Je, moto wa ajabu ardhini rombo ni dalili za kulipuka volcano iliyolala ya mlima Kilimanjaro?

Kumbe hii dunia imetoka mbali sana eeeh mimi nilifikiri dunia inaumri wa miaka 2021 tu, sasa hiyo miaka ya nyuma kwanini wasingeiongezea na hii 2021 ili tungejua saizi tupo mwaka wa ngapi e.g 3,676,066
 
Ikiwa ni mboji iliweza kufikia kiwango hiki basi pia naamini eneo litakuwa na rutuba nyingi sana na linaweza kutumiwa kwa kilimo cha zao lolote kama mahindi au ndizi ikiwa chanzo cha maji ya uhakika kitapatikana . Sema nijuavyo Rombo tatizo moja kubwa ni ukame uliotokana na uharibifu mkubwa wa mazingira, zamani kabla ya uharibifu huo inasemekana mvua zilikuwa ni za kutosha sana.
 
Punguza dharau mkuu.
 
Nakumbuka kuna wakati tulipanda mlima Kilimanjaro, ile siku moja kabla ya kufika Uhuru Peak, watu waliumwa sana vichwa na wengine kujisikia vibaya, tukaambiwa mlima umepumua. Unatoa hewa aina ya Sulphur, sikuelewa sana nimesoma kwenye hii makala ikanikumbusha hiyo siku.

Uko vizuri mkuu.

Samahani naomba kutoka nje ya mada kidogo. Niliwahi soma huko maeneo ya Moshi, niliona kama kuna idadi kubwa ya Albino, hii ina uhusiano wowote na athari za Volcano au kuna kitu kingine?
 
geologist
Jiolojisti
 
Kule Mbeya kuna chemchem ya maji ya moto,ukienda na majani ya chai na sukari unaweza kinywa chai ya moto kabisa.
 
Volcano eruption huwa ai beep kindezi ndezi…
 
Miaka million ,mm huwa nawaza sana,kama miaka ya uhuru tu ,hii 60 imetuchachafya namna hii vpi miaka elfu tano ijayo
 
Utakuwa huelewi kitu mkuu, wacha kubeza kama hujui kitu! Miaka yote hiyo kwa nini mfupa usibadilike kuwa mwamba? Unajua mbolea ya minjingu inachimbwa kutoka na maozea ya flamingos a kinyesi chao kilichokaa maelfu ya miaka?
 
Uchunguzi wa ule ujiuji uloibuka kutoka ardhini pale kurasini hali ile iliishiwa wapi.
Yaani nchi yetu kwa kutotoa mrejesho hawajambo.

Uchunguzi wa Moto Kariakoo sokoni
Umezimwa

Uchunguzi wa yule bwana aliyejiunganishia bomba la mafuta kule kigamboni
Ulizimwa

Uchunguzi wa moto ulisababishwa na tanker la mafuta kulipuka morogoro
Ulizimwa

Yaani tupo tupo tu hatuelewi kama tumekaa ama tumesimama.
 
Je tuandae makazi kilometres ngapi kutoka mlima kilimanjaro maana nahofia ng'ombe zangu 400 nilizotafuta kwa shida
 
Utakuwa huelewi kitu mkuu, wacha kubeza kama hujui kitu! Miaka yote hiyo kwa nini mfupa usibadilike kuwa mwamba? Unajua mbolea ya minjingu inachimbwa kutoka na maozea ya flamingos a kinyesi chao kilichokaa maelfu ya miaka?

Mbolea ya minjingu ndiyo inajustify kwamba mfupa unaweza kukaa miaka milioni 160 bila kubadilika? Yaani unakuwa vile vile?
 
Ni ukweli kabisa hiyo hali huwapata watu wapandapo milima mirefu na pengine huwa serious zaidi kwa mlima kama Kilimanjaro ambao bado unapumua gesi kidogokidogo.

Nimekumbuka kisa kimoja nilichosoma wakati natafiti hili andiko mtandaoni, ambapo Mwanamke wa kwanza kabisa na binadamu wa tatu kupanda mlima Kilimanjaro Mwiingereza Bibi Gertrude Benham ilimbidi apande mlima akiwa peke yake huku Maporters wake(wabebaji mizigo wazawa) wakikataa kata kata kuongozana naye kwa kuhofia "Mountain sickness" au homa ya mlimani ambayo ni hali sawa na hiyo uliyosema ya kujisikia vibaya wakati mwingine hata kutapika.

Mwaka 1909 Getrude Benham akiwa na miaka 22 tu alifika Kilimanjaro kwa lengo la kupanda hadi kileleni. Askari wa Kijerumani walimuonya kuwa hakukuwa na Mwingereza mwingine aliyewahi kupanda mlima huo zaidi ya Wajerumani, Johann Rebman na Hans Meyer ambao hata hawakuweza kufika kileleni vizuri. Waliposogea mbele kidogo walikutana na lundo la mifupa ya wafu(skeletons) Maporters wakagoma kuendelea kwa kuhofia ule ulikuwa uchuro au mizimu. Lakini pamoja na Maporters kurudi nyuma wakajificha katika pango la barafu Mwanamama shupavu Benham yeye aliendelea tu kupanda peke yake hadi akafanikiwa kufika kileleni na kurudi salama.

Maporters wale walibakia wakifikiri labda Benham alikuwa na kinga ya homa ya mlimani(Mountain sickness) kumbe basi tu ilikuwa ni kutokana na uzoefu aliokuwa amekwisha upata tokea huko Ulaya kwani kwa maisha yake yote amewahi kupanda vilele vya milima zidi ya 300 duniani kote.

Hili la Malbino Mkuu labda waje wajuzi zaidi wa mambo ya utabibu lakini binafsi ninavyofikiri sidhani kama Moshi au Kilimanjaro Maalbino ni wengi kupita maeneo mengine nchini. Albino sawa na Walemavu wengine kila sehemu duniani wapo na kama pengine sehemu fulani unaweza kuwaona wengi yawezekana ni jambo la nasibu tu, sina uhakika lakini labda kama kuna ushahidi wa kisayansi.
 
Kule Mbeya kuna chemchem ya maji ya moto,ukienda na majani ya chai na sukari unaweza kinywa chai ya moto kabisa.
Halafu Wachagga wakisema ukichoma nyama kwenye moto uliozuka ardhini inawiva vizuri mnawaita waroho wa nyama!🤣🤣
 
Moto umesababishwa na taka zilizofukiwa chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…