Wadau,
Naomba kupata maoni yenu ya nani anafaa kuiongoza Tanzania Mpya kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia December 2010? Kama ningepewa nafasi ya kumchangua mtanzania mwenzangu agombee basi ningemuomba Dr. Salm Ahmed Salm achukue form. Yeye ndiye alifaa awe Rais wa Tanzania baada ya Mkapa, lakini kwa bahati mbaya propaganda za kifisadi zilitukosesha nafasi ya kumpatia ridhaa hiyo. Je umri wake umemtupa mkono? Sidhani, Mandela alichaguliwa rais akiwa na umri mkubwa zaidi ya alionao Salm sasa, na akisikia maombi yangu atatufaa kututoa katika siasa za makundi za CCM ya sasa na kutupeleka katika Tanzania ambayo kila mmoja wetu anaitaka, na kwa kuwa umri umemtupa mkono hataweza kung'ang'ania kama ambavyo JK anataka kufanya kwa propaganda za kifisadi zisitusaidia.
Kwa upande wa upinzani, naomba niwe mkweli ni Dr. Slaa pekee ambaye naona anaweza kutuongoza. Je maoni yenu ni yapi wadau?