Je, moto wa ajabu ardhini rombo ni dalili za kulipuka volcano iliyolala ya mlima Kilimanjaro?

Hiyo mifupa inashangaza hapo tumepigwa taarifa gongana hile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ramli tu Kaka. Wataanza kusema mara carbon 14 na utumbo mwingine mwingi wa kutughiribu tuwaone Wana akili wakati ndio haohao wanaoamini mwenge unaleta amani vitani
[emoji1787] [emoji1787] Nitakujibu la mwenge, mwenge hutumika tu kama ishara na alama, ni kama Roman catholic wanavyofanyaga njia ya msalaba ni kuyaenzi yale tunayoyaamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkubwa andiko lako ni zuri, ila unajichanganya katika miaka. Unasema mlima ulitokea miaka 1000 iliyopita. Baadae unasema tena Mawezi ilitokea miaka millioni kadhaa iliyopita. Kisha unasema tena Kibo iliacha kurusha volcano miaka 200,000 na kitu iliyo pita. Kwenye miaka zingatia kuangalia wapi kuna makosa.
Lakini hata mie uwa nawasiwasi sana, nahisi ipo siku mlima kilimanjaro utalipuka volcano ya sasa haifiki nje, lakini kuna siku itafika! Mie si mwana sayansi lkn kuna siku jambo litatokea.
 
[emoji1787] [emoji1787] Nitakujibu la mwenge, mwenge hutumika tu kama ishara na alama, ni kama Roman catholic wanavyofanyaga njia ya msalaba ni kuyaenzi yale tunayoyaamini

Sent using Jamii Forums mobile app
NI utumbavu kutumia mabilioni kila mwaka kwa Hilo likibatari wakati maji mmeshindwa ku supply nchini
 
Mada nzur ya kujifunza Geography ya nchi yetu lakin Hakuna wachangiaji ingekuwa mapenz hapa wangekuja wakutosha
 
Hadithi kama hii inafanana na ile wanayosema zanzibar kuna siku itazama this depend to its foundations
 
Hayo mambo ya miaka Laki , mara milioni. Mie wala hayaniingii akilini.
Kwa mujibu wa Biblia dunia imeishi miaka takribani elfu 6. Kadri muda unavyendelea inazidi kuchakaa na kuwayawaya.
 
Wamesema ule moto umesababishwa na takataka zilizofukiwa chini, huyu mtoa mada hafatilii media
 
Kweli mkubwa nilikosea na nimeshasahihisha, badala ya miaka milioni moja niliandika elfu moja. Ingawa namimi pia si mwanasayansi mbobevu lakini hebu ngoja kwa uelewa kidogo nilio nao nijaribu kuweka vizuri hapa: Tangu kilele cha kwanza (Shira cone) kuanza kufoka wanakadiria ni miaka milioni 2.4 mpaka 3.5 iliyopita. Baadae tena miaka milioni moja(1.0) shira kilizimika vikajitokeza viotea vingine viwili ambavyo ni Kibo na Mawenzi. Viliendelea kufoka mpaka kufikia miaka 450,000(laki nne na nusu) ambapo Mawenzi kilizimika na kuacha kufoka(volcano mfu) huku Kibo kikiendelea kufoka mpaka hivi karibuni kabisa miaka 200,000(laki mbili) nacho kikasimama kwa muda kama volcano iliyolala. Kwa ujumla tangu vilele vyote kuanza mpaka sasa hivi inakadiriwa ni miaka zaidi ya milioni 2.5 na tokea mlipuko wa hivi karibuni kabisa kutokea inakisiwa ni miaka laki mbili(200,000)
 
Ngoja tuendelee kufanya tafuti, ivi iyo mifupa haikuwa jivu baada ya volcano kulipuka Mana napata mashaka kuhusu carbon14
 
Wamesema ule moto umesababishwa na takataka zilizofukiwa chini, huyu mtoa mada hafatilii media
Ni jambo la kheri mkuu ikiwa mboji itakuwa ndiyo chanzo cha huu moto na wala si volcano kama nilivyohisi maanake kwa vyovyote vile ikiwa ni mboji itazimika tu pindi mvua zikinyesha au mbolea ikiteketea yote kwa moto. Lakini niulize wadau wengine hali kama hiyo ya mboji kuwaka imewahi kutokea mahali pengine hata nje ya Tanzania na mifano ikarekodiwa? basi mwenye taarifa japo atujuze tupate kujua zaidi tafadhali.
 
Ngoja tuendelee kufanya tafuti, ivi iyo mifupa haikuwa jivu baada ya volcano kulipuka Mana napata mashaka kuhusu carbon14
Hata ikiwa jivu Watafiti wanachotafuta ni viasili vya Carbon itokanayo na kiumbe hai kilichokufa, hayohayo majivu wanaweza wakayatumia kama sampuli katika utafiti. Pia kiumbe hai si lazima kiwe ni mifupa ya binadamu au wanyama pekee bali hata miti na manyasi vinaweza kutumika. Uji wa volcano unapofunika mahali masalia ya viumbe hai yanaweza yasiungue moja kwa moja kutegemeana na ni kitu gani kilikuwa juu ya hayo masalia. Mfano ikiwa pengine yalikingwa na utando mwingine wa udongo au tabaka la takataka za viumbe wengine wafu kuna uwezekano baada ya miaka mingi ukaja kuzikuta hazijaharibika kwa chochote
 
….. walishangilia/kusherehekea kifo cha rais wet mzalendo Dkt Magufuli.
 
Maelezo yameshatolewa, moto huo umetokana na MBOJI.
kuna mkusanyiko wa majani mengi yanayosombwa na maji na kujikusanya sehemu moja na kusababisha hyo hali.
Moto haukuanzia kwenye miamba.
 
Moto wa Rombo bahati nzuri ulikuwa moto wa kawaida uliotokana na shughuri za binaadamu, kwenye eneo husika kulikuwa na taka za mimea zilizofukiwa kwenye shimo na moto ulipozifikia uliingia chini na kuendelea kama ufanyavyo kwenye tanuru la mkaa. Wataalamu walichimba na kuyatoa mabaki hayo na ndiyo ukawa mwisho wa moto huo na jarada kufungwa pia kuwezesha wanarombo kuendelea kunywa pombe zao bila hofu, ila bado ninamkumbuka mrombo mmoja aliyesikika akisema "hata ukiweka nyama inaiva".
 
Sehemu zenye jua kali mawe na mbuga kavu moto huweza kuwaka wakati wowote. Mioto tuionayo maporini mingine ilianza yenyewe kutokana na joto la jua.
 
Ahsante kwa taarifa na maarifa...

Nawaza, mlima Kilimanjaro Volcano ikianza kulipukoa tena sii itatuharibia barafu kwa kuiyeyusha yote, alafu mlima unabaki kipara...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…