Baadhi ya matatizo dunia hii kama vita na magonjwa yame na yana na yataendelea kusababishwa na hawa unaofikiria kama sio wao dunia ingekuwaje.
Mfano wanaweza kumtengeneza bacteri na kisha kumtafutia dawa baada ya hapo akaamua kuwaambukiza binadamu bacteria hao na kusha akazalisha dawa kwa wingi na kufanya biashara kubwa kabisa.
Mzungu huyo huyo anaweza kutengeneza bunduki kasha akatafuta watu wanaoongozwa na kuamua kwa jazba, akawagonganisha vichwa kisha akafanya biashara ya silaha kwa pande zote mbili. Vipi kama wasingekuwepo wagunduzi hao bunduki na bacteria wangeishi maisha gani?
Kuna jamii za kiafrika na baadhi ya mataifa mfano India kuna watu huishi porini tu na mjini hawapajui, sio hospitali wala shule, hawajui nguo wala chochote cha kitechnolojia lakini wanazaliana na kukua kuzeeka na kufa kwa kutegemea vyakula na dawa za porini, hawa wanasaidikaje na dawa, MRI au CT SCAN unazoziona ndio mwokozi wa maisha yako?