Kay unaishiaga tu kunicheka na wakati wa msaada sikuoni ,haha
Hahahaha uncleben kwanza nilikuwa nataka ni-suggest kukusaidia ku-adopt hao watoto utakaozaa na huyo kimada wako ili kuwaondoa kwenye hiyo familia yenye mkanyanyiko hivyo, ila sister wako aka-suggest mtawatunza wenyewe kwa kuwapa elimu ahera kutoka pande zote...teh teh teh watakuwa busy sana watoto wa watu...
Kuhusu kukusaidia kwenye huu mjadala kuhusu uwepo wa Mungu, niseme tu ukweli bado sija-master jinsi ya ku-articulate argument ya uwepo wa Mungu.
Ndio ninaamini Mungu yupo.
Nilimsoma mwanasayansi mmoja alisema anaamini Mungu anaji-reveal kwetu wakati tunapo-gain knowledge na uelewa wa huu ulimwengu na vitu vilivyopo na mambo yake. Niseme tu nami pia naamini hivyo. Yani kwamba, Unapo-gain knowledge na uelewa wa jambo fulani, manake ni kwamba Mungu ameji-reveal kwako. Kwa hiyo kila binadamu ana kiwango chake ambacho Mungu ameji-reveal kwake, na hii processes ni kidogo kidogo na ni on going...
Tatizo linakuja pale binadamu anapo-gain hiyo knowlege na kutotaka ku appreciate na kumu-aknowledge Mungu kwamba ndio nguvu iliyo behind hiyo specific knowlege na matokeo yake huyo mtu anashindwa kui-respect ile knowledge aliyo nayo, na ndio hapo Mungu anapogota kuji-reveal, kwasababu kwa binadamu kama huyo, hiyo knowledge itakwenda kutumika kinyume na ilivyokusudiwa... Kwa hiyo naamini Mungu yupo na anaji-reveal kwetu kwa kiasi tunavyotumia utashi wetu kutambua na kuelewa huu ulimwengu na mambo yake, na pale tunapo respect huo uelewa tulioupata ni kwamba tume m-respect Mungu naye anazidi kutupa uelewa zaidi i.e. anazidi kuji-reveal kwetu zaidi....
Tuchukue ule mfano ulioutoa hapo nyuma, mtu anakuwa na uwezo wa kutambua na kuelewa kuwa mziki hauna rangi na kwamba duara halina harufu... lakini katika quest ya kumtambua Mungu kwa articulation yangu, shida inakuja pale anaposhindwa kuwa na uwezo wa ku-apreciate "in awe" hiyo 'wonder and complexity' ya uwezo wake wa kuona+kutambua, na kunusa+kutambua, kwamba umetokana na Mungu/nguvu ambayo ipo juu yake... anachofanya ni anaikana hiyo nguvu/Mungu, kwamba haipo na wakati imeshaanza kuji-reveal kwake, kwasabau tu anataka aipangie perfection kwa standard zake yeye mwenyewe alizojiwekea kama binadamu za mema na mabaya...anajisahau kwamba bado yuko kwenye quest ya kuitambua hiyo nguvu kwa hiyo kuanza kui-criticise kwamba kwanini imeruhusu zuri hili au baya hili, haisaidii kwasababu bado yupo kwenye journey ya kuitambua, na kama atafanikiwa kufika mwisho wa hiyo safari basi labda atapata majibu ya maswali yake yote na nafikiri anaweza hata akawa amekuwa na uwezo sawa na hiyo nguvu/Mungu...teh teh teh...au hata kujikuta yeye ndie Mungu.
Uncleben, hivi kwenye vitabu vitakatifu si imeandikwa kwamba uwezo wa kujua mema na mabaya alikuwa anabaki nao Mungu tu? Sisi tulikuwa tunatakiwa tupete tu kimaisha, hatukuhitaji kujua mema wala mabaya, ilikuwa sio kazi yetu, Mungu mwenyewe ndiye ange deal na issue ya mema na mabaya...
...alafu uncleben, rafiki zako wakija na issue za kuthibitisha mie siiipo...teh teh teh...
Mimi kama mimi, ninapopata uelewa wa jambo fulani, hapo nimejithibitishia Mungu yupo ndio maana kukawa na jambo la kuelewa at first place.