Yaonyesha umeandika kwa hisia kali sana ndugu.
Ni kweli kuna tofauti kubwa kati ya Wazungu/Wanateknolojia na Weusi/Wana silia, ila pia ukumbuke kujiuliza hivi ni vyote wafanyavyo Wazungu/Wanateknolojia Dunia inavihitaji? tofautisha mahitaji ya Wazungu/teknoloji na mahitaji ya Dunia/ardhi/uhai.
Sehemu kubwa ya gunduzi zao ndio zime/zinazalisha sumu yote inayoiangamiza Dunia leo, bila hizo teknolojia tusingekuwa na haya mabadiliko tabia nchi, miti inakatwa ili ikazalishe fanicha viwandani, bahari inachafuliwa na viumbe wanaangamia huko.n.k.
Bila hizo gunduzi tunazoita maendeleo, nadhani binadamu angeishi maishi ya asili tu ambayo ndio haswa ilikuwa kusudi la Muumba wa Ulimwengu na mahitaji ya dunia hai.
Kama unakubaliana nami kuwa Dunia kwa sasa ipo taabani, mito inakauka, joto linaongezeka, magonjwa yasiyotiba kuongezeka n.k basi ukubaliane nami pia kuwa Dunia ingekuwa salama sana bila uwepo wa Mzungu/Mwanateknolojia.
Unapofurahia uwepo wa Gari, Ndege, Meli, fridge, AC n.k pia ujue haya maangamizo ya uhai wa dunia yanatoka huko.
Sasa hapo sio kazi yangu tena kujiuliza ni kwa nini Mungu alimleta Mzungu/Mwanateknolojia, ila kuna kila dalili kuwa Mzungu/Mwanateknolojia alikuja baadae, na dunia ilikua salama kwa muda wote kabla ya uwepo wa Wanateknolojia hao.
Kuhusu tiba, ugunduzi wa madawa n.k, nadhani kuna mengi sana hatuyajui kuhusu Dunia tangu zama na zama, hivyo bado ni ngumu kujiridhisha kama tuliishi tu bila namna yoyote ya kujitibia kabla ujio wa Wanateknojia, basi ndio kusema bila teknolojia hii race ingeangamia? nitakuwa wa mwisho kuamini hivyo, sehemu kubwa ya magonjwa yanayohitaji hizo tiba za hali ya juu nayo huzalishwa na uwepo wa hizo hizo teknolojia, mfano saratani mbalimbali n.k. Mimi naamini tiba zote huweza kupatikana kwenye mimea tukitumia zetu vizuri.
Tukiongelea ujenzi n.k, kuna ujenzi wa enzi hizo ulifanyika bila teknolojia iliyopo leo, mfano ni zile Piramidi za Misri, kwa hiyo sioni kama Binaadamu tulihitaji sana teknolojia ya sasa ndio tufanye shughuli zetu.
Hizo almasi na dhahabu unazozitaja hazina uhusiano wowote na uwepo/uhai wa dunia, ni Wazungu/Wanateknolojia hao hao ndio wanaozihitaji na kutufanya tuchimbue ardhi yetu kama wehu, hata tukiziacha huko ardhini hakuna tunachopoteza.
Kuhitimisha maelezo yangu ni kuwa, Mzungu/teknolojia ni artificial na Mweusi ni asilia, hivyo kaa chini ujiulize Dunia inahitaji asili au artificial?