Je, Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi?

Je, Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi?

MUNGU alikuwaepo kabla ya hiyo ''Kabla'' kuwepo. Pili MUNGU hana nafasi kwa hivyo huwezi kumpa specific location, ukimpa specific location tayari umeshamlimit. MUNGU ni mmoja hagawanyiki, yeye ndiye mwanzilishi na mmiliki wa kila jambo, hana mshirika katika utendaji wake, hana mwanzo wala hana mwisho,, hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hana mfano wowote na pia hafananishwi na chochote.
Mimi sijakataa, hapo kabla ya kabla, ambapo alikuwa hajaumba chochote, ndio alikuwa wapi? Au hapo alipokuwepo paliumbwa na nani? Maana alikuwa hajaumba kitu bado. Pia hatumpo specific location, tunaulizia generality ya uwepo wake, hata kama ni yupo sehemu zote mida wote, kabla hajaumba kitu, ni wapi alikiwepo, na hapo alipokuwepo , paliumbwa na nani wakati alikuwa hajaumba kitu bado?
 
Kama una hoja zingine zinazo thibitisha kutokuwepo kwa MUNGU zilete, tutakujibu kwa kadiri ya uwezo.
Nani kasema Mungu hayupo? Mbona mnakuwa na biased (subjective) thinking namna hiyo? Wapi nimesema hayupo, nionyeshe
 
Kabla ya kuuliza alikuwa wapi unamfahamu huyo Mungu mwenyewe ni nani?
Si mmesema ni beyond comprehension? Sasa inakuwaje tena unataka nimfahamu? Kikubwa swali ndio nimeuliza hilo, nipate majibu
 
Nafikiri ili MUNGU awe MUNGU basi inatakiwa MUNGU awe kila kitu, awe kila sehemu, awe kila roho MUNGU awe ulimwengu wote uunganishwe na kuwa nafsi hai moja ndipo MUNGU anaonekana.

Tengeneza hiyo picha kichwani mwako.
 
Namaanisha kabla ya ulimwengu kuumbwa, Mungu aliumba ulimwengu na kila kilichomo akiwa wapi? Je, alikuwa Mbinguni? Na wakati anaumba mbingu, alikuwa anaiumba akiwa wapi?
Mungu anasehemu yake na Viumbe wake wanasehemu yake ya Kuishi.

Hakuna anayejua Mungu anakaa wapi wala anaishi wapi.

Kwahiyo huwezi Jua Alikuwa wapi kipindi anaumba Chochote.
 
MUNGU alikuwaepo kabla ya hiyo ''Kabla'' kuwepo. Pili MUNGU hana nafasi kwa hivyo huwezi kumpa specific location, ukimpa specific location tayari umeshamlimit. MUNGU ni mmoja hagawanyiki, yeye ndiye mwanzilishi na mmiliki wa kila jambo, hana mshirika katika utendaji wake, hana mwanzo wala hana mwisho,, hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hana mfano wowote na pia hafananishwi na chochote.
Kwahiyo Kama Hana Mshirika Maana Yake Hawa Manabii na Mitume wote ni Waongo.

Kuanzia Kina Musa..Elia..Yesu.. Mohamedi wote hawa Hana Ushirika nao
 
Mungu hawezi kuumba wala kufanya chochote.

Mungu hayupo.

Binadamu ndiye alimuumba Mungu kwenye fikra zake.
Hongera broo kwa uwezo wako mkubwa wa kufikiria kuwa

Binaadamu alijiumba mwenyewe kisha akihisi kuwa ajajiumba mwenyewe bali yupo aliye muumba
 
Mfano kwenye biashara unapokuwa na Shea oda mwenzio huyo ni mshirika.
Ila wafanyakazi wako HAO sio WASHIRIKA.
NDIVYO ilivyo kwa Mungu Hana washirika.anafanya Mambo yake MWENYEWE
Niambie maana Labda mimi Najua Tofauti ya Mshirika.
 
Haya ni mambo ya imani na kuamin hakuna alie wai kuwaon hao manabii wala M/Mungu kwaiyo ss 2naamin 2. Alieuliz swal hana imani ata umjib vp atazd kuuliza na hatorodhika
 
Mfano kwenye biashara unapokuwa na Shea oda mwenzio huyo ni mshirika.
Ila wafanyakazi wako HAO sio WASHIRIKA.
NDIVYO ilivyo kwa Mungu Hana washirika.anafanya Mambo yake MWENYEWE
Kwahiyo kama Anafanya Kazi Yeye Mwenyewe Ana haja Gani ya Kuwa na Wafanyakazi.

Kama Mungu ni Muweza wa Yote Hana Haja Ya Kuwa na Wafanyakazi wa aina Yeyote
 
Hadith na nadharia za Mungu Zina utata na contradictions kibao,Watu was kwanza kuanza kuanzisha nadharia za Mungu ni wa accient civilization za kale kama Sumerians, Assyrian, Babylon, Egyptian, Kush, Aztec, Maya, Peru, Indus, valley nk
Hawa walianza Hizo nadharia baada ya Dunia kutembelewa na viumbe kutoka nje ya mfumo wetu wa Nyota yaani
ANNUNAK
Hao ndio waliomproject maabara Mwanadamu na kumpa ujuzi wote lengo atumike kama nguvu KAZI ya kuchimba dhahabu,dhahabu ilihitajika na hao viumbe kuizirudisha Sayari zao katika Hali ya kawaida baada ya kuharibiwa na vita vya
Nuclear reactors baada ya viumbe wale kumaliza mission na kuondoka Watu wakaanza waabudu kama Miungu na hata mwanzilishi wa Imani za Abrahamic alitokea Uru ya Ukaldayo Mesopotamia alikua akimuabudu Mungu El au Elohim (YHW)
Huyo alikua ni Moja kati ya Miungu wa Annunak na mapokeo mengi ya wayahudi Yana masimulizi ya sifa za huyo Mungu wao El mpaka pale zilipokuja zaliwa dini zenye mlengo wa huyu El kama Judaism, Christianity and Islamic
Na sio Kwamba El alikua ndie Mungu pekee hapana kulikua na Miungu wengi sana ukienda Kwa wahindi Wana Mungu wao Rama mwenye sifa kama za El
Ukienda misri Kuna Ra
Mesopotamia Kuna Anu
Kuna Enki
Na wengine wengi sana wote Wana mapokeo tofauti tofauti ila asili Yao ni Moja na Hao Miungu baadhi Yao walikua na bifu Kali sana mfano
Elohim YHW aliingia mkataba na agano na Abraham Kwamba uzao wake wote Watakua Watu wake na ni Marufuku kujihusisha na miungu mingine lengo lake awe na Watu wa kukamilisha mission zake Kwa urahisi na lengo la huyo Annunak El ni gold na dio maana mmoja wa uzao wa Abraham yaani Suleiman alikua na uwezo mkubwa sana na akili nyingi aliweza kukusanya gold Kwa maelfu ya matani na baadae zikapotea ghafla tu hata hatujui zilienda wapi hao ndio ANNUNAK na mission zao duniani

Nahitimisha ya Kwamba Hizo Hadith za Mungu mkuu muumbaji wa ulimwengu ni uongo na huyo Mungu hayupo na hajawahi kuwepo ila tu Watu waliamua kuwaita accient ANNUNAK miungu ila walikua Alliens tu!
 
Unadha ujumbe wa Mungu ungefika vipi bila kutumia binadamu wenzetu?
Mie niliuliza Kuhusu hawa Manabii na Mitume,
Musa...Elia..Yesu.. Mohammed

Je ni Waongo na Hawakutumwa na Mungu. Ndio ukasema Hapo Juu hao si Washirika ila Ni wafanyakazi. Au nimekuquote Vibaya!?
 
Back
Top Bottom