Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kama kitu hakipo. Unaanzia wapi kuthibitisha kwamba hakipo?Hivi Kiranga amewahi kuthibitisha kwamba Mungu hayupo? Kuna ushahidi aliokuja nao kuthibitisha kwamba Mungu hayupo? Au ni dhana ile ile iliyozoeleka ya kuzunguka mbuyu!
Uthibitisho wa aina gani utakufaa kuonesha kwamba kitu hakipo?
Nikikwambia pembetatu yenye pembe sita ipo, ila wewe huijui na huna akili za kuiona tu (wakati kwa kweli haipo), utanithibitishiaje kwamba haipo?
Aliyeua kwa kisu unaweza kutoa ushahidi wa alama za vidole zake ukasema huyu kaua kwa kisu, kisu kimepatikana eneo la mauaji kina damu, kina alama zake za vidole, jeraha lililoua limetokana na kisu hiki, huyu ambaye alama zake za vidole zipo kwenye kisu hana alibi.Zaidi kuna video imemrekodi akiua. Zaidi, nyumba ina alarm na ikajifunga milango, polisi wakaja wakamkuta muuaji ndani. Jirani walimuona dirishani akiua.
Overwhelming evidence. Huyu kaua.
Sasa kama hakuna aliyeua kwa kisu, utathibitishaje kwamba hakuna aliyeua kwa kisu wakati hakuna maiti, hakuna kisu, hakuna alama za vidole?
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kama alivyoandikwa katika vitabu vya Biblia na Quran, hayupo.
Hayupo kwa sababu, dhana nzima ya kuwepo kwake, inajipinga yenyewe.Contradiction.
Dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe, kwa sababu, kwa upande mmoja, Mungu huyu ni mtakatifu sana kiasi kwamba kibaya chochote hakiwezi kutoka kwake. Kwa maana hiyo, angekuwepo, dunia isingewezekana kuwa na mabaya. Ukisema aliumba dunia isiwe na mabaya ila Shetani ndiye akaleta mabaya, nitakuambia hata huo uwezo wa Shetani kuweza kuleta mabaya ni ubaya ambao Mungu mwenye utakatifu unaosemwa hatakiwi kuwa nao.
Kwa hiyo, utaona kwamba, kuwepo kwa mabaya, na zaidi, kuwezekana kuwepo kwa mabaya katika dunia hii, ni uthibitisho kwamba Mungu huyu hayupo.
Wengine wamejaribu kujibu kwa kusema Mungu kaachia mabaya ila katupa uwezo wa kuchagua mabaya na mazuri. Hili ni jibu lisilo na mantiki. Ukiwa na mtoto wako mchanga ambaye uelewa wake ni mdogo sana, na wewe una uelewa mkubwa sana kujilinganisha naye, unampenda, utampa chupa ya maziwa na pembeni umuwekee chupa ya sumu ili tu aweze kuchagua anachotaka? Hapana. Utahakikisha nyumba nzima haina sumu anayoweza kuifikia. Utampa maziwa tu.
Sasa kama binadamu mwenye uwezo mdogo, upendo mdogo na ujuzi mdogo anakataa kumpa mtoto wake mchanga maziwa na sumu ili mtoto awe na uhuru wa kuchagua, imekuwaje Mungu huyu mnayemsema mwenye uwezo usio na mwisho, ujuzi usio na mwisho na upendo usio na mwisho ameruhusu ulimwengu uwe na mazuri na mabaya ili watu wawe na uhuru wa kuchagua tu?
Watu kama wangeumbwa katika dunia ambayo haiwezekani kuwa na mabaya na mabaya hata hayajulikani, in fact hayapo kabisa hata kidhana, wangekosaje uhuru wa kitu ambacho hakijulikani wala kufikirika wala kuwepo kidhana tu?
Huyu Mungu yupo kweli au hadithi tu?
Kaachia dunia yenye magonjwa, vita, matetemeko, mafuriko, njaa, umasikini, kuteseka etc, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hivyo vyote haviwezekani watu wakaishi raha mustarehe.
Kwa nini?
Sijajibiwa jibu la kueleweka kwenye swali hili.