Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?

  • Jakaya Mrisho Kikwete (CCM)

    Votes: 591 23.9%
  • Willibrod Slaa (CHADEMA)

    Votes: 1,785 72.1%
  • Ibrahim Lipumba (CUF)

    Votes: 89 3.6%
  • Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi)

    Votes: 7 0.3%
  • Mutamwega Mugahywa (TLP)

    Votes: 7 0.3%

  • Total voters
    2,475
  • Poll closed .
Mimi nadhani ni yule atakaye jali maslahi ya taifa na si ya chama chake au jamaa zake au rafiki zake au wafadhili wake au ya kwake yeye mwenyewe.So watanzania tunahitaji uelewa wa hali ya juu sana kumtambua kiongozi kati ya wagombea hawa ambaye ana sifa zenye maslahi kwa taifa.
 
Ni yule mwenye uchu na maendeleo ya taifa. Though it's difficult for most of the p'po to identify who fits
 
mimi nampendekeza sophia simba...
huyu jaman atatupeleka wapi? mimi pia sion kama kuna mwanamke anaweza kuwa rais kwa hapa TZ kwa sasa maana hali ni mbaya sana
inahitajika mtu jasir mwenye uwezo wa uthubutu kwa kukemea mafisadi wazi wazi😛layball::mad2:
 
kikwete anafaa ingawa vigenzo vvya kutokufaa ni vingi. anayo timu ya wasidizi ndani ya chama na amethibitisha kuwa kwa uwezo wake anaweza kufikiria yale anayosema.
slaa anafaa: mapungufu yake ni mengi ukilinganisha na yale anayosema. kila siku amekuwa shabiki wa kusema uovu bila kuonyeesha njia halisi na rahisi. angepata kombination aliyo nayo kikwete basi angekuwa bora zaidi
lipumba ni kiboko; tatizo tuntatengeneza serikali kutokana na vyama vyetu. mtazamo wa CUF na Uislam utawaghalimu na utamghalimu Prof
Wadau,

Nimekuwa nikifuatilia mijadala inayoendelea katika forum hii. Nataka kutoa changamoto kwa wadau wenzangu ili tujadili swali lifuatalo:


Je, ni mtanzania gani ana SIFA na VIGEZO vya kuiongoza Tanzania? Wachangiaji wanaweza kupendekeza majina MATATU.


Itakuwa vyema kama wachangiaji watatoa sababu zinazowafanya watoe mapendekezo hayo?


Nawasilisha hoja:

UPDATE:

Majina Matatu (makubwa) Yaliyopendekezwa:

  1. Jakaya Kikwete - CCM
  2. Willibrod Slaa - CHADEMA
  3. Ibrahim Lipumba - CUF
 
mwenye uchungu na nchi yake.
Anaye jali raslima za nchi yake.
mwenye kutimiza ahadi dhidi ya maagano yake na raia wake hasa kipindi cha kampeni.
inshort,,, mwenye uchungu na nchi yake.

:A S-danger:
 
kikwete anafaa ingawa vigenzo vvya kutokufaa ni vingi. anayo timu ya wasidizi ndani ya chama na amethibitisha kuwa kwa uwezo wake anaweza kufikiria yale anayosema.
slaa anafaa: mapungufu yake ni mengi ukilinganisha na yale anayosema. kila siku amekuwa shabiki wa kusema uovu bila kuonyeesha njia halisi na rahisi. angepata kombination aliyo nayo kikwete basi angekuwa bora zaidi
lipumba ni kiboko; tatizo tuntatengeneza serikali kutokana na vyama vyetu. mtazamo wa CUF na Uislam utawaghalimu na utamghalimu Prof


Kati ya wote nafahamu kuwa JK hafai kuwa Rais. Kiti hicho ni kikubwa sana kwake, kuliko uwezo wake. JK ni mtu mzuri sana, he is man of people, a common joe, our brother, one of us. Lakini kwenye urais JK ni absolutely failure. YOu need to be extremely stupid to say that he deserves to be the president. Wanaosema kuwa JK anafaa au amefanya mazuri, either ni wale wanaotaka kuendelea utamaduni wa miaka 10 wa CCM, [kitu ambacho kwa mtazamao wa mbali si kibaya (as long as Rais anakuwa mzuri)], au wale wanaojua kuwa uwepo wa JK madarakani ni ulaji kwao. wale wanaokula hela kila anaposafiri nje, au ndugu, au wale wanaoendekeza uswahili.

Kwa kuongoza nchi kweli it is hard for JK.
 
Yule ambae atawajali wananchi masikini na kuwaonyesha njia ili waondokane na hali ngumu yakimaisha.Anae wajengea wananchi uwezo wa kujitmbua na kujitegemea si kutegemea misaada tok nje.
 
awe na njozi za kutuongoza kutoka kwenye umaskini hadi kwenye maisha yaliyo bora zaidi
 
Mtu anaepaswa kuwa rais wa tanzania mi naona anapaswa awe na sifa zifuatazo:-
1)awe mtanzania kamili.
2)awe na akili timamu.
3)awe na umri usiopungua miaka 35.
4)awe na uwezo wa kusoma na kuandika.
5)na zaidi ya yote anapaswa awe mwadilifu.
Hizo ndizo sifa za mtu anaepaswa awe rais wa tanzania.
 
Unataka majina au sifa? Kama ni sifa, turejee makala ya Ulimwengu na Hotuba ya Mwalimu Nyerere ya 1995 pale Mbeya. Kama ni majina, hapo tena ni kasheshe!

Turejee na ile hotuba ya Nyerere pale Kilimanjaro hotel siku hizi Kempinsky (mwaka sikumbuki vizuri).
 
Ambaye anaona suala la Urais si la kifamilia! Mwenye uthubutu, utashi - historia yake inavyosema, makini, mwenye fikra za kuondoa umaskini kwa kutumia resources za nchi bila kutegemea misaada na mikopo, mwenye kukemea rushwa na ufisadi, si mwoga, mwenye uelewa mkubwa na ambaye anasoma sana - mfano miswaada kabla ya kutia sahihi kuwa sheria, ambaye anaona kuwa msingi wa kuondoa umaskini Tanzania ni elimu bora ya msingi kwa watanzania wote, ambaye yuko tayari kubadili katiba kutokana na hali iliyopo, ambaye anajua kutenganisha kazi na utani, ambaye anachukizwa na upendeleo kwa misingi ya udini, ukabila, rangi, jinsia, kipato ambaye si mroho na mlevi wa madaraka, ambaye akumbatii matajiri, ambaye ni innovative and creative.
 
MIMI ni mmojawapo wa watanzania ambao tunajua kuonakipi chema na kibaya,kwa kweli kati ya wagomgbea Urais 2010 MHE. DK Jakaya Mrisho Kikwete ndiye anayefaa kuwa Rais kwa awamu nyingine tena kwani amefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa Ilani ya CCM. Hayo amefanikiwa kutekeleza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta za ;
1.Elimu
2. kilimo
3.Afya
4. Miundo mbinu na sekta nyingine
hivyo Mhe. DK. Jakaya Mrisho KIkwete ndiye anafaa kuwa RAIS WETU 2010, nawaomba watanzania wote wajitokeze kumpa kura za ndio tarehe 31 Oktoba,2010 ni YES FOR KIKWETE
 
Nionavyo ni kwamba Tanzania kama Nchi nyingi zilizo masikini ( hata kama ni matajiri wa kutupwa- madini/mafuta/ malighafi/ n.k) daima hufikiria MTU na sio Tunahitaji nini, na Raisi anakuja ili kututoa wapi na atufikishe wapi. Kifupi HATUNA mwelekeo wa wapi tuelekee. Hata H Clinton angemshinda Obama naamini wao kama Marekani wangeendelea kuwa na sera ambazo zisingebadilika sana.
Ni wakati wadau walioenda shule na wanaamini mawazo yao na ndoto zao kwa faida ya ndugu zao hasa wa vijijini.... kujitoa muhanga kuokoa taifa kwa kuingia katika vyama kutoa mchango wao na mawazo yao KIMATENDO na HASA KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI HATA URAISI....
 
Jamani tuwe makini....

Mimi nadhani Kiongozi anayefaa 2010 lazima awe na sifa zifuatazo::
1. Mhadilifu kihistoria,, background yake
2. Anayeheshimu Katiba..
3. Awe na sera ya Utawara Bora kwa viongozi wote wa serikali
4. Atakayefanya marekebisho ya Katiba
5. Atakayewabana Mafisadi wote<<< yaani washitakiwe na kufilisiwa>>>
6. Atakayerudisha Azimio la Arusha...
7. Atakayefufua Viwanda, Shirika la Ndege, Kilimo, Kuondoa Ukiritimba Tanesco, Ewura, Sumatra.
8. Kusimamia Mikataba na kuondoa mikataba mibovu...
9. Kusimamia misingi ya Muungano..
10. Kufufua uchumi na kuondoa matumizi ya dola katika biashara za ndani kusudi kuipa hela yetu dhamani
11. Kusimamia Elimu bora, waalimu shule bora za serikali. Kupata bima ya afya kwa kila Mtanzania, na Afya bure kwa Wazee na watoto
 
CCM bado ndio wanaowza kuongoza nchi, kubali kataa na vilevile ndio uhuru waangu kutamka... Ila nachoweza kusema nikuleta upinzani ndani ya CCM mpaka wanaCCm wajue nini wanaweza kuiletea Tanzania ya leo.... Kinyume na hapo nadhani safari itachukua Muda mrefu... na tutazidi kuwa na majukwaa ya mpito ya upinzani ambao ukiangalia kwa undani ni kama drama amabzo CCM inafurahia... kwahiyo Chagua CCM kwa RAIS na mbunge toa kura zako kwa upinzani ili kuwapa somo wabunge wa CCM na mwisho somo litawafikia walengwa na ndio Muda wamabadiliko utakuwa umefika. Unataka mabadiliko lakni hamna hata mmoja amejiandaa kwa mabadiliko tunayoyaita mabadiliko. Let keep on with our slow pace.
 
DR.SLAA anafaa, mabibi na mabwana habari zenu, sababu za mimi kumchagua slaa ni msimamo wake alionao tangu mwanzo bila ya uoga et kiongizi furani ata mfanya nini, amekuwa na hoja zenye maslahi kwa taifa tangu mwanzo, tumeona jinsi alivyo pambana bungeni kwa maswala ya ufisadi ambapo alichekwa na wabunge wa chama tawala lakini baadaye wakajifanya et na wao ni wapinga ufisadi,

Kwa ujumla ni msimamo wake wa dhat juu ya mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu.
mimi nimejiandikisha na nitapanga foleni mpaka usiku kupiga kura nomatter what so long as i want changes.
 
Jamiiforums mmetutaka tutoe maoni yetu kuhusu mgombea wadhifa wa u-Rais kwa kutuuliza, "Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?"

Tumeitikia; kura tunazidi kupiga. Lakini azima hii nzuri imechafuliwa na chombo pima-maoni (opinion pool instrument) mlicho-design. Ninafafanua:

Mfumo wa kupashana una sehemu kubwa kama nne hivi, ambazo wakati mwingine zinaingiliana ingiliana: Habari (Information); Elimu (Education); Propaganda; na Burudani (Entertainment).

Lengo la utafiti wa maoni ya kutaka kubaini ni nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano (2010-20150, natumaini, lilikuwa ni kuendelea kutoa habari na elimu; na sio propaganda na/au burudani! Lakini ukweli unaojitokeza ni kwamba badala ya kutuhabarisha na kutuelemisha, kinachojitokeza ni propaganda tupu, penda tusipende!

Mosi, majina ya wagombea hayakuwekwa wakati mmoja. Waliowekwa kwanza ili kuwapima kwa kupigiwa kura za maoni walikuwa ni wagombea wawili tu, yaani, Jakaya Mrisho Kikwete (CCM) na Willibrod Slaa (CHADEMA). Baadaye, majina ya wagombea wengine yaliongezwa: Ibrahim Lipumba (CUF) aliingia dimbani akifuatiwa na Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi). Mwisho, aliingia Mutamwega Mugahywa (TLP).

Natumaini Jamiiforums mwanzoni mlikuwa na maana ya kuwapambanisha hao wagombea wawili tu. Manake hamkungoja wagombea wote wapatikane au watangazwe na kampeini zianze rasmi! Matokeo ya kura hii ya maoni haimtendei haki hata kidogo mgombea u-Rais aliyetanguliwa na mpinzani wake katika kuvuna kura za ndio au hapana!

Pili, jumla ya kura pendekeza ya wagombea wote sio ya uhakika. Mpigakura anaweza kupigakura yake ya maoni leo asubuhi, akapiga kura tena mchana, akapiga kura tena jioni, akaendelea kupiga kura kesho, juma lijalo na mwezi ujao hadi hapo kufunga kwa kura hizo eti za maoni, kama anatumia kumputa tofauti! Hili nimelihakiki mimi mwenyewe!

Tatu, ukweli ni kwamba watoa maoni ni population ndogo tu ya jumla ya wapigakura wa Tanzania; sio representative sample! Ni wa-Tanzania wachache tu walio na uwezo wa internet. Mara nyingi ni wale wa mijini na wengine wako ughaibuni (hawatapigakura). Na ikumbukwe kuwa miji yetu (japo ni kama kimbunga) ni non-starter ya kuweza kuleta matokeo ya ushindo katika kupigakura.

Matokeo yanayoonekana, na yanaingilia bongo zetu (yanatongoza psyche), kulingana na usemi wa self-fulfilling prophecy. Yanatufanya tutongozeke na ku-"numb our senses and sensibilities to death." Inaweza kutuonyesha mwelekeo ambao ni tentative tu. Pengine, wanafunzi wa siasa wanaweza kutoyafuatilia kwa makini katika kutamati matokeo ya mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Rais.

Nne, internet ni sans frontières ! Kila anaye-login tovuti ya Jamiiforums out there mmjua Kiswahili anaweza kupigakura hiyo ya maoni, kama akipenda. Anaye-login anaweza kuwa ni M-Korea Kasikazini, m-Kyrgyzstani, m-Amerika, m-Kenya, m-Irani, m-Myanmari, m-Omani, m-Somali, m-Fini, m-Belize, m-Kuba, m-Komoro, m-Fiji, n.k.

Tano, najua Jamiiforums mli-design hiyo chombo pima-maoni (opinion pool instrument) kwa nia nzuri kwamba mtoa maoni angeweza kupigakura mara moja tu. Komputa yake haingemruhusu kupigakura tena; ingemwambia kuwa ameishapiga kura.

Sita, pengine, hamkuzingatia unforeseeable and confounding factors ambazo zingeingilia. Simply put, Jamiiforums hamkupanua mawazo (au mlisahau/mlipuuzia) kuwa mchakato wa siasa unaunda mazingira yanayoweza kuchafulika (the political game is sometimes polluted &#8211; politics is a dirty game).

Saba, chombo pima-maoni (opinion pool instrument) hakina validity, reliabilility na relevancy; matokeo yake sio ya ki-sayansi hata kidogo. Mchakato huu unakuwa mithili ya GIGO (garbage in, garbage out). Kwahiyo, matokeo ya utafiti huu wa kura ya maoni hautoi elimu hata kidogo; unajenga na unaimarisha hisia ya propaganda!

Naomba kufundishwa na Jamiiforums; najidai kuwa na uwezo wa kufundishika!


 
Back
Top Bottom