Je, Mpunga umeibiwa Kimazingara: Ukweli au Tamaa?

Habari wana JF,

Nimeleta uzi huu kwenu ili nipate msaada wa mawazo.

Kuna rafiki yangu wa muda mrefu zaidi ya miaka 15 ambaye alinishirikisha kuhusu kilimo cha mpunga huko Tabora. Nilipokea wazo hilo na tukakubaliana kushirikiana. Tulikodi ekari 8 na kufanikiwa kupanda mpunga. Japo muda mwingi yeye ndiye alikuwa akiangalia maendeleo ya shamba kutokana na mimi kuwa na majukumu mengi kazini, nilichangia gharama kwa asilimia kubwa sana.

Muda wa mavuno ulipowadia, nilipanga kwenda kushiriki lakini sikuweza kupata ruhusa kazini. Hivyo, ilibidi rafiki yangu aende peke yake. Alipofika shambani, alikuta mpunga umekomaa vizuri, na makadirio yalionyesha tungepata gunia 120 au zaidi. Hata hivyo, baada ya mavuno, alinipa taarifa kwamba magunia yaliyopatikana ni saba (7) tu kutoka ekari zote 8.

Nilipouliza sababu, aliniambia kwamba mpunga umeibiwa kimazingara (uchawi). Sasa naomba kuuliza:

  • Je, hili jambo la mpunga kuibiwa kimazingara linawezekana kweli?
  • Au rafiki yangu aliingiwa na tamaa?
Nawakaribisha mawazo yenu.
Alikusoma na kuona kuwa wewe ni mjinga na unafaa kupigwa. Hamjifunzi tu? Unampa mtu fedha ahangeike kulima na taabu nyingine zote halafu akuletee fedha nyumbani! Maisha siyo rahisi namna hii.
 
Mkuu ni changie kidogo kwa uzoefu wangu.

Kwanza kubali dawa zipo na hii mimi sibishi. unaweza lima na usitoe hata gunia kwa heka yaani
mazao yako yanaenda mazima mazima {kuhamishwa}

wasuku na hao wanyamwezi wanaroga hadi viazi yaani shina la kiazi unaliona limenawili bala
ukichimba unakutana na mizizi tu bila kiazi ili hali jirani yako wa ng'ambo yeye ana[ata vya kutosha.
sio viazi tu na mazao ni mazao yote.

Nenda hadi kule mliko limia jifanye unakodi kisha uliza wenyeji kuwa kwa wastani heka inatoa magunia mangapi?
baada ya hapo akikuambia muulize aliyekuwepo mwaka jana hapa mbona alipata magunia 7 kwa heka zote saba?

Hapo atakuambia ukweli wote kama kuna uchawi { hakutengeneza shamba} atakuambia ama kama alipata zaidi utaambiwa pia. usiishie huyo tu uliza zaidi ya watu4 hasa vibarua walio husika kuvuna lazima utawapata tu
Wewe ndiye member nanga kuliko wote hapa JF kwa haya mawazo ya kijinga uliyonayo.
 
Ulifanya kilimo cha online mkuu ukasubiri ufanyiwe delivery ya Faida?? pole sana ila kiukweli mwenzio kakupiga
 
Dah yan nimetoa hela nying sana zaid ya 2.5m
Uwe unafika shambani kiongozi.....Hizo story huku usukumani ni kawaida sana kuibiwa shambani kimazingara ila sio Kwa kiwango hicho, pia Kuna wizi tu wa kawaida masimela wanavizia tu hamjaenda kulinda wanapita nao yaani wanauvuna kabisaaa..ila kupigwa gunia zote hizo "kitamaduni" hakuna...
 
Hizo stori kwenye mazao ni zakawaida, hapo umepigwa hakuna uchawi. Hata kwenye walanguzi wa mazao wanapigwagwa saaana Kwa staili ya kumtuma MTU akaku langulie mzigo eti wewe uko bize na mambo mengine.
 
Habari wana JF,

Nimeleta uzi huu kwenu ili nipate msaada wa mawazo.

Kuna rafiki yangu wa muda mrefu zaidi ya miaka 15 ambaye alinishirikisha kuhusu kilimo cha mpunga huko Tabora. Nilipokea wazo hilo na tukakubaliana kushirikiana. Tulikodi ekari 8 na kufanikiwa kupanda mpunga. Japo muda mwingi yeye ndiye alikuwa akiangalia maendeleo ya shamba kutokana na mimi kuwa na majukumu mengi kazini, nilichangia gharama kwa asilimia kubwa sana.

Muda wa mavuno ulipowadia, nilipanga kwenda kushiriki lakini sikuweza kupata ruhusa kazini. Hivyo, ilibidi rafiki yangu aende peke yake. Alipofika shambani, alikuta mpunga umekomaa vizuri, na makadirio yalionyesha tungepata gunia 120 au zaidi. Hata hivyo, baada ya mavuno, alinipa taarifa kwamba magunia yaliyopatikana ni saba (7) tu kutoka ekari zote 8.

Nilipouliza sababu, aliniambia kwamba mpunga umeibiwa kimazingara (uchawi). Sasa naomba kuuliza:

  • Je, hili jambo la mpunga kuibiwa kimazingara linawezekana kweli?
  • Au rafiki yangu aliingiwa na tamaa?
Nawakaribisha mawazo yenu.
Kwa tuliowahi kuishi pande hizo yote mawili yanawezekana.Kule watu hawalimi bila dawa.Niliwahi kulima karanga eka 2 nikapata debe 5
 
Habari wana JF,

Nimeleta uzi huu kwenu ili nipate msaada wa mawazo.

Kuna rafiki yangu wa muda mrefu zaidi ya miaka 15 ambaye alinishirikisha kuhusu kilimo cha mpunga huko Tabora. Nilipokea wazo hilo na tukakubaliana kushirikiana. Tulikodi ekari 8 na kufanikiwa kupanda mpunga. Japo muda mwingi yeye ndiye alikuwa akiangalia maendeleo ya shamba kutokana na mimi kuwa na majukumu mengi kazini, nilichangia gharama kwa asilimia kubwa sana.

Muda wa mavuno ulipowadia, nilipanga kwenda kushiriki lakini sikuweza kupata ruhusa kazini. Hivyo, ilibidi rafiki yangu aende peke yake. Alipofika shambani, alikuta mpunga umekomaa vizuri, na makadirio yalionyesha tungepata gunia 120 au zaidi. Hata hivyo, baada ya mavuno, alinipa taarifa kwamba magunia yaliyopatikana ni saba (7) tu kutoka ekari zote 8.

Nilipouliza sababu, aliniambia kwamba mpunga umeibiwa kimazingara (uchawi). Sasa naomba kuuliza:

  • Je, hili jambo la mpunga kuibiwa kimazingara linawezekana kweli?
  • Au rafiki yangu aliingiwa na tamaa?
Nawakaribisha mawazo yenu.
Hapo Umepigwa babu,je uliwahi kuliona shamba baada ya kupanda mpunga,? Maana hapa naona kabisa dalili kuwa uliigwa kuanzia hela ya kukodi Hadi kuvunia kwa maana ya kwamba shamba hakulima
 
Back
Top Bottom