Je! Mungu ni yule yule?

Ndugu yangu unashindana na akili za kupandikizwa..hatokuelewa
 
Usikose kumtambulisha kwa wifi yake hapa... Ama kweli mguu wa kutoka mtume kauombea
Aisee hii familia naionea huruma ,kaka mtu anaamini Mungu yupo ,dada mtu anaamini Mungu hayupo na wifi yake anaamini Mungu wa uislamu ndio wa maana kuliko wa ukristo ,sasa hao watoto sijui wataamini nini
 
Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao dhambi inawezekana kuwepo wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani kuwepo?

Mkuu..Mungu alipomuumba bin Adam alimshirikisha baadhi ya vitu ambavyo viumbe vingine hakuvipa..na hivyo vitu ndo vinavyotutofautisha na viumbe vingine mfano akili na utashi.....kwa kutumia hizi nyenzo Mungu alidhamiria kabisa kutufanya tuweze kuovercome dhambi na matokeo yake tuishi maisha ya furaha....angeweza kutuumba kama wanyama wengine ambao wanaongozwa na Instincts lkn nafikir tusingekua kama tulivyosasa
 
Nimeuliza kabla mungu hajamuumba mtu.

Alipokuwa anafanya kuumba ulimwengu.

Alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kufanyika.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo?

Na kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote avipendelee viumbe vyake vingine na kuvibania vingine?

Kwa nini asivipe uwezo mkubwa vyote katika ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
 
Aisee hii familia naionea huruma ,kaka mtu anaamini Mungu yupo ,dada mtu anaamini Mungu hayupo na wifi yake anaamini Mungu wa uislamu ndio wa maana kuliko wa ukristo ,sasa hao watoto sijui wataamini nini
Watoto watakuwa huru kujifunza vyote kisha wakikua wataamua wenyewe tu.....
Au unaonaje hapo? Hawa watoto hawatakuwa brain washed
 
Watoto watakuwa huru kujifunza vyote kisha wakikua wataamua wenyewe tu.....
Au unaonaje hapo? Hawa watoto hawatakuwa brain washed
Teh kujifunza vyote ni bora tu wasijifunze kabisa maana tunaweza wafanya vichaa ,Wakiwa kwangu Mungu yupo ,wakienda kwa dada mtu Mungu hayupo ,wakirudi kwa mama yao Mungu wake ndio Mungu wa kweli ,inabidi tutafute utaratibu mwingine nje ya imani hizo tatu ,sasa sijui ni imani ipi
 
Hapana hatuwaambii hivyo. Tunawaambia hivi wakristo wanaamini Mungu yupo kutokana na a,b na c, pia waislamu nao wanaamini haya kuhusiana na Mungu huyo huyo, halafu pia kutokana na 1,2 na 3 watu wengine wanajua ya kwamba Mungu hayupo, lakini kwa pamoja tutawafundisha upendo. Na watakuwa bora kabisa na wakikua na watakaposoma zaidi watajua kipi wafuate
Sambaza upendo
Love is my religion
 
Teh sawa mama , nimekuelewa
 
Asante sana kwa kunielewa.
Basi kwa pamoja tusambaze upendo
Amri yangu kuu ni kumpenda jirani yangu kama nafsi yangu japo muda mwingine nashindwa kutokana na mapungufu ya kibinadamu japo najitahidi mara nyingi nisitoke kwenye huo msingi ,Mimi hata sisimizi nampenda japo hawajui kama Mungu yupo au hayupo
 
Upendo hauchagui wala haubagui.
 
Nakuona mbumbumbu wa mwisho kwenye hii mada
 
Kwahiyo mungu wenu nae ana mtengenezaji wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…