NITATOA USHUHUDA
JF-Expert Member
- Jul 6, 2017
- 757
- 728
tofauti yetu ni moja tu,mzungu anajua thamani ya muda
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HahahahaaaKama watu wanakimbizana na wanyoa viduku mpaka mwaka 2018, utapata wapi muda wa kugundua hata chanjo ya pepopunda?
[emoji101] [emoji101] [emoji106]Baadhi ya matatizo dunia hii kama vita na magonjwa yame na yana na yataendelea kusababishwa na hawa unaofikiria kama sio wao dunia ingekuwaje.
Mfano wanaweza kumtengeneza bacteri na kisha kumtafutia dawa baada ya hapo akaamua kuwaambukiza binadamu bacteria hao na kusha akazalisha dawa kwa wingi na kufanya biashara kubwa kabisa.
Mzungu huyo huyo anaweza kutengeneza bunduki kasha akatafuta watu wanaoongozwa na kuamua kwa jazba, akawagonganisha vichwa kisha akafanya biashara ya silaha kwa pande zote mbili. Vipi kama wasingekuwepo wagunduzi hao bunduki na bacteria wangeishi maisha gani?
Kuna jamii za kiafrika na baadhi ya mataifa mfano India kuna watu huishi porini tu na mjini hawapajui, sio hospitali wala shule, hawajui nguo wala chochote cha kitechnolojia lakini wanazaliana na kukua kuzeeka na kufa kwa kutegemea vyakula na dawa za porini, hawa wanasaidikaje na dawa, MRI au CT SCAN unazoziona ndio mwokozi wa maisha yako?
Hapahapa bongo tumepata rais bomba ila wenzake wanamchafuwa kila kukicha hii ni laanaBinafsi linapokuja suala la kutumia akili ili kuleta maendelea kibinafsi na kijamii huwa nashindwa kuelewa. Kwanini wazungu na sisi watu weusi tuna utofauti sana ktk global development contribution?
Huwa najaribu kufikiria how this life would have been possible kama Mungu asingeumba watu hao weupe??
Sina lengo la kuwasifia lakini najiuliza wao wamewezaje kugundua vitu tunavyoviona leo vikisaidia sana watu lakini kwa upande wetu sisi watu weusi hatujaonesha ugunduzi wowote wa kushtua dunia??
Hebu fikiria mfano teknolojia ya afya jinsi wazungu walivyoweza kugundua madawa mbalimbali ambayo mimi kama mmoja wa wanafunzi wa kozi hii huwa najiuliza hivi hawa watu walijuaje kugundua haya??
Madawa ya bacteria, fungi, protozoa na vaccinations mbalimbali za viruses hivi wao waliwezaje kugundua haya? Na kipindi wanagundua what we blacks were doing in this World??
Sometimes huwa nahisi labda Mungu aliwaumba wao kwanza halafu sisi baadae maana sioni kitu chochote kipya cha kujivunia kama mwafrika..
Technolojia za disease diagnoses kama X-rays, staining techniques, immunofluorescence, FBP, ELISA, microscope n.k Hivi wao waliwezaje kugundua? Au uwezo wa ugunduzi waliopewa wazungu ni tofauti na wa kwetu??
Ukija upande wa pharmacy utaona dawa ambazo ukizisoma utagundua nguvu kubwa ilitumika sana mpaka kuzigundua lakini kitu cha ajabu sisi weusi hakuna hata kitu tumegundua na hata kama vipo basi ni vichache mnooo!
Kuna maprofesa, madokta na PhD holders wengi tu hapa bongo lakini hakuna hata dawa moja wameweza tengeneza ikawa na brand ya kwetu tatizo liko wapi au ni mimi tu naona haya maendeleo ya watu weupe??
Ukija kuangalia teknolojia ya ujenzi wa majumba huko nako n watu hao hao weupe walio watalaamu wa kubuni mijengo mbalimbali na sisi tunaiga kwao...
Pia wameonesha uimara ktk mambo ya michezo,siasa imara,elimu za kiwango cha ajabu,n.k....sisi n miaka 50+ya Uhuru Ila hata handkerchief tunaagiza China HV where is the problem?? I ask myself the following questions..
1.Kama Mungu katuumba sawa,mbona hawa wao wameoneshwa kuwa na uwezo mkubwa kulko sisi?
2.Kama kila kitu chetu tunaiga kwa wazungu yaan utakuta kila kitu unachomilik hapo ulipo kimetengenezwa mbele ,so inamaanisha ili tuendelee lazma tujifunze kwao,je,wao wamejifunza wapi??
Kuna maneno Donald trump alitutukana waafrika lkn mm nikiyaangalia naona kama ni ukweli mtupu kabisa....anasema tumekalia Almas,dhahabu na aina zote za madini lkn bado sisi n maskini na tunaishia kugombana na kuuana sisi kwa sisi kisa Mali asilia hii,tatzo liko wapi wakubwa zangu..mm ndio naanza kukua na kuona Africa jinsi ilivyo..najiuliza kama hawa walionitangulia hawajaweza kutengeneza chochote kile hii inamaanisha sisi ni wa kuzaliwa,kukua,kuoa/kuolewa,kuzaa na kufa tu au??
Au sisi ni zao LA laana (mtanisamehe hapa) maana hamna mchango naoona uliotokana na waafrika ktk kuhakikisha a world is at good form and peace...civil wars,hunger and starvation,poverty,poor hygiene,poor housing,poor infrastructure, political intolerance, diseases,and all forms of bad issues are within us brothers and sisters!!!! Where have we messed??
I conclude kwa Leo kwa kusema HV:A world peace can be maintained without blacks in presence but the world can't run without whites??? Why???
Mkuu usiumize kichwa, ukwel ni kuwa mtu mweusi yeye anawaza KULA, KUSEX na STAREHE za KIJINGA basi. Hata ww hapo jiangalie vzur utaona mda mwing unautumia kuwaza utakula nn na utampata dem sangap.. Tunapoteza mda mwmg kweny mambo yasiyo ya msing (vchwa vyetu havifikiri vyema)Sasa n kwann cc tunashindwa hata kukopi?? Miaka 57 ya Uhuru now??
Tatzo liko wapi??
Ubongo mdogo au tumerelax sana
KAMA SISI WAAFRIKA TUNA AKILI NYNGI MBONA HATUKWENDA ULAYA KUWATAWALA WAZUNGU?Mkuu umeibua hoja nzuri sana. Nataka nikufahamishe tu kuwa kama tukitazama kwa hoja yako hiyo ya Upendeleo basi Mungu alitupendelea maarifa sisi waafrika ila tu hatuna juhudi hasa kizazo hiki cha sasahivi.
Mwandishi Walter Roodney aliwahi kuandika kitabu cha HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA. Katika kitabu hiko ameelezea namna gani Afrika ilikua na maendeleo zaidi ya wazungu.
Ukisema kwamba waafrika hatuna maarifa ya kugundua kitu unakua unakosea sana. Kwanza tambua kwamba uhusiano wa Mzungu na mwafrika ulianza mnamo karne ya 15. Hapo tunazungumzia miaka ya 1400.
Wazungu walipokuja Afrika kwa mara ya kwanza, walikuta tayari tumeendelea kuzidi wao wenyewe kiasi kwamba wakaiga sehemu kubwa ya teknolojia yetu na kwenda kuziendeleza kwao. Najua utabisha katika hili, lakini nitakudhibitishia kwa nadharia za kihistoria na kisayansi kupitia nyanja zifuatazo.
ELIMU
(Hesabu na maandishi)
Hesabu nyingi unazoziona hivi leo zilianzia MISRI (Egypt). Njia hii tunayotumia leo kuhesabu ilianza zaidi ya miaka 35000 iliyopita kutoka Africa. Wamisri walianza kuandika vitabu kuhusu hesabu za kugawanya kuzidisha, hesabu za sehemu na Geometry.
Mfumo wa kuandika herufi tunazozitumia leo, ulianza Misri pia mnamo miaka ya 3100 KB (Kabla ya kristo).
Kalenda inayoipa dunia siku 365 na robo , ilitengenezwa na wamisri. Kugwanywa kwa masaa 24 kwa siku kulianza misri zamani sana na enzi hizo walitumia misimu hasa ya maji kutambua masaa.
DAWA
Katika hoja yako umesema kwamba wazungu wamegundua dawa. Sio kweli!! kuna tofauti kati ya kugundua na kuendeleza. (invent and develop)
Dawa zinazotumiwa leo ziligunduliwa Africa zamani sana huko Misri, Nigeria na Afrika kusini enzi hizo kabla nchi hizo hazijapewa hayo majina. Walitumia mizizi na mimea kutibu magonjwa mbalimbali. kwamfano Salicylic acid kwaajili ya kupunguza maumivu ambayo leo hii wazungu wameindeleza tunaitambua kama Aspirin. Kaolin Acid kwaajili ya ugonjwa wa kuhara ambayo leo hii dawa inaitwa Kaopectate. Utafiti umeendelea kueleza kua, waafrika walikua na uwezo wa kufanya upasuaji (under antiseptic conditions) wakati huo ujuzi huo ndo ulikua unaanza kuibuka barani ulaya.
ENGINEERING
Moja ya kidhibiti hai cha utafiti kwamba Africa ilikua na maengineer na maachitecture wake hata kabla ya wazungu ni Pyramid of Giza (Cairo) ambayo ipo kwenye maajabu saba ya dunia. Utafiti unaonyesha Pyramid hyo ilijegwa mnamo Miaka ya 2580 KB (Kabla ya kristo) kipindi ambacho hta mzungu hakuwa na jengo lolote la ajabu kama hilo. Kinachofanya pyramid hii iwe ya ajabu ni ufundi uliotumika.
Waliosimamisha pyramid ile walibeba tani milioni sita na nusu za mawe ambapo kila jiwe lilikuwa na tani zisizopungua 9. Kwa kipindi hiko ambapo hakukua na mawinch wala minyororo wala cement waliwezaje kupandisha haya mawe? Ni wazi kabisa mwafrika alikua na teknolojia ya kipekee kabla ya mzungu.
Nina mifano mingi natamani kukushirikisha ila kwa leo naishia hapo. Waafrika tuna akili na kama ni upendeleo basi Mungu alitupendelea sisi. Ila tu waafrika sisi ni wavivu kujituma na kufikiri. Mzungu hana akili kama tunavyodhani, ila tu kapewa juhudi na kiu ya kujifunza. Sisi tumelala sana na kwa mantiki hiyo Mzungu anaokana ana akili kuliko sisi.
ASANTENI!!
Na wapo waliotengeneza bunduki wakafungwa badala ya kuendelezwa . Sheria za kikoloni zilizokuwa zinatukwamisha zinakumbatia.Hapana hutatui tatizo kwa fikra zako zilivyo unaangalia tulipoangukia huangalii tulipo jikwaa tunaweza hata sasa ipo mifano hai ya wahandisi wetu km yule bwana zanzibar katengeneza helkopta kakatazwa kulusha yupo wa makambako katengeneza umeme kazuiwa kuusambaza unaweza kuona tungewakamata mkuu
Upo dunia gani boss?Mwarabu, muhindi, mchina nao wamegundua nn?
Sasa hapo ndipo nasema bhc cc akili zety n ndogo sana maana kama tungekuwa na akili vzur tusingekubali kuharibiwa mambo yetu mazur na kukubali yaliyo mabaya so it seems wazungu walituzid maarifaWe na kusoma kote lkn kichwani kwako hakuna kila kitu
Je unajua jamii za watu weusi na aztecs ziliokua zimestaarabika kabla ya ujio wa wazungu na wazungu wamefundishwa ustaarabu na weusi
Wazungu wameua na kuharibu mifumo na elimu zetu ambazo zilikua bora kuliko unayoipata
Je unajua hata elimu ya madawa unsyoisomea ndo chanzo kikubwa cha vifo na uharibifu wa kinga ya mwili kuliko dawa zetu za asili
Wazungu wametu beain wash mpaka huu mfumo wa maendeleo unaouona saivi tunaona unafaa wametuteka kisaikolojia
Stay woke brother think again unachokisifia kina kufaa kweli
Sio yote ndg ...yapo ambayo yametengenezwa sikatai ila n machacheBrother unajua biotechnology mkuu
Plus conspiracy
Then dig deep utakutana organisation kama CDC na Itneligent agencies in likage to economic and power
We umekosha.....n kweli kwa Mungu tuko sawa ila hoja ilkuwa kwann wengne wako juu sana kulko ccHatuwezi tukawa na akili sawa.
matabaka na madaraja yapo kila mahali.
Yote hayo ya hapa hapa duniani.
Kwa mungu haangalii mwenye akili nyingi.Bali
MWENYE MATENDO MEMA.
Duuuh....kaz IPO kweli ....mambo yameharibika mudaSio kweli mtoa uzi inabidi uzame zaidi na utagundua zaidi kwa mfano
1. Miji ya Mali, Gao, Cairo na Timbuktu ilikuwa mpaka na Universities zao
2.Kulikuwa na wagunduzi kama Abu Hazen, Algebra ambao gunduzi zao kwa kiasi kikubwa zimefanikisha gunduzi kubwa za sasa Ulaya
3. Kulikuwa na Viongozi na wafanyabiashara mahiri kuliko hata hawa wa dunia ya sasa ambao tunahisi tumeendelea zaidi
Kwa mfano mtu kama Sundiata Keita mpaka leo hii chukua top 100 billionaires kusanya mali zao hawamfikii Keita
4.Wizi, uporaji na ukoloni
Kikubwa tulichoibiwa ni KUJIAMINI hiki kitu kimetugharimu sana na kitaendelea kutugharimu
Hebu jiulize miaka 50 ya kujitawala bado tunahitaji kiingereza kuwa lugha. Ya kufundishia mashuleni ?
Hivi bado tunahitaji taratibu zetu za kimahakama ziendeshwe kwa kiingereza ?
Hivi kama umesoma historia kuanzi darasa la 4 hadi form 6 wapi umesikia mwalimu wa history ametoa changamoto kama hii aliyoileta mtoa made
Hivi wachumi/ watawala wetu wameandika/ wamejifunza nini toka kwa mtu kama Gaddafi, Lumumba au hata Karume ?
Wakatabahu