Facts1
JF-Expert Member
- Dec 23, 2009
- 307
- 28
nionavyo mimi, Rais as an individual pekee haitoshi kumfanya mtu afae, nionanvyo mimi. Tunahitaji powerful, effective governing structures kama bunge ambazo zinaweza kumfanya hata rais wa kawaida sana aendeshe nchi kwa namna inavyotakiwa...wabunge wasio watumishi wa serikali, wanaoweza kumdindishia rais na kumwambia kama atafanya hicho au kile, wanaweza kummwaga kwa kura za kutokuwa na imani naye...
Mbalamwezi, basi kama ni hivyo mimi naona wananchi wasiji-involve moja kwa moja kumchagua rais tuwe kama Marekani, wananchi wachague wabunge kama wawakilishi wao bungeni, bunge kama mwakilishi wa wananchi lipendekeze majina matatu na kuyapigia kura angalau moja kutoka chama tawala na jingine toka upinzani, atakayepata kura nyingi ndiye awe rais mshindi wa pili awe makamu wa rais, hii si tu itasaidia kupunguza gharama za uchaguzi pia italifanya bunge kuwa na nguvu kwenye utendaji wa rais.
Kazi itakatakiwa kwa vyama vyote kuhakikisha kinapata wabunge wengi ili kiweze kutoa rais na hata makamu wake.