Naona kuna watu wanadai kuwa imeshindikana kumthibitishia bwana Kiranga habari za uwepo wa Mungu hii sio kweli shida iliyopo ni utofauti wa imani Kiranga hana imani ile waliyonayo wale wanaoamini juu ya uwepo wa Mungu
Kiranga ili aamini kuwa kitu hiki kipo ni mpaka akione au akishike, akinuse nk kinyume na hapo haamini kama kitu hicho kipo kitu ambacho ni kigumu kufanyika kwa Mungu ili tumthibitishie maana katika hili Mungu wetu anasema Hakuna mwanadamu yeyote atakayemuona akaishi
Kinyume na wale ambao tunaamini kuwa Mungu yupo kwa maana hahitajiki mpk tumguse au tumuone ndipo tuamini laa maana imani kwa kadri ya maana yake nitanukuu kutoka
EBR. :11:1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Kwa hiyo tunaamini yupo japo hatujawahi kumuona maana hiyo ndio imani inavyotaka.
Lakini pili sisi tunamthibitisha Mungu yupo kupitia Neno lake yaani maandiko matakatifu kupitia humu Mungu amejifunua sana na habari zilizoelezwa humu zinathibitika kisayansi na hata kihistoria kuwa ni kweli yalitokea mfano tawala za zamani kuanzia za Wamisri, Babeli, Uamedi na Uajemi, Ugiriki nk lkn pia habari za gharika na ishara yake ya Upinde wa Mvua ambalo ni agano ambalo Mungu aliweka kuwa hataigharikisha dunia kwa maji tena haya yote yanathibitisha kuwa Mungu yupo
Lakini Kiranga kwenye hili pia haamini anadai hata biblia nayo ni contradictions
Katika hali hii huwezi kutegemea kumthibitishia kuwa Mungu yupo maana haya mambo yapo kiroho na kiimani pia. Wapo watu waliokuwa kama Kiranga tunaowasoma katka biblia ambao hawakuamini juu ya uwepo wa Mungu mfano ni Farao huyu Musa alipoenda kumuomba awaruhusu wana Waisraeli waende kumuabudu Mungu wao jangwani alimuuliza huyo Mungu ni yupi? Kwa maana nyingine hakumjua huyo Mungu wala kutambua uwepo wake na Mungu alijithibitisha mwenyewe. Mwingine ni mfalme Nebukadneza wa Babeli huyu akijawa kiburi lkn alishushwa na kufanywa kama mnyama na alipelekwa kondeni akawa kama mnyama akala nyasi miaka saba Mungu akimfunza na alipofika ktk sura ya nne ya Daniel alimkiri Mungu na uweza wake
Kwa hiyo Kiranga sio wa kwanza kupinga uwepo wa Mungu wapo wengi ila kwa muda Mungu atajithibitisha kwake na huenda siku moja akakiri kuwa kweli Mungu yupo