Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?

  • Jakaya Mrisho Kikwete (CCM)

    Votes: 591 23.9%
  • Willibrod Slaa (CHADEMA)

    Votes: 1,785 72.1%
  • Ibrahim Lipumba (CUF)

    Votes: 89 3.6%
  • Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi)

    Votes: 7 0.3%
  • Mutamwega Mugahywa (TLP)

    Votes: 7 0.3%

  • Total voters
    2,475
  • Poll closed .
kwani mnataka rais tajiri tu au uwezo wake? rais ni mfumo
 
Kingunge Ngomable Mwiru anafaa kuwa rais wetu 2010
 
Bi Kidude anafaa. Mtu wa watu, hana makuu, anakubalika kwenye jamii.
 
NINJA
lakini unadhani mikiki mikiki ya urais ataweza kukabiliana nayo kwani tz ya sasa imebadilika sana
 
NINJA
lakini unadhani mikiki mikiki ya urais ataweza kukabiliana nayo kwani tz ya sasa imebadilika sana

Kwa jinsi TZ ilivyobadilika, hakuna anayemfikia kwa ubora. kazi ngumu kwake itakuwa kusafiri na kutia sahihi. Mikiki mikiki si taabu sana, spika wa bunge akiwa Khadija Kopa atamsaidia sana hasa kwa mipasho.
 
Tanzania ya leo inahitaji mtu muadilifu na mkatili, ambaye hatashindwa kuwanyonga wezi wa mali ya umma.
 
Tanzania ya leo inahitaji mtu muadilifu na mkatili, ambaye hatashindwa kuwanyonga wezi wa mali ya umma.

Hapa labda tubinafsishe kwa wachina. Baada ya wiki tu baraza la mawaziri la sasa watabaki manaibu tu. mawaziri wote watakuwa wamenyongwa. Halafu manaibu wote watajiuzulu. Kuteuliwa uwaziri itakuwa kama kuchaguliwa kwenye kikosi cha kutegua mabomu.
 
Wadau,

Nimekuwa nikifuatilia mijadala inayoendelea katika forum hii. Nataka kutoa changamoto kwa wadau wenzangu ili tujadili swali lifuatalo:

Je, ni mtanzania gani ana SIFA na VIGEZO vya kuiongoza Tanzania? Wachangiaji wanaweza kupendekeza majina MATATU.

Itakuwa vyema kama wachangiaji watatoa sababu zinazowafanya watoe mapendekezo hayo?

Nawasilisha hoja.

Rais bado atatoka CCM , Wapinzani bado hawajakaa vizuri, Sasa hivi Mzee Mapesa anampigia debe JK. Mrema naye yuko kwa JK. Hao ndiyo wapinzani wenye sauti kidogo. Anabakia Mbowe na chama chake , Kuna tetesi za Baregu kugombea kupitia CHADEMA. Swali linakuja je Baregu atapishwa na Mbowe?
Lakini tusisahau kuwa kamati ya Mwinyi bado haijatoa ripoti, Pia hatima ya makundi katika CCM. Je wale wanampinga JK wataendelea kumpinga mpaka dakika ya mwisho? Wataenda na ajenda gani kwa NEC na CC katika vikao vya kupitisha wagombea( Urais na Ubunge).
 
kwanza awe ni mtu mwenye kijitambua na kutambua, na mwenye kuzijua hasa alama za nyakati
 
Mimi hapa nafaa kuwa Rais wenu 2010.

sababu nimechoka na uongozi usiokidhi mahitaji ya wananchi na ufujaji mali za nchi ikiwa ni pamoja na kuishi kwenye nyumba za mabilioni wakati jirani yako just few meters mbele anaishi kwa rent ya elf tano sijui kumi na hana uhakika kama atalala amepata dinner.

Nimechoka kuona uongozi usiokuwa sensitive na malalamiko ya wananchi. miaka nenda rudi tuko pale pale kiuchumi kisiasa hata kama kuna mabdaliko yanakuja kwa desimali na sio asilimia inayoeleweka ambayo wananchi tunaeza kuifeel kwamba kweli kuna mabadiliko.

in general am tired of everything in this dear country of ours and if you choose me to be your president nitaiendesha kidikteta mpaka watu wakomae akili ujinga ujinga sitaentertain kabisa posho za kukaa bungeni why wakati ni sehemu yako ya kazi inakuwa included in a salary package yako???
 
kaka itabidi tujiulize amepata wapi fedha za kununua uongozi wetu , kwani nasikia bongo tunauza vyeo vya kisiasa na utendaji,
 
Edward+Moringe+Sokoine.jpg


Mwaka 2010 hakuna mwingine ni Bw. Edward Moringe Sokoine.

 
Wadau,

Nimekuwa nikifuatilia mijadala inayoendelea katika forum hii. Nataka kutoa changamoto kwa wadau wenzangu ili tujadili swali lifuatalo:

Je, ni mtanzania gani ana SIFA na VIGEZO vya kuiongoza Tanzania? Wachangiaji wanaweza kupendekeza majina MATATU.

Itakuwa vyema kama wachangiaji watatoa sababu zinazowafanya watoe mapendekezo hayo?

Nawasilisha hoja.

asiyependa mapato na maisha ya udhalimu
 
Nimesikiliza wimbo wa mjomba katika thread iliyopostiwa na Mzeemwanakijiji. Nimehuzunika sana, machozi yamenitoka. BONYEZA HAPA kuisoma thread hiyo.

Nimeamua kukuuliza wewe MwanaJF unadhani ili hii nchi itoke hapa ilipo inapaswa kutawaliwa na mtu wa namna gani kati ya hawa
1 - Dikteta
2 - Bogus politicians kama ilivyo sasa
3 - Watawala wa sasa
4 - ................................
5 - .................................
7 - ..................................

please endelea, bado nafuta machozi
 
(taifa litakombolewa na kila mwananchi sio zito pekeyake) ukombozi wa nchi hauna uhusiano wowote na madaraka


Inawezekana kama tukiwa na Tumaini Moja na kwa kumtumaini Mwenyezi Mungu(S.A.W).Inshallah tutafika !
 
Mi na utajiri wangu lazima niongoze Tanzania.. We need leadership for all, not the rich, not the poor. We just need serious leadership. That is what lacks, sio wezi, sio wasanii, watu ambao wako tayari kufanya chochote kitakachobidi kuiinua Tanzania ikawa na nafasi katika dunia hii ya kare ya ishirini na moja na ile ijayo ya 22.
 
....Kwa mawazo yangu binafsi mimi ningependa kuona wanahabari na wanaharakati kama kweli tunataka mapinduzi ya halisi basi tuanze kwenye mizizi ya matatizo haya ambayo ni sisi WANANCHI WENYEWE WAKATI WA KUPIGA KURA....Tuanze kwa kuwaelimisha wapiga kura kuanzia kitongoji hadi kitongoji..kata hadi kata..kijiji hadi kijiji..wilya hadi wilaya na mkoa hadi mkoa na mwisho kitaifa...Huu ndio utakuwa ufaumbuzi wa kudumu kwa jinsi navyoona hapa suala si nani ana kashfa gani bali jee sisi wapiga kura tunaulewa gani nini madhara ya kuchagu pumba itakuwa ni sawa na kujaza maji kwenye gunia kusema huyu ni mbaya...mara huyu anatuhumiwa na kesi ya rada ..huyu naye anapenda kubembea pasipo kujipanga na kuelimishana kwa mapana ili kuokoa Taifa LETU...kwa nini huu muda tusiutumie kwa kumwelimisha yule ambaye hajui nini hatima ya maisha yake kama atamchagua kiongozi ambaye si sahihi kwa ufupi Kiongozi FISADI WA MALI ZAUMMA AU KIONGOZI FISADI WA ELIMU YAKE BINAFSI na nini madahara ya kuendelea kuchagua haya madabwada tuliyazoea...Yote ya matatizo yote haya ni sisi wenyewe wananchi kwa kupenda kusahau matatizo ya miaka mitzno au zaidi na kushabikia takrima za khanga na miche ya sabuni kwa muda wa kampeni za uchaguzi tuu.. Nina uhakiaka kama elimu tosha ya kupambanua mambo itapenyezwa ndani ya vichwa vya sisi wadanganyika TUTASHINDA NA KUONDOA UONGOZI DHALIMU MADARAKANI...
 
Wadau,
Naomba kupata maoni yenu ya nani anafaa kuiongoza Tanzania Mpya kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia December 2010? Kama ningepewa nafasi ya kumchangua mtanzania mwenzangu agombee basi ningemuomba Dr. Salm Ahmed Salm achukue form. Yeye ndiye alifaa awe Rais wa Tanzania baada ya Mkapa, lakini kwa bahati mbaya propaganda za kifisadi zilitukosesha nafasi ya kumpatia ridhaa hiyo. Je umri wake umemtupa mkono? Sidhani, Mandela alichaguliwa rais akiwa na umri mkubwa zaidi ya alionao Salm sasa, na akisikia maombi yangu atatufaa kututoa katika siasa za makundi za CCM ya sasa na kutupeleka katika Tanzania ambayo kila mmoja wetu anaitaka, na kwa kuwa umri umemtupa mkono hataweza kung'ang'ania kama ambavyo JK anataka kufanya kwa propaganda za kifisadi zisitusaidia.

Kwa upande wa upinzani, naomba niwe mkweli ni Dr. Slaa pekee ambaye naona anaweza kutuongoza. Je maoni yenu ni yapi wadau?
 
Back
Top Bottom