Je! Mungu ni yule yule?

Nashukuru kwa kukiri kuwepo kwetu duniani kunaweza kuwa kumesababishwa na jambo lingine ambalo hatulijui...... Na hilo jambo ndio Mungu, japo baadhi ya watu wanabisha bila kuwa na maelezo ya msingi .

Vinginevyo embu tumia logic kuelezea binadamu tumefikaje hapa duniani. I know u don't have that explanation.
 

hapana mkuu najifunza hapa...................kwa manufaa ya wote...embu tueleze Zaidi juu ya aina kuu tatu za Imani juu ya Mungu?
 
Unajua unapoandika kwamba jambo ambalo hatulijui ni Mungu unafanya makosa haya.

1. Logical non sequitur - ume conclude kitu bila kuunganisha premise na conclusion. Umeambiwa kuna mji unaitwa Washington DC, ukahitimisha lazima upo Tanzania. Bila kutoa sababu.
2. Umefanya uvivu - hujajishughulisha kuchunguza iliujue sababu,umerahisisha tujibu kwamba sababu ni Mungu.Hii ni sababu moja kubwa watu wanaamini Mungu yupo. Hawataki kufanya uchunguzi kujua sababu za vitu,kitu chochote wasichokielewa ni "kazi ya Mungu' tu.
3. Nishaeleza hapojuu kwamba hata kama sijui jibu sahihi lakuelezea watu tumefikaje hapa duniani, hilo halina maana kwamba nikipewa jibu lisilo sahihi ni lazima nitashindwa kujua hili jibu si sahihi.

Tumeona kwamba unaweza ukawa hujui square root ya 2 ni nini, lakiniukajua kwamba jibu si 10.

Kwa sababu jibu hili lina contradiction inayoonesha jibu ni la uongo.

Naweza kuwa sijui watu tumefikaje hapa duniani, lakini nikajua jibu si Mungu.

Kwa sababu jibu hili lina contradiction inayoonesha jibu ni la uongo.
 
umeona eeehhh ...yaani unaanzaje kutomjua kiranga ..wakati ma genius wakubwa wakubwa wote waliopo humu wanamtambua
Nikiwemo mm pia kama genius huyu jamaa kweny jopo letu la magenius tunamfahamu
 
Hii habari ya kuamini kwamba kitu usichokifahamu kimetokea kwa uwezo wa Mungu,bila hata kukichunguza na kukijua, ndiyo iliwafanya baadhi ya babu zetu kuamini Wazungu ni miungukwa sababu wana gramophone inapiga muziki, au wanaweza kutabiri kupatwa kwa jua.

Kumbe nimambo rahisi tu kuelezeka bila kuhitaji hawa wazungu wawe miungu.
 
Nikiwemo mm pia kama genius huyu jamaa kweny jopo letu la magenius tunamfahamu
karibu genius ..nawewe anza kumwaga nondo ..tuachie lolote lile unalolijua kuhusu uwepo wa Mungu kama yupo kweli au LA !!!?
 
Mkuu naomba tuukutane ana kwa ana nitathibitiha kuwa yupo Mungu wa kweli aliyeumba vyote vilivyomo na ambavyo havimo

Sio muandikaji mzuri mimi
 
Kasome kitabu cha mwanzo utajua kwamba Mungu alituumbia hiyo 'dunia' isiyo na dhambi, isiyo na mateso, isiyo na shida lakini binadamu akatenda dhambi iliyofanya Mungu amuadhibu huyu binadamu ambapo leo anaishi hivi unavyomuona.

Hata hivyo Mungu hakumtupa kiumbe wake, akamleta Yesu Kristo, mwana wake wa pekee ili kila amuaminie apate Uzima milele na katika huo Uzima wa milele ndio tutarudi kwenye raha ya milele ambayo Adam na Eva walitusababishia tuikose

Lakini baada ya Yesu Kristo wa Nazareth kupaa mbinguni kwa namna Mungu Anavyotupenda akatuachia roho mtakatifu ili atuangalie.

Hivyo kusema Mungu hatujali ni kutojua neno la Mungu.
 
hapana mkuu najifunza hapa...................kwa manufaa ya wote...embu tueleze Zaidi juu ya aina kuu tatu za Imani juu ya Mungu?
Kwakweli ni mada ndefu lkini kama una access ya jukwaa la dini kaitafute inaitwa Mungu, Dini na Imani uisome!..
 
Unapoelezea uwepo wa Mungu halafu ukaiquote Biblia tambua Waislamu hawatakuwa upande wako!.. unazani kwanini?, hawaamini katika uwepo wa utatu mtakatifu, hawaamini katika yesu kuwa Mungu na kwa point kama hizo watu kama kina kiranga wanatumia divide-rule kuweza attack point zenu!..
 
wewe nawe umekuja huku ...huku hapakufai mamaa waweza jikuta unaacha kubeba Bible na kuacha kwenda church



Haaaa nayapata vizuri mno mno hayo madude... nilisomaga sijui wapi watu walikua wanatuona kama wehu........ miaka hiyoooo nilisomaga philosophy ila kuiapply yote in real life ndo hapana aisee.. sasa kutana na mtu kasoma philosophy akaunganisha na sharia ajajajajajajajajajajaj mwehu kasorobo



cc Smart911
 
Ahaaa hahaaaaa. ...hebu tuache aiseee bakieni na Mungu wenu
 
Kila swali linalo mhusu Mungu linajibika ila inawezekana wengi wanashindwa kumjibu kwa sababu biblia kwenyekitabu cha zaburi,
Zaburi 14:1 imeandikwa, Mpumbavu asema moyoni Hakuna Mungu.
Kwahiyo kwavyovyote unapojibu swali lolote linaloeleza kutokuwepo Mungu unakuwa unazungumza na mpumbavu na mpumbavu ni mtu ambae hawezi kuelewa jambo
 
"men are conscious of their desire and unaware of the causes by which [their desires] are determined.."
Baruch Spinoza-Letter 58 to G. H Schuller
 
Bado sijajua usichoelewa hapo ni nini unless uwe unataka ligi

Nasisitiza I can prove the presence of God via logic, but u can't prove otherwise by using logic

Point yako na ma atheist wenzake imejikita kwenye the so called contradiction kuhusu mambo yanayomuhusu Mungu

Lakini nikueleze, u are just a human being.... Huwezi kumuelewa Mungu, kwani haeleweki kwa akili ya kibinadamu. Huwezi kumuelewa creator wako.

Hii ni sawa na gari litake kujua kuhusu binadamu, ambaye ndiye aliyelitengeneza, it is impossible braza.
 
Naona kuna watu wanadai kuwa imeshindikana kumthibitishia bwana Kiranga habari za uwepo wa Mungu hii sio kweli shida iliyopo ni utofauti wa imani Kiranga hana imani ile waliyonayo wale wanaoamini juu ya uwepo wa Mungu

Kiranga ili aamini kuwa kitu hiki kipo ni mpaka akione au akishike, akinuse nk kinyume na hapo haamini kama kitu hicho kipo kitu ambacho ni kigumu kufanyika kwa Mungu ili tumthibitishie maana katika hili Mungu wetu anasema Hakuna mwanadamu yeyote atakayemuona akaishi

Kinyume na wale ambao tunaamini kuwa Mungu yupo kwa maana hahitajiki mpk tumguse au tumuone ndipo tuamini laa maana imani kwa kadri ya maana yake nitanukuu kutoka
EBR. :11:1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Kwa hiyo tunaamini yupo japo hatujawahi kumuona maana hiyo ndio imani inavyotaka.

Lakini pili sisi tunamthibitisha Mungu yupo kupitia Neno lake yaani maandiko matakatifu kupitia humu Mungu amejifunua sana na habari zilizoelezwa humu zinathibitika kisayansi na hata kihistoria kuwa ni kweli yalitokea mfano tawala za zamani kuanzia za Wamisri, Babeli, Uamedi na Uajemi, Ugiriki nk lkn pia habari za gharika na ishara yake ya Upinde wa Mvua ambalo ni agano ambalo Mungu aliweka kuwa hataigharikisha dunia kwa maji tena haya yote yanathibitisha kuwa Mungu yupo

Lakini Kiranga kwenye hili pia haamini anadai hata biblia nayo ni contradictions

Katika hali hii huwezi kutegemea kumthibitishia kuwa Mungu yupo maana haya mambo yapo kiroho na kiimani pia. Wapo watu waliokuwa kama Kiranga tunaowasoma katka biblia ambao hawakuamini juu ya uwepo wa Mungu mfano ni Farao huyu Musa alipoenda kumuomba awaruhusu wana Waisraeli waende kumuabudu Mungu wao jangwani alimuuliza huyo Mungu ni yupi? Kwa maana nyingine hakumjua huyo Mungu wala kutambua uwepo wake na Mungu alijithibitisha mwenyewe. Mwingine ni mfalme Nebukadneza wa Babeli huyu akijawa kiburi lkn alishushwa na kufanywa kama mnyama na alipelekwa kondeni akawa kama mnyama akala nyasi miaka saba Mungu akimfunza na alipofika ktk sura ya nne ya Daniel alimkiri Mungu na uweza wake

Kwa hiyo Kiranga sio wa kwanza kupinga uwepo wa Mungu wapo wengi ila kwa muda Mungu atajithibitisha kwake na huenda siku moja akakiri kuwa kweli Mungu yupo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…