Je, Mungu kaumba baadhi ya wanadamu kwa upendeleo wa akili na maarifa?

Hili swala la uchoyo wa maarifa lipo sana maofisini na mashuleni hata mitaani pia .

Huwa napata maarifa mengi sana kupitia mitandao kama YouTube n.k na huko watu hujitoa kuelekeza vitu mbalimbali na bure compared na wabongo haupati somo lolote mitandaoni.
 
Uwezo wa kifikra inaendana na spirits/rituals za jamii husika.Mimi kwa kutazama tu na changamoto chache nilizopitia nilibaini kuwa jinsi tunavyoishi sisi watanzania hatuwezi fanya kitu kikubwa mfano angalia mtaani kwenu kuanzia wazazi wananaedesha maisha yao vipi? Shule ya msingi watoto wa mtaa wenu,vijana wa mtaa wenu? Je mawazo yao yapo vipi? Starehe Ulaya ndio kwao lakini bado watu wanafanya mambo makubwa sisi ata kilimo nenda kijijini ukutane na washirikina! na wazee wasio na Upeo wakiwaathiri vijana wao utasikitika!..
 
Ndugu unafikiri ni uchoyo wa maarifa..hicho unachokisema mimi napenda kuanzia sasa watu wakifahamu kama kukosa Ufahamu!.. kuna kitu kukariri hicho kimeathiri sana jamii zetu!.. Mtu akikariri ana faida juu ya atachoulizwa tu!..kuhusu wabongo kutokuweka mambo mtandaoni ni ishara kuwa ata wale wabongo wanaotufundisha asilimia kubwa wamekariri..Mara ngapi wanashindwa kuja na ubunifu..hadi leo mtihani mgumu unaaminika kuwa ndio kipimo cha uelewa hivyo basi atakaekuwa amekariri kuliko mwenzake ndio atafaulu mtihani! pia kuna changamoto ya uvivu wa kujifunza vitu vipya!
 
Ngoja nikupe mfano! Kuna Siku nilienda kijijini nikakuta kuna magogo flani wanatengeneza kama pembe tatu kwa ajili ya kubebea plau(Jembe la kukokota na ngo'mbe) nikawauliza wazee kwa vijana inakuwaje wanatumia zana kama hiyo tangu enzi na enzi na inaleta mmomonyoko wa ardhi na kuleta makorongo, kwa nini hawafikirii kuweka matairi? majibu waliyonipa niliona yahitajika zaidi ya karne hicho kizazi kitoweke kabisa ndio maarifa yaje! hadi tunajadili hili ni watu wachache watajitokeza kuchangia!..wabongo hatutaki kuchoma kichwa,tunapenda mada za kelele kelele.. mtu akishapata sehemu ya mkate imetoka hiyo!
 
Mfano mwingine Mi nakaa karibu na Airport Jana umeme ulikatika mtaani na Uwanja wa Taifa kukiwa na mechi mchuanao wa CAF, wakati huko Airport umeme unawaka na ndege zinatua! Tujiulize tu! kwa nini Airport na sio kwingine utabaini udhaifu wetu! lakini watakuja watu kutetea ujinga badala ya kuomba radhi nakufanya mageuzi!
 
Hakuna haja ya kumlaumu Mwenyezi Mungu.Hakuna taifa lolote duniani lililoendelea bila ya kuwekeza KIKAMILIFU kwenye ELIMU.Ni kuwekeza KIKAMILIFU na si KIMZAHA na KUJARIBUJARIBU.Kosa kubwa mno kucheza na elimu.Kama nchi haitengenezi 'SKELETON' ya elimu iliyo madhubuti;yenye kuzalisha wataalamu wabunifu na si wasaka cheti, skeleton hiyo ikatekelezwa kiuadilifu na commitment ya hali ya juu na uzalendo usiotia shaka,nchi ikimbie kwa kasi ya kimbunga.Tusitafute mchawi kama tutacheza na elimu.
 
i think its just our thinking, mi naona wapo sawa tu na sisi hao wazungu maana kuna matajiri na maskini tu kama uku , na wanasoma sawa na sisi tu maana si kuna watu wanaendaga kusoma mambele akianza na raisi nyerere kabisa ila bado nchi ipo pale pale
 
mkuu kanywe soda ya ntalipa maana daa! una akil sana aisee umetoboa pale pale
 
Great poets ndo hao wazungu,
Great novel writers ndo hao wazungu,
Great fiction writers and actors ndo hao wazungu,
Great preachers ndo hao wazungu,
Great philosophers ndo hao wazungu,
Great lawyers & doctors ndo hao wazungu,
Great architect ndo hao wazungu,
Great painters ndo hao wazungu,
Great leaders ndo hao wazungu,
Great bloggers/freelancers ndo hao wazungu,
Great physician and phsycologists ndo hao wazungu,
Great teachers/lecturers/speakers/journalists ndo hao wazungu,

huku kwetu tumekalia majungu na roho mbaya, kwa mifano michache: mtu kasomea philosophy lakini hadi anakufa akiwa mzee hana hata falsafa mpya kuhusu chochote aliyoibaini.

Mtu kasomea literature lakini hadi anazeeka na kufa hajawahi kuandika great novel/poem ambayo mtu akisoma anapata cha kujifunza.

Wasomi wengi wanapambana kuwa malecturers lazimishi na siyo malecturers ongozaji. Watakulazimisha kuelewa walichokariri hawatakuongoza kuelewa.

UDSM na vyuo vingine vimejaa coward elites mtu kasomea economics halafu hadi anakufa hana CV yoyote ya kuanzisha economic venture yoyote, yaani mtu anakufa na CV ndefu ya utumishi wa umma lakini kwenye private life ana zero Cv.

Wazungu wanawaambia wanao: Mwanangu soma ili ujielewe na kuelewe mazingira yako.

Waafrika wanawaambia wanao: mwanangu soma uje uajiriwe na kutajirika.

Hivi kweli Maprof wa hapa Tz watakufundishia mtoto apate akili ya kujiongeza nje ya elimu? Maana wao wenyewe wanaishi kwa huruma za serikali, hapa Tz karibia maprof wote wako controlled in minds.

Controlled minds can't think to discover new things.
 
Hii ni hoja dhaifu mno ya kujifariji. Mpaka unahisi wao wanatengeneza mashua/meli zinazoweza kutoka ulaya mpaka Africa sisi tulikuwa tumetengeneza nn cha ajabu walichoiga? Mpaka wao wanagundua kuwa madini ni mali na kutusainisha mikataba ya kilaghai sisi tulikuwa wapi kugundua hayo yote?
 
Good comment
 
Aliyechangia kwamba kabla ya kuja wazungu tulikua na tekinologia yetu lakini wakatudanganya na kuiharibu, sasa mtu kuja nyumbani na kukudanganya ni akili ya hali ya juu. Ni kwa nini wewe usitumie akili uende kwake?? Wamejaliwa akili na maarifa ya kutosha. Umeshaona formula ya kisayansi ya mwafrika? Tunaishia kukariri za kwao eg Archimedes principle, Newtons law of motion nk Basi tuseme hakuna Mungu kwani hakuna Mungu mwenye upendeleo kiasi hicho. Check the concept of time in Africa
 
Hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…