Je, Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi?

Je, Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi?

Sasa kama haujui funza kafikaje kwenye embe utaweza kweli kujua mungu alikuwa wapi kabla ya kuumba ulimwengu?
Hapa mi nitakuwa sawa na mtu anaelima mpunga kwa lengo la kuvuna mahindi.
Hiyo kazi sifanyi
Siwezi jua huyo mungu(hongera kwa kuabudu mizimu) alikuwa wapi maana ni mungu wako wewe ila Mungu wa kwangu mie najua, bilashaka huwezi fanya iyo kazi maana akili yako imeishia kwenye mahindi mwambie uyo mungu wako akusaidieee ukishindwa muombe kaka mshana akusaidie maana sibishani na waabudu mizimu mie
 
Hapakuwa na 'kabla' kabla muda haujaumbwa. Ni sawa na kuuliza north of north pole! Hauwezi kuuliza kilichokuwepo kabla wakati hiyo kabla inatokana na muda
Kwahiyo Mungu hakuwepo kabla ya muda sio? , Mungu ana Mwanzo?
 
Namaanisha kabla ya ulimwengu kuumbwa, Mungu aliumba ulimwengu na kila kilichomo akiwa wapi? Je, alikuwa Mbinguni? Na wakati anaumba mbingu, alikuwa anaiumba akiwa wapi?
Hili ni swali la Mungu, humu JF tunahusikaje? Namna ya kumpata Mungu na umuulize Hulu swali nahisi unaijua vema tu, sisi humu unatutupia kitu kizito sana Kama nyundo ya utosini
 
Mungu hawezi kuumba wala kufanya chochote.

Mungu hayupo.

Binadamu ndiye alimuumba Mungu kwenye fikra zake.
Unalaaana na muda sio mrefu utakutana naye...Elimu,ujuaji,maisha magumu au mazuri yasikufanye ukamuasi na kumdharau Mungu..katubu mapema kabla jua alijazama
 
Kama Hana mfano Sasa Mungu yule atakayeingiza unyayo wa mguu wake kule Jehanamu siku ya kiama kwa mujibi wa Qur'an huo mguu ameutoa wapi na huo unyayo unafananaje? Mnajiconradict wenyewe kwa hivyo vitabu vyenu sometimes
Wana allah wanamnadi allah wao eti hana mfano sasa huo unyayo hawaoni tayari ashakuwa classified?
 
Ulimwengu huu hakuna aujuwae mwanzo wala mwisho wake.

Mwenyewe kwenye Qur'an anasema yupo karibu na wewe, hujijuwi tu.

Usimfananishe Mwenyezi Mungu na chochote. Unapata tabu kwa sababu ulishaaminisha zile picha za mzungu kuwa ni mungu wako.
Unashangaa picha ila hushangai unavyompigania kwa mabomu as if ni dhaifu huoni tayari ushamfananisha?
 
Hili ni swali la Mungu, humu JF tunahusikaje? Namna ya kumpata Mungu na umuulize Hulu swali nahisi unaijua vema tu, sisi humu unatutupia kitu kizito sana Kama nyundo ya utosini
Sio lazima ujibu.., unaweza ukaacha wenye cha kuchangia wajadili halafu wewe ukabaki msomaji tu..
 
Namaanisha kabla ya ulimwengu kuumbwa, Mungu aliumba ulimwengu na kila kilichomo akiwa wapi? Je, alikuwa Mbinguni? Na wakati anaumba mbingu, alikuwa anaiumba akiwa wapi?
Mkuu. wewe kabla ya kuzaliwa na wazazi wako, je unafahamu ulikua wapi?
 
Sikuwepo popote, nilikuwa sijaumbwa bado
Vizuri Mkuu. Kwa muktadha huo hakuna kiumbe yoyote aliyekuwepo kabla Mungu hajaumba ulimwengu. Viumbe vyote tulikuwepo baada ya Mungu kutuumba. Hivyo, hakuna kiumbe anayejua Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi.

Hivyo Basi, swali ulilouliza halina majibu, kwa sababu hatukuwepo popote, tulikua hatujaumbwa bado na hatujui Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi.
 
Kama huna majibu, we baki kuwa msomaji tu..
 
Namaanisha kabla ya ulimwengu kuumbwa, Mungu aliumba ulimwengu na kila kilichomo akiwa wapi? Je, alikuwa Mbinguni? Na wakati anaumba mbingu, alikuwa anaiumba akiwa wapi?
Kwa ninavyomfahamu Mungu kwa wema, hekima na upendo wake. Ukimuomba kupitia sala bila.kuchoka akuoneshe creation episode atafanya hivyo.

Mimi na wewe tumezaliwa juzi tu hapa. Sasa tunawezaje kukufunulia mambo yaliyojiri miaka mamilionj huko nyuma? Yaani ni sawa kama unaulizia kitanda na godoro vilivyotungia mimba ya babu yako wa kwanza kwenye ukoo.
 
Then clearly humfahamu Mungu, endelea kuwa msomaji tu..
 
Siyo kila anayemfahamu Mungu atajiingiza kwenye mizaha ya kipuuzi.

Omba utamfahamu vyema.

Ninavyomfahamu mimi, hajapata kamwe kubadilika ukuu wake. Inawezekana ukadhani ni nadharia lakini endelea kumtafuta hakika atajidhihirisha kwako
 
Endelea kusoma michango ya wengine tu
 
Back
Top Bottom