Je! Mungu ni yule yule?

mkuu,endelea kulala!
 
Kiranga bana! Umeelewa nilichoandika lakini? Ukiambiwa una macho lakini huoni utahisi umetukanwa?
Hawa watu ishasemwa wameamua tu wenyewe kutoamini, yaani wameamua tu kwa kiburi chao. Na si kwamba wana hitaji la kutafiti wakabaniwa.
Sasa kuniuliza kwanini wafungwe sijui blah blah nashindwa kukuelewaa.
 
Si ndio washirika wenu? Sishangai.. Hapa unazuga tu..
Wanachoamini Freemasons ni Mungu yupi? Maana hoja si Mungu tu, kuna wengine kwao Jiwe ni Mungu..
Hapa naona jinsi gani udini unakusumbua, uzi huu unazungumzia kuhusu Mungu na wala sio hizo dini ulizoamua kusimamia
 
Utasemaje wameamua tu wenyewe wakati Quran inatuambia mungu kaifanya mioyo yao kuwa migumu wasimjue?

Unataka kusema Quran imedanganya?
 
Hongera sana naona finally umepata hawara sasa[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Jimena nikwambie ukweli tu aisee siwezi kwenda maabara nikakuthibitishia Mungu halafu nika scan matokeo nikakutumia...

We ukihisi homa unaenda kupima je ukihisi upendo unapima wapi...?! Hebu kapime upendo uniscanie matokeo niyaone... nijue upo kiasi gani
 
Bado sijauhisi upendo. Ntakapouhisi ntakuthibitishia kwa namna yake na utaelewa, ingekuwa upendo hauthibitishiki watu wasingekuwa wanaoana

Sasa acha kuzunguka ovyo lete ushahidi wa huyo Mungu wako kisha tuendelee
 
Hebu na wewe tuthibitishie kuwa Mungu hayupo.
 
Hebu na wewe tuthibitishie kuwa Mungu hayupo.
Kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo.

Kwa sababu hakipo. Ili kuthibitisha, inabidi kitu kuwepo.

Kuthibitisha ni uwanja wa vilivyopo. Ndiyo maana Polisi wakipata warrant ya kesi ya maadawa ya kuelvya, hawamwambii mtuhumiwa "thibitisha nyumba yako haina maadawa ya kuelvya". Wanayatafuta mpaka wayapate wao. Kwa maana kama nyumba haina maadawa ya kuelvya, mwenye nyumba hawezi kuthibitisha hilo.

Hivyo, swali linageuka kwa wanaosema mungu yupo.

Tuthibitishieni kwamba mungu yupo.
 
Ndio maana nakwambia acha kuokoteza stori za vijiweni na kuja kubisha bisha hapa, kwanaza freemason ni order members ni waumini wa dini mbalimbali...

Hao wanawake uliowaleta unaweza ukakuta ni wa order ya Eastern Star...
 
Hebu na wewe tuthibitishie kuwa Mungu hayupo.
Hizo mnazoita vitabu vya Mungu ndo zenye uthibitisho wa kutosha.
Mungu huyo huyo tunaeambiwa ndo kaumba kila kitu (ikiwemo dhambi) na ni huyo huyo anaandaa moto achome watu ambao alikuwa na uwezo wa kuwafanya wasitende dhambi ila akaawaacha tu

Huyu Mungu hayupo wala hajawahi kuwepo bali zile ni hadithi tu ambazo yataka ujitoe fahamu kuziamini
 
Bado sijauhisi upendo. Ntakapouhisi ntakuthibitishia kwa namna yake na utaelewa, ingekuwa upendo hauthibitishiki watu wasingekuwa wanaoana

Sasa acha kuzunguka ovyo lete ushahidi wa huyo Mungu wako kisha tuendelee
Unathibitishikaje...?! Sina vipimo vya kupima Mungu nikakuscania ili uone...

Ona sasa mimi nakwambia upendo wewe unawaza ngono, hivi upendo huwa ni kwa jinsia tofauti halafu ni kwa mtu mmoja tu...?! Yaani mke na mme...
 
We usinilishe maneno ambayo sikutamka. Bado sijawaza ngono kabisa,
We ulitaka uthibitisho wa upendo nimekupa sasa hayo maswala ya jinsia yakusanye yote yaweke kwa Mungu wako, jiulize maswali kisha ujijibu ila ukishapata uthibitisho ndo uje kubishana, kama huna logic kwanini unabisha???
 
Kiranga said:
Kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo.
That's stolen concept logical fallacy

Utajuaje kuwa hakipo kabla haujathibitisha kuwa hakipo?

Kitu kisichopo hakithibitishiki,umejuaje kuwa hakipo kabla haujathibitisha?

Kwa sababu hakipo. Ili kuthibitisha, inabidi kitu kuwepo.
Umejuaje kuwa hakipo kabla haujathibitisha?

Au ume-assume tu out of blue?

Jibu maswali yangu hapo juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…