Aisee. There is so much wrong with these statements sijui hata nianzie wapi.
1. Utumwa. Slavery.
Nchi kama marekani haijajijenga yenyewe, watu weusi watumwa walienda wakawajengea nyumba zao, wakawajengea reli ili treni zipite, wakawafanyia kazi bure kwenye mashamba yao, wakawanzishia viwanda vyote ambavyo leo vimewarahisishi hadi kufika kua wengi wao ndio matajiri namba moja duniani, wakapata mda, kama watumwa wanakuletea chakula, wewe unakaa nyuma unakula na kuweza kujijenga na mambo mengine.
Akili za binadamu zinaendelea ku develop as we go, tunahitaji A ili tufike B, cheki mfano windows 98 zilivyokua na cheki windows 10, akili za waliotengeneza hazikuweza kufikiria muonekano wa windows 10, hadi baada ya kupitia window 98-xp-vista-7-8 kisha ndo ten, huu ni mfano mdogo, everything is gradually done, kitu kimoja baada ya kingine, so mfano wa hapo ni kwamba windows ya kwanza kabisa ndo ilikua A kisha zote zinazofuata ni B,C,D,E.. so inabidi kupitia zote hizo ili kufika F au Z, so ninachojaribu kusema, kwenye chochote kama tulikua A wote, wenyewe wakataka nguvu zaidi, kwahiyo wakapata watumwa na kulazimisha kuwasaidia wao wafike B na C na D haraka kabla ya kila mtu, ofcourse watakua wamefika G kabla yetu, sijui kama bado inaeleweka, anyway.
2. Capitalism is the white mans System.
Tunadanganywa kila siku ohh ukifanya kazi kwa bidii utakuja kumfikia hata bill gates, au kua kama mark zuckerberg, lakini hamna kitu kama hiko,tukiendelea kucheza mchezo wao labda mmoja au wawili watawafikia lakini wengi itakua wao tu. Huu ni mchezo wao, wakipata hela wanagawana wenyewe kwa wenyewe, hata hapahapa Tanzania, kuna wataliii wanakuja kutembelea Tanzania, wanakaa kwenye ma lodge ambayo sitanii... wanalipa hadi milioni 14 na zaidi kwa siku 5-7, hizo lodge pia wenye nazo ni za watu weupe, so hela zinabaki kwao.
Hela zinaendeshwa na benki kuu, ndio maana hatuwezi sema tu hela yetu ina thamani kiasi flani, inabidi
kutokana na stocks kwenye market na mambo mengine mengine ndio inapanga value, so basically hzi noti ambazo tunazo hapa benki kuu wanajua zipo ngapi zinazunguka, kwahiyo kama hela zipo elfu kumi, na elf saba zinazunguka kwa watu weupe tu, hizo elfu tatu mnagawana wote wengine, there is no chance for anyone to get anywhere other than the white man. Najua na over simplify, lakini kusema watu weusi wameachwa nyuma kwenye system za watu weupe is also over simplifying mambo mengi sanaa.
3.Akili za utumwa. Slavery mentality.
Tumepata uhuru kwenye makaratasi, lakini kiakili bado.
Wengi hawato lisikia hili, lakini kuanzia dini zetu, tunavyoendesha nchi kiserikali, tunavyofundisha watu madarasani vyote vimeletwa na wakoloni, na bado hadi leo tunavitumia, kabla ya utumwa tulikua tuna imani zetu na njia zetu jinsi gani tunakuza watoto na kuwafundisha, tulikua na utawala wetu, lakini wakaona kua wa Afrika ni watu wachini wasiojielewa na kuja kututawala, hata hii mipaka tunayoiheshimu na kupigania waliichora wao, kwa kua wanagawana vipande vya bara hili.
So jiulize kila siku, ni nini unachokubaliana ambacho sio cha kweli ni kuambiwa tu na mtu mweupe kua hivi ndivyo inavyobidi iwe? Kama kulazimisha watoto weusi kunyoa nywele zisikue mashuleni kwetu, ni kwamba wa Afrika tulionekana ni wachafu na hatuna thamani, ndio maana tunaamini hadi leo nywele nyeusi zikikua inabidi zinyolewe kila mda.
Anyway. Someni vitabu.
Sikiliza watu wanaoongea.
Soma historia vizuri, tupendane wote, tufanye kazi pamoja.
Watu weusi tuna ujasiri ambao wenyewe hawatoweza pata kamwe, ukitoa hizi system zao.
Angalieni nini kinaendelea na wamarekani weusi, wasikilizeni walichopitia na kwanini wengi wao ni wafungwa na hawana nafasi nyingi, wao wanajaribu sana kupigana na hizi system, sisi tunabaki nyuma.
Mafanikio kwa wote yapo, ila sio burebure.