Jamiiforums mmetutaka tutoe maoni yetu kuhusu mgombea wadhifa wa u-Rais kwa kutuuliza, "Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?"
Tumeitikia; kura tunazidi kupiga. Lakini azima hii nzuri imechafuliwa na chombo pima-maoni (opinion pool instrument) mlicho-design. Ninafafanua:
Mfumo wa kupashana una sehemu kubwa kama nne hivi, ambazo wakati mwingine zinaingiliana ingiliana: Habari (Information); Elimu (Education); Propaganda; na Burudani (Entertainment).
Lengo la utafiti wa maoni ya kutaka kubaini ni nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano (2010-20150, natumaini, lilikuwa ni kuendelea kutoa habari na elimu; na sio propaganda na/au burudani! Lakini ukweli unaojitokeza ni kwamba badala ya kutuhabarisha na kutuelemisha, kinachojitokeza ni propaganda tupu, penda tusipende!
Mosi, majina ya wagombea hayakuwekwa wakati mmoja. Waliowekwa kwanza ili kuwapima kwa kupigiwa kura za maoni walikuwa ni wagombea wawili tu, yaani, Jakaya Mrisho Kikwete (CCM) na Willibrod Slaa (CHADEMA). Baadaye, majina ya wagombea wengine yaliongezwa: Ibrahim Lipumba (CUF) aliingia dimbani akifuatiwa na Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi). Mwisho, aliingia Mutamwega Mugahywa (TLP).
Natumaini Jamiiforums mwanzoni mlikuwa na maana ya kuwapambanisha hao wagombea wawili tu. Manake hamkungoja wagombea wote wapatikane au watangazwe na kampeini zianze rasmi! Matokeo ya kura hii ya maoni haimtendei haki hata kidogo mgombea u-Rais aliyetanguliwa na mpinzani wake katika kuvuna kura za ndio au hapana!
Pili, jumla ya kura pendekeza ya wagombea wote sio ya uhakika. Mpigakura anaweza kupigakura yake ya maoni leo asubuhi, akapiga kura tena mchana, akapiga kura tena jioni, akaendelea kupiga kura kesho, juma lijalo na mwezi ujao hadi hapo kufunga kwa kura hizo eti za maoni, kama anatumia kumputa tofauti! Hili nimelihakiki mimi mwenyewe!
Tatu, ukweli ni kwamba watoa maoni ni population ndogo tu ya jumla ya wapigakura wa Tanzania; sio representative sample! Ni wa-Tanzania wachache tu walio na uwezo wa internet. Mara nyingi ni wale wa mijini na wengine wako ughaibuni (hawatapigakura). Na ikumbukwe kuwa miji yetu (japo ni kama kimbunga) ni non-starter ya kuweza kuleta matokeo ya ushindo katika kupigakura.
Matokeo yanayoonekana, na yanaingilia bongo zetu (yanatongoza psyche), kulingana na usemi wa self-fulfilling prophecy. Yanatufanya tutongozeke na ku-"numb our senses and sensibilities to death." Inaweza kutuonyesha mwelekeo ambao ni tentative tu. Pengine, wanafunzi wa siasa wanaweza kutoyafuatilia kwa makini katika kutamati matokeo ya mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Rais.
Nne, internet ni sans frontières ! Kila anaye-login tovuti ya Jamiiforums out there mmjua Kiswahili anaweza kupigakura hiyo ya maoni, kama akipenda. Anaye-login anaweza kuwa ni M-Korea Kasikazini, m-Kyrgyzstani, m-Amerika, m-Kenya, m-Irani, m-Myanmari, m-Omani, m-Somali, m-Fini, m-Belize, m-Kuba, m-Komoro, m-Fiji, n.k.
Tano, najua Jamiiforums mli-design hiyo chombo pima-maoni (opinion pool instrument) kwa nia nzuri kwamba mtoa maoni angeweza kupigakura mara moja tu. Komputa yake haingemruhusu kupigakura tena; ingemwambia kuwa ameishapiga kura.
Sita, pengine, hamkuzingatia unforeseeable and confounding factors ambazo zingeingilia. Simply put, Jamiiforums hamkupanua mawazo (au mlisahau/mlipuuzia) kuwa mchakato wa siasa unaunda mazingira yanayoweza kuchafulika (the political game is sometimes polluted – politics is a dirty game).
Saba, chombo pima-maoni (opinion pool instrument) hakina validity, reliabilility na relevancy; matokeo yake sio ya ki-sayansi hata kidogo. Mchakato huu unakuwa mithili ya GIGO (garbage in, garbage out). Kwahiyo, matokeo ya utafiti huu wa kura ya maoni hautoi elimu hata kidogo; unajenga na unaimarisha hisia ya propaganda!
Naomba kufundishwa na Jamiiforums; najidai kuwa na uwezo wa kufundishika!