Je! Mungu ni yule yule?

Hujatibitisha kwamba mungu yupo.
 
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

To the contrary.

Huwezi kuthibitishiwa kile ambacho unakijua, kwa sababu unakijua tayari, huhitaji uthibitisho.

Unachohitaji uthibitisho wake ni kile usichokijua.
Kujua kitu na uthibitisho wa hicho kitu kuna husiana vp?
Ina maana kila tunachokijua kipo na ndiyo maana haitaji kuthibitishiwa? Unaanzaje kumthibitishia mtu kitu ambacho hakijui?na ndiyo maana ulikuwa unauliza chanzo cha mungu ambaye unasema hayupo
 
Uhusiano wa kujua kitu na kukithibitisha ni kwamba huwezi kuthibitisha usichokijua.

Utahitaji vipi kuthibitishiwa kwamba wewe ni wewe wakati tayari unajua kwamba wewe ni wewe?

Unamthibitishia mtu kitu ambacho hakijui kwa kuanza kwenye anachokijua.

Nauliza chanzo cha mungu ambaye hayupo in a Socratic dialogue kuonyesha kwamba hayupo. Mpaka sasa hujathibitisha kwamba yupo.

Thibitisha mungu yupo.
 
Kazi kwel hizi dini hizi wanafanya modifications tu itafikia stage watu kwenye za ibada watu waingie na chupi maana Dar joto
 
Kwa hiyo vyote tunavyovijua vipo hivyo haitaji uthibitisho?
 
Yesu uliyemwona anafanana na wale waigizaji akina Brian Decon au yeye yupo tofauti?
Au ulivuta picha kutoka katika zile movies?
 
Nimependa sana hili jibu lako mkuu......
 
Unarudirudia maneno ka santuri ya 1960 ilionasa Sindano.
Huna jipya zaidi ya hili?
Narudia kwa sababu hujathibitisha.

Thibitisha uone kama nitarudia.

Ukweli kwamba hamuwezi kuthibitisha uwepo wa mungu au kutatua matatizo ya logical consistency katika uwepo wa huyo mungu unaonyesha kwamba hayupo.

Mungu huyu ni hadithi tu ya kutungwa na hayupo kiuhalisi.
 
Hapa mada ni ipi? Mbona kiranga umepindisha?
 
Unaweza kuniambia ni kwa nini wenye kusema kuna mungu huitwa waamini mungu?
 
Unaweza kuniambia ni kwa nini wenye kusema kuna mungu huitwa waamini mungu?
Kwa sababu wanaamini.

Unaruhusiwa kuamini chochote, hata kile ambacho si kweli.

Ukianza kusema ni cha kweli tu, umeshaalika maswali na kujiondolea leseni yako ya kuamini bila kuulizwa.
 
Nimepindisha wapi? Kivipi? Kwa nyuzi ngapi?

Umetumia kipimo gani kujua hilo?
Jamaa kauliza MUNGU NI YULE YULE? hajataka uthibitisho wa kuwepo au kutokuwepo.

Yeye hadi kuuliza hivyo tayari ashajua yupo
 
Jamaa kauliza MUNGU NI YULE YULE? hajataka uthibitisho wa kuwepo au kutokuwepo.

Yeye hadi kuuliza hivyo tayari ashajua yupo
Jamaa kauliza nyimbo za Msondo na Sikinde zina rangi ile ile?

Utamjibuje?

Utakubali nyimbo zina rangi au utamwambia nyimbo hazina rangi?
 
Jamaa kauliza nyimbo za Msondo na Sikinde zina rangi ile ile?

Utamjibuje?

Utakubali nyimbo zina rangi au utamwambia nyimbo hazina rangi?
Hahaahahaa hapo bora kuanza mwanzo kabisa.... Kujua yupo au hayupo... Lkn kiranga haunahaja ya ku kompliketisha uwepo wake maana hiyo ni issue ya iman sio siasa wala sayansi
 
Hahaahahaa hapo bora kuanza mwanzo kabisa.... Kujua yupo au hayupo... Lkn kiranga haunahaja ya ku kompliketisha uwepo wake maana hiyo ni issue ya iman sio siasa wala sayansi
Sijakataa kwamba ni imani.

Lakini hata imani, ikishaletwa JF inajadiliwa.

Kama hutaki ijadiliwe usilete JF.

Ndiyo maana huwezi kunikuta nimeanzisha thread kuhusu haya mambo, najibu watu tu walioanzisha thread.
 
Naona mnabishana sana ila inabd mfahamu hv mambo ya mungu hupimwa na iman na sio akl.
Nnachokiona hapa kuna ukdhan Wa vtu viwili kat ya akili na iman
 
Kwa sababu wanaamini.

Unaruhusiwa kuamini chochote, hata kile ambacho si kweli.

Ukianza kusema ni cha kweli tu, umeshaalika maswali na kujiondolea leseni yako ya kuamini bila kuulizwa.
Kwa mujibu wa maelezo ni kwamba kuna kuamini vya kweli na visivyo kwa kweli, nakubaliana na wewe kwa hilo. Sasa naomba mfano japo mmoja wa jambo ambalo watu wanaliamini na ni la kweli.
 
Naona mnabishana sana ila inabd mfahamu hv mambo ya mungu hupimwa na iman na sio akl.
Nnachokiona hapa kuna ukdhan Wa vtu viwili kat ya akili na iman
Imani ni nini na akili ni nini?

Na ukitaka kujua ukweli unatumia imani au akili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…