Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
napendekeza anayeongoza awe wa kwanza kwenye orodha, wa pili na mpaka wa mwisho
Mbona hujampigia kura?anayefaa ni Jakaya Mrisho kkikwete
Anayeongoza kivipi? Unamaanisha mwenye kura nyingi? Maana anayeongoza nchi ni Kikwete na hivyo ndiye aliye wa Kwanza katika orodha! Tafadhari fafanua unataka kifanyike nini? (tutamwomba Moderator afanye kulingana na matakwa ya wachangiaji).
Hofu yangu ni kwamba idadi ya kura inabadilika wakati wowote. Kwa hiyo si ajabu tukamweka mwenye kura nyingi wa kwanza halafu baada ya muda nafasi yake ikachukuliwa na mtu mwingine, tukatakiwa kubadilisha tena. Lakini kama hilo linawezekana (kubadilisha kila baada ya muda fulani) basi moderators watusaidie.Namaanisha mwenye kura nyingi
Ni Dr Slaa
Sababu
1. NI Mzalendo wa kweli
2.Anapenda Watanzania
3.Anajali Maskini
4.Mtetezi wa wanyonge
5. Anasifa kadhaa za Mwalimu
6.Anachukia Ufisadi
7. Hapendi uonevu
8.Anapenda Maendeleo ya Mtanzania
9. Ana Hofu ya Mungu
10. Si mbaguzi
11. Mzalendo wa kweli
12. Anaitakia Mema Nchi yetu
13. Hajajilimbikizia
14. Ni kiongozi wa kweli
15. Bila yeye tusingejua mafisadi
16. Hana woga
17. Kajitoa kutuokoa na wanyonyaji
18. Tukiwa naye nchi itafika mbali
19. Habagui rangi
20 Si mkabila wala mdini!
Hofu yangu ni kwamba idadi ya kura inabadilika wakati wowote. Kwa hiyo si ajabu tukamweka mwenye kura nyingi wa kwanza halafu baada ya muda nafasi yake ikachukuliwa na mtu mwingine, tukatakiwa kubadilisha tena. Lakini kama hilo linawezekana (kubadilisha kila baada ya muda fulani) basi moderators watusaidie.
Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge utakaofanyika October mwaka huu tuna wagombea wengi ambao hadi hivi sasa wameshajitokeza kuwania nafasi ya urais wa nchi. Nafikiri tujaribu kuangalia ni nani atafaa kuwa Rais wa Tanzania kati ya hawa wengi waliojitokeza na kwanini tunafikiri atatufaa. Ni rukhusa kuandika sifa zote ambazo tunazitaka kwa Rais wetu na kuelezea ni nani anazo na nani hana. Ukiweka na sababu kwanini anazo au hana, itapendeza zaidi.
Karibuni tuchangie na tupige kura.
Waliojitangaza hadi sasa ni
Jakaya Kikwete
Wilbroad Slaa
Ibrahimu Lipumba
Mutamwega Mugahywa na
Rungwe
Kama kuna anayemiss mnaweza kuongeza
Kikwete alisema anawajua wala rushwa,wauza madawa ya kulevya,wezi wa EPA waliorudisha fedha(???) na wale wahujumu wa Bandarini lakini kashindwa kuwataja wala kuchukua hatua ilihali yeye tumempa mamlaka yote kikatiba ili ailinde nchi hii na mali zake. Slaa ni mzalendo wa kweli maana pamoja na kuwa hana mamlaka ya kuwafanya lolote Mafisadi lakini kawataja hadharani bila woga au kuumauma maneno ingawa anajua hatari inayomkabili kupambana na watu wa aina hiyo. Huyu akipewa mamlaka ya kuongoza nchi mafisadi,wezi wa mali za umma nk, itabidi wakajichimbie makaburi wajizike wenyewe. Slaa ndio Rais anayefaa kwa wakati huu tulionao.
Sorry, nafikiri kulikuwa na makosa ya kiuandishi. Please mods tusaidieni kuliweka sawa hilo jina kama inawezekana.Mbona jina hili limimeandikwa kwa kifupi?
Mengine yote yapo full name!!
Kwa kweli sijui kama hii program inaweza kufanya hivyo. Lakini kwa ajili ya objectivity pia si vibaya ibaki hivyo ilivyo, asije mtu akawa influenced na nani anaongoza kwa kura.sijui ni program gani inatumika hapo, inaweza wekwa ambayo itakuwa ina update automatically, kama votes zimefungana then majina yao alphabetically
Wote waliosema Dr Silaa nakubaliana nao ila nchi haiongozi na mtu mmoja. Je ana timu ya kumsaidia kuongoza kuanzia Makamu wake, mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya? Hapa namaanisha vile vyeo vya kisiasa.
Kikwete alisema anawajua wala rushwa,wauza madawa ya kulevya,wezi wa EPA waliorudisha fedha(???) na wale wahujumu wa Bandarini lakini kashindwa kuwataja wala kuchukua hatua ilihali yeye tumempa mamlaka yote kikatiba ili ailinde nchi hii na mali zake. Slaa ni mzalendo wa kweli maana pamoja na kuwa hana mamlaka ya kuwafanya lolote Mafisadi lakini kawataja hadharani bila woga au kuumauma maneno ingawa anajua hatari inayomkabili kupambana na watu wa aina hiyo. Huyu akipewa mamlaka ya kuongoza nchi mafisadi,wezi wa mali za umma nk, itabidi wakajichimbie makaburi wajizike wenyewe. Slaa ndio Rais anayefaa kwa wakati huu tulionao.