worms
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 978
- 911
Hili swala la uchoyo wa maarifa lipo sana maofisini na mashuleni hata mitaani pia .Kinachotuponza waafrika wengi ni uchoyo wa maarifa
Most of waafrika ni wabinafsi na wachoyo kupitiliza
Huwezi ukapata knowledge yoyote kutoka kwa muafrika kirahisi hivyo labda uwe mzungu
Yani iko hivi, mtu yuko tayari kufa na ujuzi wake kuliko kumpa muafrika mwenzie maana anajua akimpa atanufaika nao nayeye hataki mtu afanikiwe kupitia yeye.
Lakini muafrika huyohuyo jinsi alivyo bashite wa kiwango cha lami akitembelewa na mzungu atampatia siri zote za ujuzi wake huku akikenuakenua meno na kujiona amewin.
Yani wabongo safari yetu bado sana
Mpaka ikifika stage tumejitambua, tukajikubali na kujithamini kwa jinsi tulivyo bila kuwa na inferiority feeling hapo ndipo tutakapotoka kwenye hili dimbwi la kuwa mkia na kuamini kwamba nikimsaidia mwenzangu akafanikiwa kunizidi mimi its okay
Huwa napata maarifa mengi sana kupitia mitandao kama YouTube n.k na huko watu hujitoa kuelekeza vitu mbalimbali na bure compared na wabongo haupati somo lolote mitandaoni.