Whitepanther
JF-Expert Member
- Sep 27, 2021
- 289
- 458
Una hoja ya msingi na isipingwe naipitishaNI utumbavu kutumia mabilioni kila mwaka kwa Hilo likibatari wakati maji mmeshindwa ku supply nchini
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Una hoja ya msingi na isipingwe naipitishaNI utumbavu kutumia mabilioni kila mwaka kwa Hilo likibatari wakati maji mmeshindwa ku supply nchini
Punguza dharau mkuu.Wanasayansi wa bongo ni bure kabisa yaani ni empty set ,jana maTV yote yameonyesha kwamba wamegundua mifupa ya mjusi iliyoishi miaka milioni 160 hahaaaaa ukiangalia hiyo mifupa ni kama jiwe lilitokana na zege,mfupa ukae miaka milioni 160 halafu utoke kama jiwe hahahaaaa nonsense.
Hapo wakija wazungu hapo rombo watatoa report sahihi lakini hao ma geologist wabongo wanaenda kupiga perdiem tu.
Anasema kweli, lile tope la Kunduchi mpaka leo wakazi wanalalamika hawajapata jibu huku nyumba zao zikizidi kuathirika kwa kudidimia.Punguza dharau mkuu.
JiolojistiKwa wakaazi wa Wilaya ya Rombo na maeneo mengine yote kuuzunguka mlima Kilimanjaro chochote kinachotokea kuhusiana na Mlima huu ni lazima kiwaguse moja kwa moja kutokana na maisha yao kutegemea miteremko yake kwa maelefu ya miaka iliyopita. Ingawa uwezekano wa Volcano ya mlima huu kulipuka wanasayansi wanasema ni mdogo sana lakini bado wanasisitiza kwamba ni jambo linaloweza siku moja kuja kutokea kutokana na sababu kwamba volcano yake imelala tu na si kama imekufa kabisa.
Mlima mrefu kuliko yote Afrika Kilimanjaro(Kibo) ni mlima uliotokea Duniani baada ya mlipuko wa Volcano chini ya ardhi yapata miaka zaidi ya 1,000,000 hivi iliyopita. Ukiwa na vilele duara 3 (cones), Shira, Kibo na Mawenzi, kila kimoja kilijitengeneza kwa wakati wake huku Shira(kilele-mama) kikiwa ndicho kilichoanza kutokea yapata miaka zaidi ya mlioni 2.5 iliyopita kisha kikaja kuzimika kabisa (kufa) na kuzuka Mawenzi na Kibo vilivyoanza wakati mmoja miaka 1,000,000 iliyopita.
Kufikia miaka 450,000 iliyopita kilele cha Mawenzi kilisimama kabisa kurusha volcano na kuwa volcano mfu pia(iliyokufa) huku Kibo kikiendelea kurusha volcano yake mpaka ilipofika miaka 150,000 hadi 200,000 iliyopita ambapo nacho kilisimama lakini kwa muda tu siyo kufa kabisa kama wenzake Mawenzi na Shira. Hii inamaanisha kwamba kuna uwezekano siku yeyote ile Kibo kikaja kuanza tena kulipuka na kurusha volcano na majivu ya moto.
Kwa mujibu wa Wataalamu wa mambo ya miamba(geologists) Mlima Kilimanajaro na milima mingine ya kivolcano iliyopo Africa Mashariki kama mlima Kenya, mlima Meru, Mlima Elgon, Ol Doinyo Lengai, Dalafilla, longonot, mlima Nyiragongo pamoja na Maziwa mbalimbali kama vile ziwa Victoria, Nyasa, Tanganyika, Turkana nk. ingawa si vyote vipo ndani ya bomde la ufa lakini vyote ni matokeo ya shughuli za kivolcano zilizosababishwa na mpasuko wa umbo la nje la ardhi ya dunia ( tectonic plates) ambazo kila moja hujivuta kutoka kwa mwenzake na kusababisha Bonde kubwa la ufa kutokea katikati.
Mpasuko huo umesababisha baadhi ya maeneo kuwa dhaifu hivyo kusababisha eneo la ndani kabisa la Dunia ambalo kimsingi huwa na joto kali sana kupitisha uji-uji wenye mchanganyiko wa madini mbalimbali na miamba nje ya uso wa dunia(volcano). Uji huu ndio husababisha milima kama Kilimanjaro kutokea taratibu baada ya maelfu ya miaka kupita ukitiririka. Bonde la ufa limeanzia huko Ethiopia mpaka Msumbiji likipitia nchi za Somalia, Kenya, Uganda, Burundi, rwanda, Malawi na Zambia.
Katika eneo ulipozuka mlima Kilimanjaro na kwa kuwa bado shughuli za kivolcano bado zinaendelea chini ya ardhi hasa ukanda mzima wa Bonde la Ufa la Afrika Mashariki basi kuibuka kwa hali kama tunayoishuhudia Rombo yawezekana isiwe ni jambo la ajabu sana. Eneo tukio la Rombo lilipotokea si mbali na ulipo Mlima Kilimanjaro.
VIASHIRIA VINGINE.
ZIWA CHALA
Ziwa chala ni moja kati ya “vijitoto” vilivyotokana na volcano iliyounda mlima Kilimanjaro, ni ziwa lililopo Wilayani Rombo na linakadiriwa kutokea muda sawa na kilele cha Kibo miaka takriban 200,000 ilyopita. Utafiti uliofanyika kwenye ziwa hilo kwa kuchunguza matabaka ya mlundikano wa majivu ya volcano (tephra layers) ndio uliothibitisha muda halisi wa kutokea kwa mlipuko wa mwisho kiasi cha mikaka 150,000 hadi 200,000 tofauti na jinsi ilivyodhaniwa kabla kwamba ni mamilioni ya mika mingi iliyopita. Hivyo unaweza kuona miaka 200 elfu si mingi sana katika umri wa kijiolojia.
Mpaka sasa hivi hata watu wanaopanda mpaka kufika kilele cha Uhuru wanaweza kuhisi harufu ya gesi za salphur kutokea katika Crater ya mlima Kilimanjaro pale juu kabisa, ishara kwamba bado kuna shughuli za kivolkano bado zinaendelea chini ya mlima huu lakini kwa kiwango cha chini (under low pressure) kiasi majivu na uji wa miamba haviwezi kuruka umbali mrefu
Binafsi mimi (Haya ni maoni yangu lakini) nimefikiria moto wa Rombo labda inawezekana ikawa ni moja kati ya viotea vya mlima Kilimanjaro (monogenetic parasitic eruption associated with Mt Kilimanjaro) mfano wa ziwa chala na vilele vingine mfano kama ilivyotokea mawenzi na Kibo baada ya Shira, ingawa hivi vya sasa vyaweza kuwa na athari ndogo sana na vinavyoisha muda mfupi tu vikiwa na majivu ya udongo wa moto badala ya volcano na uji mzito wa miamba ya chuma shauri ya presha ndogo iliyopo ardhini kwa sasa.
Katika maeneo mengine Afrika Mashariki katika ukanda wa Bonde la Ufa kumewahi kuripotiwa moto wa ardhini ingawa sifikirii kama unafanana kabisa na huu wa Rombo. Huko Kenya mpaka wamefikia hatua ya kufua umeme kwa kutumia moto kama huu (Geothermal energy). Katika maeneo mengine duniani mfano katika msitu wa Amazon nimewahi kusoma kuna eneo fulani pana mto wa maji moto yanayochemka, nadhani pengine inaweza kuwa ni kitu kama hikihiki kilichotokea Rombo.
MATETEMEKO YA ARDHI
Bado Rombo na maeneo mengine kando kando ya Kilimanjaro kuna nyakati hutokea matetemeko ya ardhi, ishara nyingine kwamba shughuli za kivolcano chini ya eneo zima na ukanda wa bonde la ufa la Afrika Mashariki bado zinaendelea. Tetemeko la ardhi la mwisho lilitokea Rombo mwaka jana.
Tafiti nyingi sana zimeshafanyika na wanasayansi kuhusiana na uwezekano wa kulipuka tena kwa mlima Kilimanjaro, unaweza kutafuta “google’ na kuona ingawa karibu kila mtafiti anasema kwamba hamna uwezekano mkubwa wa mlima huo kulipuka tena hivi karibuni na hata yawezekana kilele cha Kibo kikaja kufa kabisa kama wenzake Shira na Mawenzi. Hili lakini halina uhakika kwa asilimia mia moja.
Wakaazi wa Kilimanjaro tukio kama hili la Rombo halipaswi kutupa taharuki, badala yake tutulie tukichukua tahadhari pamoja na ushauri serikali itakaoutoa baada ya Wataalamu wake kumaliza uchunguzi.
Ingawa Wataalamu wengi wameshafanya tafiti mbalimbali na kuthibitisha volcano ya mlima Kilimanjaro kutokuweza kulipuka hivi karibuni na hata hivyo kungelikuwa na viashiria vikubwa zaidi kama matetemeko na gesi nyingi kuonekana katika crater ya Kibo. Mabadiliko makubwa ya kijiolojia huchukua mamilioni ya miaka hivyo ukilinganisha na umri wa vizazi vyetu usiozidi hata miaka 100 unaweza kuona ni sawa tu na tone dogo sana la maji baharini.
Hata hivyo serikali ina wajibu wataalamu wake kuchunguza na kutoa maelezo ya uhakika zaidi kwetu wananchi ikiwa ni pamoja na tahadhari za kuchukua ikiwa kama kuna hatari zozote zile zinazoweza kuambatana na mabadiliko ya kijiolojia hata kama yatakuwa ni madogo kama haya ya Rombo ili kuepusha Wananchi kuingia taharuki au kwenye imani zingine potofu mfano za ushirikina nk.
View attachment 1960785
Makala hii imeandikwa na mtafiti wa masuala ya kijamii kwa msaada wa vyanzo mbalimbali mtandaoni.
Halafu wakija watatumia vipimo vilevile kama vya wataalamu wetu,kumbe bado tuna ile hali ya kuamini kwamba wataalamu wa nje ndiyo wako bora kuliko wa hapa.Na mimi nimewaza hivyo, itafutwe timu wabobezi kutoka nje ya nchi wakafanye kazi pale
Sent using Jamii Forums mobile app
Utakuwa huelewi kitu mkuu, wacha kubeza kama hujui kitu! Miaka yote hiyo kwa nini mfupa usibadilike kuwa mwamba? Unajua mbolea ya minjingu inachimbwa kutoka na maozea ya flamingos a kinyesi chao kilichokaa maelfu ya miaka?Wanasayansi wa bongo ni bure kabisa yaani ni empty set ,jana maTV yote yameonyesha kwamba wamegundua mifupa ya mjusi iliyoishi miaka milioni 160 hahaaaaa ukiangalia hiyo mifupa ni kama jiwe lilitokana na zege,mfupa ukae miaka milioni 160 halafu utoke kama jiwe hahahaaaa nonsense.
Hapo wakija wazungu hapo rombo watatoa report sahihi lakini hao ma geologist wabongo wanaenda kupiga perdiem tu.
Punguza dharau mkuu.
Utakuwa huelewi kitu mkuu, wacha kubeza kama hujui kitu! Miaka yote hiyo kwa nini mfupa usibadilike kuwa mwamba? Unajua mbolea ya minjingu inachimbwa kutoka na maozea ya flamingos a kinyesi chao kilichokaa maelfu ya miaka?
Wengi wamesoma vyuo vya huko kwa hao mabeberu hivyo usiwabeze.Mfupa umekaa miaka milioni 160 na bado imara? Bado unawaamini hao Bush geologist wenu?
Ni ukweli kabisa hiyo hali huwapata watu wapandapo milima mirefu na pengine huwa serious zaidi kwa mlima kama Kilimanjaro ambao bado unapumua gesi kidogokidogo.Nakumbuka kuna wakati tulipanda mlima Kilimanjaro, ile siku moja kabla ya kufika Uhuru Peak, watu waliumwa sana vichwa na wengine kujisikia vibaya, tukaambiwa mlima umepumua. Unatoa hewa aina ya Sulphur, sikuelewa sana nimesoma kwenye hii makala ikanikumbusha hiyo siku.
Uko vizuri mkuu.
Samahani naomba kutoka nje ya mada kidogo. Niliwahi soma huko maeneo ya Moshi, niliona kama kuna idadi kubwa ya Albino, hii ina uhusiano wowote na athari za Volcano au kuna kitu kingine?
Halafu Wachagga wakisema ukichoma nyama kwenye moto uliozuka ardhini inawiva vizuri mnawaita waroho wa nyama!🤣🤣Kule Mbeya kuna chemchem ya maji ya moto,ukienda na majani ya chai na sukari unaweza kinywa chai ya moto kabisa.
Moto umesababishwa na taka zilizofukiwa chiniKweli mkubwa nilikosea na nimeshasahihisha, badala ya miaka milioni moja niliandika elfu moja. Ingawa namimi pia si mwanasayansi mbobevu lakini hebu ngoja kwa uelewa kidogo nilio nao nijaribu kuweka vizuri hapa: Tangu kilele cha kwanza (Shira cone) kuanza kufoka wanakadiria ni miaka milioni 2.4 mpaka 3.5 iliyopita. Baadae tena miaka milioni moja(1.0) shira kilizimika vikajitokeza viotea vingine viwili ambavyo ni Kibo na Mawenzi. Viliendelea kufoka mpaka kufikia miaka 450,000(laki nne na nusu) ambapo Mawenzi kilizimika na kuacha kufoka(volcano mfu) huku Kibo kikiendelea kufoka mpaka hivi karibuni kabisa miaka 200,000(laki mbili) nacho kikasimama kwa muda kama volcano iliyolala. Kwa ujumla tangu vilele vyote kuanza mpaka sasa hivi inakadiriwa ni miaka zaidi ya milioni 2.5 na tokea mlipuko wa hivi karibuni kabisa kutokea inakisiwa ni miaka laki mbili(200,000)