Je! Mungu ni yule yule?

Kila mtu ana Mungu wake. Ndo maana hata mheshimiwa anasema niombeeni akiamini Mungu ni wengi, angekuwa ni mmoja wala asingetuomba maana si tayari yeye keshamuomba.
 
Kila mtu ana Mungu wake. Ndo maana hata mheshimiwa anasema niombeeni akiamini Mungu ni wengi, angekuwa ni mmoja wala asingetuomba maana si tayari yeye keshamuomba.
Watawalamara zote hutumia dhana ya Mungu kuwaunganisha watu na kuwaweka sawa ili wawe wanatawalika kirahisi.

Ukishamuaminisha mtu kwamba mamlaka ya watawala yanatoka kwa Mungu, mtu huyo kukupinga wewe mtawala itakuwa kama anampinga Mungu.

Kwahiyo dhana ya Mungu imetumiwa sana na watawala tangu enzi za Babeli, Misri,Uchina,Uyunani, Roma mpaka Uingereza na Marekani.

Karl Marx alisema dini ni kilevi cha the masses.

Munguni huyu wa contradiction ni uongo mtamu unaofariji pasipo na matumaini na kutoa machungu mengi ya maisha yasiyotabirikawala kueleweka.
 
Kaka hawa hawawez kukuelewa maana wengi wao humu toka ana mwaka1 kutwa kuuzulia kanisani na kubwia misumu ya watu wa mbali,kwa sasa wamekomaa hawa sasa kuwatoa huko inahitaji nguvu za ziada hawawez kukuelewa...

mimi nina umri wa miaka 24 kwa sasa na nilikuwa natumikia kanisa la roman cathorik...nimebatizwa huko nikapokea komnio mpka kipaimara ila niko tofaut nao sanaa kwa maana nilipokuwa na umri kama miaka nane hivi au saba huko nyuma nilipinga kuisujudia state ambayo ni roma wakati uo nakumbukuka haya makanisa ya roman tulikuwa tunayaita R.C,kifupi asa baadae nikaja gundu kirefu cha r.c...ni roman na roma nikawa naifaam kupitia chombo cha habar kimoja cjui bbc au dw dochevere ...mle kuna mbibi fulani hivi alikuwa akiiongerea sana roma.....


nikafikilii wee nkaona mmh hii roma si nchi inakuwaje tunaisadiki imani yao huku na sikuwa nawependa..mi ni mtu kuamini sana mizimu ya babu zetu wa kale nikaona isiwe tabu...sasa nilipokufikia umri mkubwa na nilikwisha pokea kipaimara nlikuwa nishajua vingi na mapungufu ya kanisa hilo hususani bibilia yao nilivibwaga vyote sikua pa1 na hao tena..


kilichonifanya nitoke huko kikubwa ni ile hadithi yao iko siku mungu atakuja kumuhukumu shetani hapa duniani,hivi kweli wakuuu tuchukulie mfano ww una banda la kuku,baati mbaya kicheche kaingia mule na una rungu au panga uwezo wa kumpiga yule kicheche asiendelee kula kuku mule unao,ivi unaweza ukawa umesimama tu kwa kumtizama na huku ukijisemea nakuacha ipo siku yako maalum,ina maana yule kicheche atamaliza kuku wote bandani kabla ya iyo siku uliyoipanga ww....


Hii dhana ya iko siku yake shetani wakati machafu yanameza kabisa mema mimk siilewi...
 
Ni bora tu hata hujaliweza hili maana ungeliweza ungesema nimekutukana.
Kuulizwa maana yake si kutoliweza. Unaweza kuulizwa kwa kuhakiki tu.

Mungu wa contradiction mlioletewa kwwnye hivyo vitabu hayupo.

Ukikubali yupo umekubali pembetatu yenye pembe sita ipo.

Habari zote hizi zina contradiction, sasa kwa nini ukubali contradiction moja na ukatae nyingine?
 
Kwa hiyo wewe habari za Mungu hazipo kabisa?? Inatisha.
 
kwanza kabisa kusema tu pembe tatu yenye pembe sita ni fallacy. huwezi kuendelea kusema pembetatu yenye pembe zingine ukawa bado uko sound. ukishasema pembe tatu hiyo body umemaliza habari zake.

nasisitiza kuwa unamuona Mungu kuwa contradiction kwa kuwa uko limited to a set of knowledge you have gained so far. you would have a shifted position if you had better knowledge which you are vehemently trying to push away. ni kama mimi nilipokuwa darasa la kwanza, logic couldn't explain how 2-5 was possible. leo hata square root ya -2 is possible to evaluate. you just need better knowledge to acknowledge that God lives! (a contradiction?? 😀😀😀) Hallelujah!!!
 
Amen
 
Unaelewa kwamba kusema kuna Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote (pembe tatu) ambaye alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usiowezekana kufanyuka mabaya lakini hakuumba ulimwengu huo akaumba huu ambao mabaya yanawezekana (pembe sita) ni sawa sawa kabisa na kusema kuna pembe tatu yenye pembe sita?

Kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Mnasema uwezo alikuwa nao. Ujuzi alikuwa nao. Uoendo alikuwa nao.

Kwa nininhakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani na hayapo kabisa?

Unaweza kujibu swali hili?
 
Hata Biblia inayosemwa kitabu kitakatifu imepangwa na maaskofu wa Mfalme Constantin wa Roma katika Council of Nicea. Hapo ndipo walipoamua kitabu ganibkiwekwe kwenye Biblia na kipi kisiwekwe.

Halafubkeo unaambiwa Biblia kitabu cha Mungu. Kumbe kitabu cha Warumi.

Sent from my LGLS992 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo wewe habari za Mungu hazipo kabisa?? Inatisha.
Tujadili hoja.

Kwa nini nikubali habariza Mungu?

Leo nikikwambia kwamba katika geometri ya Euclid kuna pembe tatu yenye pembe sita utakubali?
 
Tujadili hoja.

Kwa nini nikubali habaribza Mungu?

Leo nikikwambia kwamba katika geometri ya Euclid kuna pembe tatu yenye oembe sita utakubali?

Sent from my LGLS992 using JamiiForums mobile app
Kwa kitu ambacho sikijui siwezi kukataa wala kukubali, kama uwezekano wa kujiridhisha upo nitaenda nijiridhishe kwanza. Labda nikuulize, wewe unaamini ulitokea wapi? Aliyekuzaa naye alitokea wapi? Nini chanzo cha viumbe??

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app
 

ulielewa niliposema kuwa Mungu hakuumba wa haumbi automatons? unafahamu automaton ni kitu gani?
 
Unapokuwa unajiridhisha, unatumia msingi gani kujiridhisha?

Kama kila kitu ni lazima kiwe na chanzo, Mungu chanzo chake ni nini? Akiwa na chanzo naye atakuwa Mungu bado?

Kama Mungu hana chanzo, huoni kwamba ushafungua mlango wa kuvunja kanuni ya "vyote lazima viwe na chanzo"?



Unaelewa kwamba dhana nzima ya muda kutiririka, mwanzo na mwisho, kuelezewa bila muktadha, ni upotofu unaotokana na ufinyu wa mawazo ya kibinadamu na kiasili?

Unaelewa punje ya mwanga inayokwenda kwa spidi ya mwanga haina muda, muda uliopita, ujao na uliopo vyote vimefunganishwa pamoja kwa mujibuwa punje hii?

Unaelewa hayonimambo yameandikwa kuanzia miaka100iliyopita na Albert Einstein katikaRelativity, na kuwa proved over and over again?

Unaelewa katika Quantum Physics,hususan kwamuktadha wa Copenhagen, habari nzima ya chanzo na matokeo ya chanzo inaweza kuvunjwa kiasi kwamba "tokeo la chanzo likatokea kabla ya chanzo" ?
 
ulielewa niliposema kuwa Mungu hakuumba wa haumbi automatons? unafahamu automaton ni kitu gani?

au·tom·a·ton
ôˈtämədən,ôˈtäməˌtän/
noun
  1. a moving mechanical device made in imitation of a human being.
    synonyms: robot, android, cyborg, droid, bot
    "assembly-line automatons"
    • a machine that performs a function according to a predetermined set of coded instructions, especially one capable of a range of programmed responses to different circumstances.
    • used in similes and comparisons to refer to a person who seems to act in a mechanical or unemotional way.
      "she went about her preparations like an automaton"

Ukiamini kwamba Mungu yupo, na ana nguvu hizo mlizompa, mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote:-

Mungu wenu kwa mamlaka mliyompa tayari kashaumba automatons.

1. Mnasema mtu kaumbwa kwa mfano wa Mungu.Imitation.acentral characteristic of automatons.

2.Kaumba viumbe ambao hawana control watazaliwa kwa mwili gani (watu, wanyama , wadudu) wanajikuta tu wamezaliwa. Lack of control and predefined contsrains are central characteristics of automatons.

3.Kaumba viumbe ambao hawana control juu ya muda, muda unaenda mbele tu,haurudi nyuma, kwa hili viumbe ni automatons. Pre-programmed to exist in a universe where they can't go back in time.

4.Kaumba viumbe ambao hawawezi kutoka nje ya ulimwengu aliouumba. Kwa hili viumbe ni automatons. Again, predefined contrains and boundaries.

5. Kunamambomengi sana yako controlled na genes, kuanziamagonjwa mpaka tabia.Kwa hili huwezikusemaviumbe si automatons.

6.Ukisema watu wanamjua Mungu kwa neema tu na si kwa uwezo wao, hapo maana yake watu ni automatons.

7.Ukisema Mungu anajua yanayokuja, na anachojua lazima kiwe, basi huwezi kuepuka kwamba watuni automaton.

8. Watu ni lazima wafariki, kwahili watuni automatons.

9. Watu wamejikuta wamezaliwa bilakuulizwa na kukubali kuzaliwa. Kwa hiloni automatons.

10. Watu hawana uwezo wa kubadili mifumo ya nguvu asili kama mizunguko ya sayari na misimu, kwa hiloni automatons.

Kama unaamini Mungu yupo.

Swali langu la msingi hujalijibu.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambaohaunamabaya na watu wana uhuru wa kuchagua mazuri tu?

Kwa sababu,hata ulimwengu huu mnaosema Mungu katupauhuru wa kuchagua mazuri na mabaya,tunaona kuna mipaka ya kuchagua.

Hatuwezi kurudi nyuma katika muda, hatuwezikuepuka kufa,hatuwezi kuchagua tuzaliwe wapi,kwa wazazi gani etc.

Kwa hiyo habari ya kwamba tuna uhuru wa kuchagua mema na mabaya ina walakini, kwa sababu uhuru wetu una mipaka.

Sasa kama kweli ulimwengu umeumbwa na Mungu, na yeye ndiye kawekamipaka ya kinachowezekana na kisichowezekana (mfano, muda kwenda mbele tu kwa watu, usirudi nyuma), kwa nini hakuwekamipakakwamba mabaya yasiwezekane, yawezekane mazuri tu?

Swali hili linakuwa na maana sana ukizingatia.

1. Mungu huyu mnasema alikuwa na uwezo wote wa kuumba hivyo.
2. Mungu huyu mnasema alikuwa na ujuzi wote wa kuumba hivyo.
3.Mungu huyu mnasema alikuwa na upendo wote wa kuumba hivyo.

Kwa ninihakuumba hivyo?

Kwaninihakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Ukijibu hakutaka automaton, nitakuuliza,hivi tetemekola ardhi linapotokea, jambo ambalo halihusiani na uamuziwa watu kuchagua mazuri na mabaya, halafu watto wachanga maelfu wakafariki ikatili kwa kuzikwa hai, hapo Mungu anakataa automaton gani?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi hayatokei?

Kama hakushindwa, je ni kweli ana upendo wote anapoachia viumbe wake wateseke sana?

Kama alitakakuumba hivyo, lakini hakuweza, je nikweli ana uwezo wote?

Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo woteyupokweli?

Au ni hadithi tu?

Mbona dunia tunayoishi inam contradict?
 

Mungu hajabadilika tabia, kwa sababu hayupo. Kitu ambacho hakipo hakiwezi kubadilika tabia.

Watu walioandika hivyo vitabu ndio waliobadilika tabia, kwa sababu vitabu vimeandikw akwa muda uliovitenganisha kwa maelfu ya miaka.Ni wazikulikuwa na mabadiliko katika waandishi wa mwanzona wa injili.

Ukichukua vitabu vinavyoitwa "vya Musa" ukahesabu miaka na vizazi mpaka kufikia vitabu vya Injili vya miaka 2000 iliyopita, kuna wasomi wa Biblia wamefanya mahesabu wakakuta kunamiaka kama 4,000 kutoka stories za mwanzo ziandikwe mpaka alipozaliwa Yesu na habari za injili zilipoandikwa. Hii ndiyo sababu kuna watu wanasemadunia ina miaka 6,000. Wanahesabu kuanziakitabu cha mwanzo mpaka sasa.

Kwa hiyo, kwa sababu vitabu hivi si vya Mungu (Mungu hayupo),na vimeandikwana watu tu, ni lazima tuone tofauti zinazoakisi tofauti katika jamii na tamaduni vilipoandikwa.

Ndiyo maana unaona tofauti hiyo.

Ukitakakujua zaidi kwamba Bibliasikitabu cha Mungu, ni kitabu cha watu tu, angalia contradictions na inconsistencies zilizopokatika Biblia nimeziweka hapa awali.

Link hii hapa Bible Inconsistencies - Bible Contradictions

By the way, Biblia licha ya kuwa sikitabu cha Mungu, na kuwa ina habari za kijinga nyingi sana, bado piaina mafunzomazuri mengisana pia.
 

hapa umenielewesha kuwa pamoja na kuweka definition ya automaton umeshindwa kujua umeweka nini. vyote ulivyoviweka hapa haviusiani na mambo ambayo mwanadamu ANAYAFANYA kwa sababu kawa PROGRAMMED na Mungu. tunapozungumzia automation hapa tunazungumzia the mind that pushes a man to CHOOSE. those faculties ambazo umezitaja hapo hazihusiani na power of choice in what is available to that man.

sasa kwa sababu umeshindwa hata kung'amua automaton ni kitu gani pamoja na kuisoma kote huko, nilikwambia huko nyuma wewe huna uwezo hata wa kugundua hata pale nitakapokuthibitishia kuwa Mungu yupo. Akili hiyo huna. unazunguka tu na realm yako iliyofungiwa kwenye logic ulizojifunza kwa kusikia kilichotokea ndani ya hii miaka 6000 ya uwepo wa dunia wakati Mungu amekuwepo tu from the eternity.

ungejua kuwa anaowaumba wana power ya kuchagua chochote within their reach katika hii miniature scenario ungefahamu kuwa Mungu si wa kulazimisha vitu vifanya kama anavyotaka ingawa anaweka matokeo ya kufanya uchaguzi huo. na hiyo ni kanuni yake ambayo hata yeye mwenyewe haivunji.

we unanichosha tu. hujui unachozungumza unaleta usiyoyajua hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…