wa kibondemaji
Member
- Aug 1, 2024
- 30
- 53
Habari wana JF,
Nimeleta uzi huu kwenu ili nipate msaada wa mawazo.
Kuna rafiki yangu wa muda mrefu zaidi ya miaka 15 ambaye alinishirikisha kuhusu kilimo cha mpunga huko Tabora. Nilipokea wazo hilo na tukakubaliana kushirikiana. Tulikodi ekari 8 na kufanikiwa kupanda mpunga. Japo muda mwingi yeye ndiye alikuwa akiangalia maendeleo ya shamba kutokana na mimi kuwa na majukumu mengi kazini, nilichangia gharama kwa asilimia kubwa sana.
Muda wa mavuno ulipowadia, nilipanga kwenda kushiriki lakini sikuweza kupata ruhusa kazini. Hivyo, ilibidi rafiki yangu aende peke yake. Alipofika shambani, alikuta mpunga umekomaa vizuri, na makadirio yalionyesha tungepata gunia 120 au zaidi. Hata hivyo, baada ya mavuno, alinipa taarifa kwamba magunia yaliyopatikana ni saba (7) tu kutoka ekari zote 8.
Nilipouliza sababu, aliniambia kwamba mpunga umeibiwa kimazingara (uchawi). Sasa naomba kuuliza:

- Je, hili jambo la mpunga kuibiwa kimazingara linawezekana kweli?
- Au rafiki yangu aliingiwa na tamaa?