Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?

  • Jakaya Mrisho Kikwete (CCM)

    Votes: 591 23.9%
  • Willibrod Slaa (CHADEMA)

    Votes: 1,785 72.1%
  • Ibrahim Lipumba (CUF)

    Votes: 89 3.6%
  • Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi)

    Votes: 7 0.3%
  • Mutamwega Mugahywa (TLP)

    Votes: 7 0.3%

  • Total voters
    2,475
  • Poll closed .
I wish iwe hivihivi kwenye on the election day. I am sooooooooooooooooooooooooooooooooooo fade up of CCM. They make me sick.
 
Simfahamu vizuri Dk. Slaa siwezi kugarantii uwezo wake lakn nafikiri yeye na chama chake ndio mbadala sahihi wa CCM kwa sasa.
CCM wanafikiri watanzania bado ni wajinga sana kutokana na kauli na majigambo yao.
Wananiudhi, wanakera.
Tukiwapiga chini hata msimu mmoja tu wataelewa kuwa tumeamka na si wajinga tena.
Hawataacha kushughulikia kero zetu ili wazitumie kwenye kampeni maana wanajua mwerevu na aliyeendelea hatawaliki, hawadanganyiki.
Tuamke wakati wa mabadiliko ndio huu.
 
Raia Wa Tanzania, mwenye miaka zaidi ya 35, ana akili timamu, hajawahi kushtakiwa kwa uhalifu, na anayependekezwa na chama cha siasa.

Yaleyale, ya kuzuia wagombea huru au binafsi. By the way miaka 35 ndiyo nini? Kwani akina Alexander the Great walikua na miaka mingapi walipoanza kutawala?
 
Nawashukuru wanajamii. Mimi ni mara yangu ya kwanza kushiriki jukwaa hili murua kabisa. Nafarijika kujikuta niko miongoni mwenu wana wa nchi mnaosumbuka kufikiri namna bora ya kuifanya inchi yetu isonge mbele. Kwa kuzingatia mada iliyopo, Ningependa Tanzania ipate Rais ambaye anathubutu kufanya maamuzi katika uongozi wake, kufanya maamuzi nai hatua muhimu ya kusonga mbele katika kushughulikia matatizo mbalimbali yanayokuwepo katika nchi. Pili ninapenda Tanzania ipate Rais, ambaye uongozi wake hauzingatii urafiki katika kupewa nafasi ya kuongoza eneo fulani bali rais ambaye kwake sifa kuu ya mtu kupewa uongozi ni kuwa mchapa kazi na mtu asiye wa NDIYO MZEE. Tunahitaji Rais ambaye ana maono kuhusu Tanzania ijayo, atuambie anataka kuipeleka wapi Tanzania kimaendeleo katika nyanja za jamii, kiuchumi, kimazingira na kiuchumi. Tunataka Rais, ambaye kwa kinywa chake anathubutu kuonesha ni kwa namna gani anakerwa na UFISADI na madaraja yanayojengeka katika jamii yaani ( wenye nacho na wasio nacho). Tunataka Rais, kwa namna ya pekee kabisa yuko tayari kuona kwamba udhaifu wa Katiba ya nchi ni sehemu ya kikwazo kikubwa cha kukwama kwetu katika kupiga hatua za kimaamuzi na hivyo kuathiri maendeleo ya nchi kwa ujumla wake. Mwisho tunahitaji Rais, ambaye kwake Tanzania na Watanzania ni namba moja katika kupanga na kutekeleza mipango yoyote ya kimaendeleo, hivyo atakuwa tayari kulinda na kuhifadhi rasilimali za nchi kwa ajili ya vizazi vijavyo. Kwa sababu hizi nilizozitoa hapo juu, na nikizinagatia hiki ni kipindi cha kuelekea uchaguzi, ninaamini na kushawishika kutoka nafsini mwangu kwamba DR.SLAA ndiye anatufaa kuwa Rais kama mtanzania mwenzetu.
 
Kura yako ya urai mpe kikwete,alafu ya udiwani na ubunge wape wapinzani.
 
Kwa kuwa mara nyingi Watanzania huwa hatuko makini na mambo muhimu inatulazimu tutumie zaidi ya miaka mitano kufikiria jina la rais anayetufaa kuongoza nchi.....wakati ttukiendelea kuwaza tumwachie kwanza Kikwete amalizie anachodhani amekibakiza then by that time tutakuwa tumempata mwenye uwezo wa kuongoza nchi hii; tusingelipenda kufanya majaribio kwenye post nyeti kama hii.

Sidhani kuwa unachokiandika hapa unakimaanisha ndugu yangu. Kuna wakati nilikuwa nafikiria kuwa hata miaka mitano ambayo JK amekuwa Rais ni mingi sana.

Haiwezekani tukawa na subira hata kama tunaona mambo yakiharibika. Uchaguzi ni nafasi nyingine tunayopewa ya kuchagua kuendelea na uovu, uzembe na ubadhilifu ule ule au kubadili na kuanza upya au kuweka mtu anaeweza zaidi. Nafasi hii siwezi kuitumia kumchagua Rais wa CCM mwaka huu. Nafsi yangu itanisuta.

Hakuna majaribio mabaya kama ya kuendelea kumwachia mtu alionyesha kushindwa kabisa kutawala. Rais wetu alishasema kuwa, ametumia miaka mitano ya kwanza kujifunza. Sijaona na kujihakikishia kuwa ameelewa mafunzo aliyopata kwa miaka mitano aliyokuwa madarakani.

Nafasi ya uRais haiitaji mtu anaekwenda kujifunza. Kama ilivyo nafasi yoyote yenye heshima na nyeti katika taasisi yoyote, URais unahitaji mtu mwenye uwezo, nia na namna ya kutekeleza majukumu ya nafasi hiyo kwa ukamilifu. Kwa vyovyote vile, Dr. Slaa anaweza zaidi ya JK, hata kama JK atajifunza kwa miaka mingi mingine.

Unajua Dalili za mvua ni mawingu, na uwezo wa uongozi huanza katika familia then kwenye chama hatimae taifa. Sasa hizo SILAHA nyumbani zimekwishawalipukia watoto, kwenye chama zimeuzwa kwa bei rahisi marikiti; zinakwenda sasa zinafyatuka tu(hazina control) halafu tuzipeleke Ikulu...anyway tusingelipenda Somalia ya pili........uongozi na jazba no.............kama tumekosa mtu basi tumpe mama Maria Nyerere atawale nchi kwa jina la mmewe tutadumu japo mwezi baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.

Hii nadhani ni kejeli tu.
 
Nionavyo, swala la msingi zaidi ni "Tufanyeje ili tupate uhuru wa kweli wa kufanya maamuzi yetu, na sio huu wa sasa wa bendera tu?". Endapo tutaendelea kutegema wafadhili ( wahisani, development partners nk), kamwe hatutajikomboa toka dimbwi la utegemezi. Hivyo, tutaendelea kuwa watumwa tu (tena vibaya zaidi watumwa wa kifkira) na kutekeleza mikukuta!!
 
Bw.Dotori pamoja na Wadau wote naomba nianze kwa Kuomba Samahani,na Msamaha huu ni kuwa ntatoka nje ya Mada hii Kidogo.

Tumekuwa hadi hii Leo na Viongozi(Watawala) tulowachagua ktk Awamu nne tofauti(Zingatia Kung'atuka kwa Mwalimu)ndani ya misingi 'safi kabisa ya Kidemokrasia',na dhamira Kuu ya Watanzania wote kwa kuwachagua Watawala hawa ni ili basi watujengee Mazingira na Misingi bora Tujikwamue katika Dimbwi la Umasikini wa: Hali, Kiakili, Mali.

Tofauti yake ni kwamba:

Dimbwi hili la Umasikini limekuwa likiongezeka KINA kila Awamu,na watanzania walio Vijijini na hata Mijini, wazidi Kuzama kwasababu ya Afya Duni,Ujinga na Ulofa ulokidhiri,matokeo yake
Watanzania tunaishi Kimiujizaujiza tu,hakuna mipangilio,bora Liende!kwa mfano:Upo ndani ya daladala, kwa wale tunaoishi kati ya maeneo ya Magomeni(Mapp) na Fire, kila siku ya Mungu Unaona Kundi la watu,hawana vikapu mikononi,mabegi,au hata Ndoo za maji basi, likiwa kwa miguu linakatiza maeneo ya jangwani linaelekea katikati ya Jiji,watu wanajikusanya na kukaa katika vikundi ili kupiga Gumzo tu(Vijiweni)kwa kweli Nnajiuliza Maswali mengi sana pasipo majibu!!

Kuna usemi kuwa Muda kamwe Hauongopi!
Labda ni Uzee Unaingia au napatwa Na Wendawazimu sijui!,lakini yapata Miaka 40 hivi, kwa kweli sijaona Umuhimu/Sababu ya KUWA NA RAIS NCHINI TANZANIA.Nnaelekea kufikiri basi hata tukaweka PAKA MWITU pale Ikulu,bado hilo li-Nchi litakwenda tu!!

Ukweli ni kwamba sisi watanzania wenyewe naona tunajitakia huu umaskini!
nasema hivyo kwa sababu watanzania tumekuwa tukifumbia macho matendo yakidhalimu yanayofanywa na viongozi wetu kufikia hatua hata nchi zingine wanatushangaa. tanzania inasifika kwa kuweka mipango madhubuti lakini isiyotekelezwa hata siku moja. tumekuwa tukikubali kusukumwa na nch tajiri na tunanyamaza. nashindw kuelewa hizi nchi ndo zilizo wasaidia kuingia madarakani au kipi hasa chanzo. suala la EPA limezimwa kiaina bila hata maelezo, kesi ya RICHMOND haijulikani imeishia wapi. hebu watanzania wenzangu mseme wenyewe kweli hii ni halali? kwa tetesi nlizopata ni kwamba zile pesa za account ya madeni ya nje zingeweza kuwasaidia watanzania kupunguza umaskini kwa kias cha 50%. sasa si tungejikwamua kiuchumi kabisa? na cha kushangaza zaidi utaona wananchi hao hao wanaolalamika kuhusu maisha kuwa mabaya watawapa tena viongozi walewale madarake waendelee kuitafuna nch.

AU NDO ULE MSEMO USEMAO ZIMWI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKWISHA?????????????
 
Mtanzania anayefaa kuwa Rais wa Nchi (Tanzania) kwa 2010 hadi 2015 anatakiwa awe na sifa zifuatazo:

  1. Amjuwe Mwenyeezi Mungu
  2. Awe na mwenendo muruwa (mwema) katika maisha yake ya wazi (na ya siri)
  3. Awe na heshima na taadhima kwa watu
  4. Awe na uwezo wa kupanga mipango mahsusi kwa maendeleo ya watu na vitu
  5. Awe na uwezo wa utumizi makini wa hekma na busara
  6. Awe na akili na maarifa ya kujiongoza, kuongoza watu wengine kwa haki, uadilifu na usawa (insafu)
  7. Awe na uwezo wa kujali anaowaongoza
  8. Awe tayari kujitoa muhanga kwa haki kwa ajili ya anaowaongoza
  9. Awe na uwezo wa akili ya kujitambua na kujitambulisha kwa haki si kwa kibri au misifa
  10. Awe na uwezo wa akili ya kujikosoa na kukubali kukosolewa
  11. Awe mkweli msadikivu na asimamie ukweli unaoaminika ni kweli
  12. Awe na elimu sahihi ya watu na mazingira
  13. Asiwe na tamaa, pupa na harara ya kupupia mali kwa njia za kifisadi
  14. Awe timamu kiafya (akili, mwili na roho)
  15. Awe na umri unaomtofautisha na watoto na wazee waliyepitiliza (miaka 35 hadi 70)
  16. Asiwe na madoa ya matumizi ya ubabe, umafia au uzuvendi wa kijambazi
  17. Awe tayari kufa kutetea haki ya wanyonge (wakulima, wafanyakazi na wananchi masikini)
  18. Awe tayari kurasmisha mali ya asili ya Tanzania (ardhi na madini) kwa Watanzania
  19. Awe tayari kuirejeshea Tanzania heshima na utu wake kwa kuleta mabadiliko ya jumla ya Katiba
  20. Awe tayari kusimamishwa jukwaani na kuadhibiwa pale itakapobainika amekwenda kinyume na "kiapo na ahadi" ya kuwatumikia Watanzania kwa haki, uadilifu na usawa.
 
Bw.Dotori pamoja na Wadau wote naomba nianze kwa Kuomba Samahani,na Msamaha huu ni kuwa ntatoka nje ya Mada hii Kidogo.

Tumekuwa hadi hii Leo na Viongozi(Watawala) tulowachagua ktk Awamu nne tofauti(Zingatia Kung'atuka kwa Mwalimu)ndani ya misingi 'safi kabisa ya Kidemokrasia',na dhamira Kuu ya Watanzania wote kwa kuwachagua Watawala hawa ni ili basi watujengee Mazingira na Misingi bora Tujikwamue katika Dimbwi la Umasikini wa: Hali, Kiakili, Mali.

Tofauti yake ni kwamba:

Dimbwi hili la Umasikini limekuwa likiongezeka KINA kila Awamu,na watanzania walio Vijijini na hata Mijini, wazidi Kuzama kwasababu ya Afya Duni,Ujinga na Ulofa ulokidhiri,matokeo yake
Watanzania tunaishi Kimiujizaujiza tu,hakuna mipangilio,bora Liende!kwa mfano:Upo ndani ya daladala, kwa wale tunaoishi kati ya maeneo ya Magomeni(Mapp) na Fire, kila siku ya Mungu Unaona Kundi la watu,hawana vikapu mikononi,mabegi,au hata Ndoo za maji basi, likiwa kwa miguu linakatiza maeneo ya jangwani linaelekea katikati ya Jiji,watu wanajikusanya na kukaa katika vikundi ili kupiga Gumzo tu(Vijiweni)kwa kweli Nnajiuliza Maswali mengi sana pasipo majibu!!

Kuna usemi kuwa Muda kamwe Hauongopi!
Labda ni Uzee Unaingia au napatwa Na Wendawazimu sijui!,lakini yapata Miaka 40 hivi, kwa kweli sijaona Umuhimu/Sababu ya KUWA NA RAIS NCHINI TANZANIA.Nnaelekea kufikiri basi hata tukaweka PAKA MWITU pale Ikulu,bado hilo li-Nchi litakwenda tu!!

"ha ha ha aaaa paka mwitu?"
 
Nyie vipi? Anne Kilango Malecela for presidency 2010....nani hataki?

Hilo ndo tatizo lenu wabongo kazi ya Kupata mtu mnategemea front page ya magazeti akionekana anapambwa mnaingia mkenge msiangalie umaarufu angalie uadilifu,JK alipambwa sana leo kiko wapi?
 
Mtanzania anayetufaa kuwa rais ni yule ambaye ataweza kudhibiti mfumko wa bei na kutufanya watanzania wengi ambao kipato chetu ni kidogo tusiyaone makali ya maisha. Angalia unga wa ngano ambao kwa hakika sisi tuliowengi hatuwezi kuukwepa maana kama hutoula asubuh ktk kifungua kinywa basi utakutana nao mchana la sivyo kabla ya kulala utaula. Unga huo wa ngano umekuwa ukipanda kila siku nakumbuka kutoka kati ya Tsh. 300/= - 350/= wakati wa Mkapa na sasa kati ya Tsh. 1100/= - 1300/= katika kipindi cha Kikwete. Huo ni mfano mmoja lakini yapo mengi ambayo kwa ufupi naweza kusema mtanzania anayetufaa kuwa rais siyo Kikwete kwani ameshindwa kutufikisha nchi ya ahadi. Nawakilisha.
 
Mods na Wahusike wengine wa huu mjadala.

Unapokuwa na kitu kama hiki, inabidi kuuliza walau kila baada ya mwezi mmoja. Sasa naiona hii imekaa kitambo sasa.

Ingelikuwa vema Muifunge na matokeo yaliyopo muyatunze kwa kumbukumbu.

Mwezi ujao ianzishwe nyingine na hapo itakuwa vema kuona jinsi watu walivyobadilika katika kipindi hiki cha kampeni ua uchaguzi.

Ninaweza kuwa zamani nilikuwa mpenzi wa Kaka yangu Lipumba ila leo hii nimeona kuwa Slaa ndiye anafaa. Kesho ninaweza kugundua kuwa kumbe Slaa ni bomu kabisa na nikahamia kwa Dr. Kikwete. Sasa kama nilipiga kura zamani, haitaleta sura ilivyp baada ya kampeni.

Mchango wangu ni huo kwenye hii thread.
 
Kelly
kwa mtizamo wangu ni kwamba Tanzania bado haijafikia huko kwa kusema raisi awe mwanamke au mwanaume, sisi bado tuko kwenye kutafuta raisi atakae irudisha Tanzania kwenye mstari ulionyooka. Kiukweli tuko nyuma sana, na bahati mbaya hatufanani kuliona hilo katika siku za karibuni, imefikia mahali tunaitwa "wadanyanyika", jamani tufungue macho
 
Ni mtanzania yeyote mwenye maono mazuri na nchi yetu,anayeweza kuwafanya watanzania wanufaike na jasho lao.Wawe na imani na serikali yao,wajiamini kwenye nchi yao,kitu ambacho tunakikiosa wa kipindi chote hicho.
 
Kwa kweli kwa mimi ' Slaa anafaa sana! Tumpe kura!

That is if they will not get stolen!
 
Back
Top Bottom