumia cheo chake, haya hapo umepata faida gani?
 
Angetumia jina lake! Kwa sababu akihamishwa hapo mwakani watu watauliza kwa nini mkurugenzi mpya hajafuturisha!
Angetumia jina lake hawezi kujulikana kama ni mkurugenzi eee
 
Ww aliyekwambia anatumia hela ya serikali nani au umbea tu unakusumbua huyo mkurugenzi hana hela ya kufutulisha? Wangetangaza manispaa ya kinondoni inafutulisha hapo sawa ujue kutofautisha maisha binafsi ya mtu na ya kazini
Mkurugenzi wa wilaya, anafuturisha wenyeviti wa...! Hivi hadi hapo bado una amini pesa za kwake? Ungesikia hivi, "Bwana Mazindu anategemea kufuturisha kina fulani bin fulani.." then sie wazee wa majungu tukajiuliza huyo Mazindu ni nani? Halafu jibu likaja kua ni mkurugenzi wa wilaya, hapo wala isingeleta maswali wala
 
Does it matter?
Who cares?
 
Are you serious?
Yaani mkurugenzi wa manispaa asifahamike?

Ndio hafahamiki na watu na ndio maana ametumia cheo chake.
Kwani mkurugenzi ni nani afahamike na kila mtu? Sana sana anafahamika na watumishi wenzake au na watu aliowahudumia na waumini wenzake. Hapa nilipo simfahamu mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya wala mkurugenzi wa wilaya kwa sababu sijapata huduma yao moja kwa moja!
 
Ukiishi kwa chuki maisha haya utakufa mapema.

Mkurugenzi kufuturisha mbona jambo dogo sana? Makampuni yote kwenye manispaa yanachukuwa tender kwake unadhani anaweza kushindwa kufadhiliwa futari ya millioni 4 au 5?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…