Je mtaji wa ml.8 unatosha kufuga layers 600 mpaka waanze kutaga?

MZIGO HUU APA KARIBUNI CALL US 0781647066:
S&Q GROUP INTERNATIONAL LIMITED KWA KUKU BORA
1734810374135.jpeg
 
Inaweza tosha kwa kubana bana sana, kuku 100 wale angalau milion 1 na point hadi kuanza kutaga.

kuku 600 angalau milion 6+ inaweza watosha.

Hapo ni chakula pekee make chakula ni asilimia 70 ya gharama zote za ufugaji.
nashukuru mkuu kwa ufafanuzi,je ni kampuni ipi ni bora kwa vifaranga vya layers kwa uzoefu wako
 
Shukran mkuu. Kwa uzoefu wako hyo 8ml inaweza faa idadi gani. Na vp kampuni za vifaranga vizuri
Weka 400, kampuni za Vifaranga zipo nyingi lkn nakushauri chukulia silverland. Chakula uwe wanunua cha NASSAD kwa hapo Tanga kwa uzoefu wangu maana mitaa hio nimewah kufuga.
 
Inaweza tosha kwa kubana bana sana, kuku 100 wale angalau milion 1 na point hadi kuanza kutaga.

kuku 600 angalau milion 6+ inaweza watosha.

Hapo ni chakula pekee make chakula ni asilimia 70 ya gharama zote za ufugaji.
Usimdanganye mwambie ukweli tu kwa kuku 600 hiyo pesa haitoshi pia usiingie kichwa kichwa hii biashara inataka ujuzi na uvumilivu hasara na Faida zinakaribiana sana.
 
Weka 400, kampuni za Vifaranga zipo nyingi lkn nakushauri chukulia silverland. Chakula uwe wanunua cha NASSAD kwa hapo Tanga kwa uzoefu wangu maana mitaa hio nimewah kufuga.
Shukran sana mkuu muongozo,Vp kuhusu kumix chakula wakiwa wakubwa kwa jamii hii ya layers. Au ni watakula special food maisha yao yote
 
sawa mkuu, je kwa uzoefu wako hiyo bajeti inafaa kwa idadi gani. Waweza kuweka ABC kama hautojali
 
8M kwa ufugaji wa kuku wa mayai (layers) 600, hiyo pesa haitoshi. Huo ndio ukweli mchungu, hao wanao kwambia inatosha hawana uzoefu wowote ule na ufugaji. Wana andika tu kwakuwa wameona ni 8M basi wakajua inaweza tosha.

Ufugaji wa kuku wa mayai (layers) una hatua nyingi mpaka kufikia kuku kutaga. Kwa wastani kifaranga mmoja anahitaji si chini ya Tsh 15k kwa matumizi mpaka kufikia kutaga, hivyo kwa kuku 600 unahitaji uwe na wastani wa Tsh 9M mpaka 10M. Hiyo pesa ni kwa ajili ya ununuzi wa kifaranga, chakula, chanjo na madawa. Banda inabidi uwe nalo tayari, hiyo pesa haihusiani na ujenzi wa banda.

Kwa ushauri mwingine, ni vizuri zaidi ukaanza na kuu 200 ili kupata uzoefu na kujifunza zaidi. Haishauriwi unapo anza kuanza na idadi kubwa ukiwa mgeni kwenye sekta hiyo, anza na kidogo utakuwa unaongeza kidogo kidogo mpaka kufikia idadi unayo itaka. Kila la kheri na karibu.
20241023_083712.jpeg
 
8M kwa ufugaji wa kuku wa mayai (layers) 600, hiyo pesa haitoshi. Huo ndio ukweli mchungu, hao wanao kwambia inatosha hawana uzoefu wowote ule na ufugaji. Wana andika tu kwakuwa wameona ni 8M basi wakajua inaweza tosha.

Ufugaji wa kuku wa mayai (layers) una hatua nyingi mpaka kufikia kuku kutaga. Kwa wastani kifaranga mmoja anahitaji si chini ya Tsh 15k kwa matumizi mpaka kufikia kutaga, hivyo kwa kuku 600 unahitaji uwe na wastani wa Tsh 9M mpaka 10M. Hiyo pesa ni kwa ajili ya ununuzi wa kifaranga, chakula, chanjo na madawa. Banda inabidi uwe nalo tayari, hiyo pesa haihusiani na ujenzi wa banda.

Kwa ushauri mwingine, ni vizuri zaidi ukaanza na kuu 200 ili kupata uzoefu na kujifunza zaidi. Haishauriwi unapo anza kuanza na idadi kubwa ukiwa mgeni kwenye sekta hiyo, anza na kidogo utakuwa unaongeza kidogo kidogo mpaka kufikia idadi unayo itaka. Kila la kheri na karibu. View attachment 3186544
Mkuu nashukuru kwa ushauri. Itabidi nianze kwanza na idadi ndogo
 
Back
Top Bottom