Hatuwasiliani kabisa, ila tukikutana inakuwa surprise na kuitana classmate tu no matter tumezidiana elimu na vipato, wengine wana hadhi za kisiasa, wengine hadhi za wanadini, wafanyabiashara, wanataaluma, wajasiriamali na wengine raia wa mitaani wasio na shughuli rasmi huku kukiwa na walioharibika akili japo wana ufahamu na utambuzi kuwa tulisoma pamoja.
Ila kuna changamoto kama utataka offer kwa aliyekuzidi kipato hutapata katika wengi, ni wachache sana wanaweza kukujali akakupa japo soda au chochote cha ghafla kuonesha ku approciate u schoolmate wenu. Wengine mkishatofautiana hadhi ni ngumu hata kusalimiana kwa kuwa anaona wewe si hadhi yake.